matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Maombi hayatengenezi SGRBado maombi yana nguvu. Puuza wanaopuuza maombi.
Maombi Yanaweza kugeuza maamuzi ya Serikali na viongozi wakubwa wa nchi. Mfalme wa Iran Koreshi, Altashasta na Dario walijikuta wanaendeshwa na maombi ya wakina Danieli, Nehemia, Ezra licha ya ukatili wao.
Maombi yalimtoa Petro Gerezani.
Maombi yalizuia mvua miaka 3, na kuileta kwa neno la Eliya.
Maombi yalimfanya mtu mmoja Ibrahim aishi kama jeshi, na hakuna aliyemuweza.
Maombi yalimfanya Yakobo apite katikati ya maadui zake bila kuguswa.
Maombi yanaangusha ngome
Maombi yana nguvu ya kupasua bahari.
Maombi maombi maombi
Usipuuze maombi.
Ni hayo tu
Mtumishi Matunduizi
😂😂😂atakwambia NDIOCHADEMA wanaweza kufanya maombi kuindoa CCM madarakani??
Ndio. Na hauna maombi ya kitaifa yamewahi kufanyika kuukataa umasikini.Tanzania tunaweza kuomba umaskini ukaisha?
Ni sahihi.Maombi huenda na vitendo. Bila kuwa na ari ya kutaka kukamilisha jambo huwezi toboa.
Yani ni sawa na uwe na software bila kuwa na hardwares. Huwezi kufanikisha chochote.
Maombi + vitendo = Matokeo
Ni kweli. Lazima waje ila ni kutafuta hekima ya kuwapotezeaKuna wanaobeza thread hii ya maombi msichanganye mambo ya ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili chanzo cha mambo mengi ni ulimwengu wa roho tatzo wengi hamna elimu na haya mambo
Yanaweza.Maombi hayatengenezi SGR
Wao sio chama cha maombi, ni chama cha siasa. Waje na kitu bora ambacho kama mbadala wa hiki tunachokiona.CHADEMA wanaweza kufanya maombi kuindoa CCM madarakani??
Wanawasilikiza wazungu waliofeli maisha.Neno la MWENYEZI MUNGU ni upanga waefeseo6:17
Shida ya vijana wa leo wametanguliza mzaha sana na kufuata mkumbo
Alafu wanataka waombe kwa siku moja na kufanikiwa
Amani hailetwi na maombi wewe, kwani huko Lebanon , Ukraine, Urusi, Syria hakuna wanaofanya maombi?Yanaweza.
Bila amani, ambayo ni matokeo ya Maombi hizo reli zinaweza kuobiwa zote na kuuzwa vyuma chakavu china.
Au mtu mmoja akabugia pesa yote na mke wake ukabaki na mchoro tu. Mambo yanaenda kwa sababu wako watu wanaomba mkuu.
Wakikubaliana wote inakuja.Amani hailetwi na maombi wewe, kwani huko Lebanon , Ukraine, Urusi, Syria hakuna wanaofanya maombi?