Kwanini Balozi za Marekani, Uingereza, EU na Canada hazijatoa tamko lolote kuhusu kukamatwa Mbowe?

Kwa vile suala liko mahakamani na kwa vile huwa wanaheshimu the rule of law, nadhani wanasubiri waone mwelekeo wake.
 
kwasababu wao ndio waliwaambia watanzania ugaidi wa Mbowe. Majasusi wao ndio wametoa taarifa za Mipango ya huyo Gaidi
 
Samia alipoingia madarakani amekuwa fair sana kwa wapinzani, lakini walitaka mpanda kichwani na kumdharau kama mwanamke. I think it is a message, 'msinichezee, mimi ni Amir jeshi'. Kwa sasa watamuheshimu, kumfungulia mashtaka ya ugaidi Mkuu wa upinzani nchini, inahitaji ujasiri.
 
.mkuu ni wewee? Siku hizi umwbasilika sana. Umerogwa nini?
Ninaishi kwenye realities. Siwezi kuendelea kupinga Serikali inapofanya mambo mazuri. Nilimpinga Mwendazake 24/7 kwa miaka mitano kutokana na alivyokuwa ana abuse rule of law, Katiba, Raslimali za Taifa na double standard kwenye maamuzi.

Kwa miezi 4 ya Rais SSH tumeona uhuru wa maoni ukirudi, TAKUKURU wakifuta kesi za kubambikiza, Serikali ikichukua hatua kujikinga na COVID-19, Diplomasia ya kimataifa ikiboreka, wawekezaji wakirudia nchini. Hata ajira kwa waalimu na sekta ya afya zikitolewa japo kidogo.

Hawa CDM Rais alisema atakutana nao muda mwafaka baada ya kukutana na makundi mengine, wao wakataka aanze na wao kwanza, kwenye Katiba alisema subiri nipange uchumi kwanza wao hawataki wanasema Katiba kwanza, akaruhusu mikutano ya ndani ila mikutano ya hadhara akasema isubiri afanye review wao wakasema hatuwezi kubembeleza.

Dharau ya Mbowe na Lissu ni ya kijinga dhidi ya Rais, hakuna mtu atawasikia
 
Ni sehemu gani kwenye katiba pamekataza mikutano ya hadhara?
Au ni sheria gani inakataza watu wasikutane kujadiri issue za katiba mpya.?

Kama SSH alikataa kuonana nao na akaruhusu mikutano ya ndani, kwani kongamano walilopanga kufanya Mwanza lilikua ni mkutano wa hadhara na sio mkutano wa ndani?

Nimekuuliza tu mkuu nataka unijibu
 

Kwanini Balozi za Marekani, Uingereza, EU na Canada hazijatoa tamko lolote kuhusu kukamatwa Mbowe?​


Marekani, EU, Canada etc walikuwa na Mission eradicate Magufuri and his Economic policy. Mpango was done successful using akina Mbowe na Takata zingine. Mpango ulitumia gharama baada ya mpango kukamika nani anataka kuendelea na vita isiyo na Adui kwa manufaa ya matumbo ya vibaraka. Mbwa wa nini wakati hakuna Adui. Hata Libya, Tunisia, Afghanistan,Iraq na kwingineko baada ya mpango wa kumuua OSAMA kufanikiwa wameachwa kama yatima wapambane na hali yao. CHADEMA na Mbowe wametumikia Kafiri. Akili za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Hapa ndio makosa nayaona, CHADEMA ni taasisi haiwezi kuacha kufanya daily operations zake be it vikao, makongamano, mikutano eti kisa uchumi unajengwa. If that's the case vilabu vya soka, makanisa, kumbi za starehe zifungwe ili kupisha uchumi kujengwa!!!

CCM mbona wanafanya mikutano ya ndani na nje ila hatujasikia wakiambiwa wapishe kwanza mama ajene uchumi? Au mkutano wa ndani ukifanywa na CHADEMA unakua na madhara kiuchumi???

Maadam wanafanya passive politics sio za kuandamana au kushika bunduki sioni kama kuna hasara yoyote. Kikwete pamoja na failures zake nyingi mbona wapinzani walikua wanaongea sana na hatukuona wamekwamisha uchumi usimaintain 7%?? Kipindi kile katiba mpya, sensa, Uchaguzi n.k vilienda pamoja lakini hatukuona retaliation kama hii???

Ni kukosa hekima tu, JPM alifanya mengi say miundombinu lakini kilichomharibia ni kushindwa uongozi wa compromise na wanaokua na maoni kinzani. Mama Samia alianza vizuri ila kwa kukosa busara ndogo tu popularity imeporomoka, na ikitoka ripoti ya CAG ndio tutamzika rasmi kwenye siasa za TZ.
 
Sema wewe.
 
Najuwa RC wa Mwanza ndiyo ana majibu ya maswali yako mimi siwezi kujuelekeza huko.
Ila nakuhakikishia kuwa kwa akili za Mbowe na Tundu Lissu ambazo zimekosa hekima na busara haziwezi kuja kuitoa CCM madarakani.

Ila kama unataka kutumika kuwarengenezea mkate wao basi kesho nenda na wewe Mahakama ya Kisutu
 
Katika siku 100 za kwanza CDM walikuwa ndiyo wanufaika wakuu wa uongozi wa Samia mpaka humu ndani kuna thread inasema "Je Samia ni CHADEMA".

Na wakamsifia kuwa anaupiga mwingi. Kama Mbowe angekuwa na busara kidogo alipaswa amu handle Rais SSH kwa namna alivyo. Yaani kama mtu ni brutal na wewe unakuwa brutal. Kama mtu ni muungwana unampinga kiungwana. Wame my approach Mama kwa kiburi na dharau sana mpaka wanataka wampangie ratiba ya lini akutane na CDM.

Hiyo miscalculation imeirudisha CDM miaka 10, take it from me.
 
Wacha uboya kijana kwani ujui mama kesha uza nchi siku nyingi makinikia yanakenda kama zamani sasa hao mabolozi watake nini tena
 
Shida ilianza alipokataa kukutana nao..... Mbona Kenyatta alikutana na Odinga mpka leo kumetulia huko west na coast bila hivyo ingekua maandamano kila leo.

Angewaita ili awaeleweshe vision yake mbona wangekua wapole ila sasa wao kawadharau so hawakua na choice kma chama zaidi ya kudeclare war.

Na nikwambie tu watu pekee waliobaki kumsupport mama ni CHADEMA pekee.... We ngine wote hasa wana CCM bado wanasumu za JPM so wanamuona msaliti.

Trust me 2025 utakua mgumu kwake, hasa ndani ya chama. Na akitoka nje atakutana na radical opposition. Kma CHADEMA wata ally na Sympathizers wa old regime naona anguko la Samia.

You can take it to the bank
 
Patience, wisdom ndiyo tatizo la akina Mbowe. Mbona Rais SSH ni very friendly, approachable na muungwana??

Kumbuka kwenye Chama chake walikuwa wanamchukulia vipi anapofanya yale maamuzi ya akina Sabaya.

Huwezi kumpangia Rais mwenye appartus zake ratiba kama unawapangia wale BAWACHA. She is Pesident if URT.

Mkitaka kuwasaidia CDM wakosoeni, lakini kama mnaunga mkono hata huo ujinga wa Mbowe na Lissu chama kitapotea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…