Mzalendo_Mwandamizi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2007
- 1,117
- 4,772
Kwa wanaofuatilia masuala ya diplomasia, wanatambua kuwa mara nyingi balozi za Marekani, Uingereza, Canada na Umoja wa Ulaya nchini Tanzania huwa mstari wa mbele kutoa matamko pindi viongozi wa upinzani wanapokamatwa. Kumbukumbu ya karibuni ni balozi hizo zilipoijia juu serikali ya Magufuli kufuatia kukamatwa kwa Marehemu Maalim Seif na viongozi mbalimbali waliokuwa wakipinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Hata hivyo, leo ni wiki kamili tangu Mbowe akamatwe na zaidi ya masaa 48 tangu afunguliwe mashtaka ya ugaidi lakini hakuna ubalozi wowote uliotoa tamko.
Kuna watakaosema "mbona kamati ya bunge la Marekani ilitoa tamko?" Actually, tamko lao lilitolewa kabla polisi hawajamtuhumu Mbowe kuhusu ugaidi.
Angalizo: Matamko ya balozi za wenzetu hao hutokana na ushauri wa mashirika yao ya intelijensia katika nchi husika. Ubalozi wa Marekani Dar una bureau ya CIA, ya Uingereza ina ofisi za MI6, Canada nao wana maafisa wao wa CSIS, na EUINTCENT kwa EU.