Kwanini bado usipuuze Maombi?

Kwanini bado usipuuze Maombi?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Bado maombi yana nguvu. Puuza wanaopuuza maombi.

Maombi Yanaweza kugeuza maamuzi ya Serikali na viongozi wakubwa wa nchi. Mfalme wa Iran Koreshi, Altashasta na Dario walijikuta wanaendeshwa na maombi ya wakina Danieli, Nehemia, Ezra licha ya ukatili wao.

Maombi yalimtoa Petro Gerezani.

Maombi yalizuia mvua miaka 3, na kuileta kwa neno la Eliya.

Maombi yalimfanya mtu mmoja Ibrahim aishi kama jeshi, na hakuna aliyemuweza.

Maombi yalimfanya Yakobo apite katikati ya maadui zake bila kuguswa.

Maombi yanaangusha ngome

Maombi yana nguvu ya kupasua bahari.

Maombi maombi maombi

Usipuuze maombi.

Ni hayo tu

Mtumishi Matunduizi
 
Maombi hayatengenezi SGR
 
Tanzania tunaweza kuomba umaskini ukaisha?
Ndio. Na hauna maombi ya kitaifa yamewahi kufanyika kuukataa umasikini.
Ila korona tuliikataa na kwa maombi bila ssyansi ilitoka.

Majibu ya maombi ni ya ajabu. Sio muujiza tu, hata kuonua kiongozi. Israel walipoteseka sana Mungu alimuinua Musa aliyelelewa aje kuwa farao, akawa kiongozi aliyewavusha bahari.
 
Maombi huenda na vitendo. Bila kuwa na ari ya kutaka kukamilisha jambo huwezi toboa.

Yani ni sawa na uwe na software bila kuwa na hardwares. Huwezi kufanikisha chochote.

Maombi + vitendo = Matokeo
Ni sahihi.
Maombi hayat4nganishwi na wajibu.
Maombi hutoa stamina ya kutekeleza hata yasiyowezekana
 
Kuna wanaobeza thread hii ya maombi msichanganye mambo ya ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili chanzo cha mambo mengi ni ulimwengu wa roho tatzo wengi hamna elimu na haya mambo
Ni kweli. Lazima waje ila ni kutafuta hekima ya kuwapotezea
 
Maombi hayatengenezi SGR
Yanaweza.
Bila amani, ambayo ni matokeo ya Maombi hizo reli zinaweza kuobiwa zote na kuuzwa vyuma chakavu china.

Au mtu mmoja akabugia pesa yote na mke wake ukabaki na mchoro tu. Mambo yanaenda kwa sababu wako watu wanaomba mkuu.
 
CHADEMA wanaweza kufanya maombi kuindoa CCM madarakani??
Wao sio chama cha maombi, ni chama cha siasa. Waje na kitu bora ambacho kama mbadala wa hiki tunachokiona.

Pia sio lazima mbadala wa CCM iwe chadema. Inaweza pia kuwa CCM iliyobadilika au Mungu akafumua wote wawili akaleta kitu kipya.
 
Neno la MWENYEZI MUNGU ni upanga waefeseo6:17

Shida ya vijana wa leo wametanguliza mzaha sana na kufuata mkumbo

Alafu wanataka waombe kwa siku moja na kufanikiwa
 
Neno la MWENYEZI MUNGU ni upanga waefeseo6:17

Shida ya vijana wa leo wametanguliza mzaha sana na kufuata mkumbo

Alafu wanataka waombe kwa siku moja na kufanikiwa
Wanawasilikiza wazungu waliofeli maisha.
 
Yanaweza.
Bila amani, ambayo ni matokeo ya Maombi hizo reli zinaweza kuobiwa zote na kuuzwa vyuma chakavu china.

Au mtu mmoja akabugia pesa yote na mke wake ukabaki na mchoro tu. Mambo yanaenda kwa sababu wako watu wanaomba mkuu.
Amani hailetwi na maombi wewe, kwani huko Lebanon , Ukraine, Urusi, Syria hakuna wanaofanya maombi?
 
Amani hailetwi na maombi wewe, kwani huko Lebanon , Ukraine, Urusi, Syria hakuna wanaofanya maombi?
Wakikubaliana wote inakuja.

ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

2Nyakati 7:14
 
Back
Top Bottom