Du! Vinuka mkojo ndio nini!!Mi napokwenda bank nikikutana na CC mwanaume mwenzangu at least huwa na breath a sigh of relief lakini si vile vinuka mkojo vilivyomaliza form six juzi na vi simu vyao vya mchina!
CRDB nadhani kwa sasa wamepata kiburi baada ya kuwa na wateja wengi mno...., ni masharobaro wa kufa mtu!
Jambo la kwanza linaloniboa sana mimi ni kitendo cha kuwa na vibanda 6 vya tellers, halafu unakuta cashiers wako wawili tu, vibanda vingine viko empty!...Natamani niingie kule ndani wanakozunguka zunguka na kuwakwida kuwapeleka kwenye vibanda vya cashier.
Hata cashier anayekuwa kibandani unakuta anajigeuzageuza tu, wala hajali fioleni iliyo mbele yake!
Kwakweli dawa ni kufunga account tu!
Du! Vinuka mkojo ndio nini!!
Wasichana wenye umri mdogo ambao hawajafahamu namna ya kusafisha sehemu zao baada ya kutoka haja ndogo!
Back to the topic:
Huduma mbovu kwa Tanzania ni kila sehemu, hata haya Makampuni ya "Kigeni" ni vile vile tu!
Kwanini?
1. Waajiriwa wengi wamepewa kazi kwa "favour" au "rushwa"!
2. Mishahara ni midogo kiasi kwamba waajiriwa wengi ni "mguu nje, mguu ndani"
3. Watawala wengi ni mbumbumbu
Nimesikitishwa sana na Huduma zinazotolewa na bank za hapa nchini, huduma zao ni mbovu zisizojali wateja na wafanyakazi wa bank wanadharau utafikiri huduma hiyo ni ya bure kumbe unalipia all transaction na isitoshe pia kuwa mishahara yao inatokana na wateja kuweka au chukuwa pesa. Isitoshe ukiingia bank utamuona mfanyakazi wa bank anachezea kasimu kake kana kwamba wameajiriwa kuchezea simu. Ukiomba kukutana na Meneja ili utoe malalamiko utazungushwa na kuulizwa maswali utafikiri umekamatwa na polisi kwa kosa la kuua. Kwa nyie Mameneja na vibaraka wenu mnaofanyakazi za bank kuweni wastaarabu kwa kuwasiliza wateja. Ninavyojua mimi kuwa Bank hairuhusiwi kuzungumza na simu wala kuchezea simu ikiwa na maana kuwa kama mtu amekuja kuchukuwa pesa halafu kama unawaambia vibaka nje kuwa mtu amevaa ngu rangi hiyo amechukuwa kiasi hicho, kutumia simu Bank ni uhalifu hasa kama mfanyakazi wa ndani. Kwa kweli sifurahiwi na huduma zenu.
KCB hawana tofauti, nishaenda pale downtown nyuma ya PPF tower kuangalia michongo yao ili nifungue akaunti nikakuta wateja wanayeyushwa eti hela zipo Mlimani City Branch tukitaka twende huko, watu wakawapaka wakaanza.Nenda KCB wako kiKENYA KENYA!
HAHAHA...hapo kwenye bold...Kiherehere chao....ndo maana wawekezaji wanaajiri watu toka nje, wabongo customer care zero kabsaa! nilienda deposit pesa nmb lile tawi pale karibu na bima(NIC) posta, kitu kilikuwa km m10 kwa vile nilikuwa nimezoea bnk binafsi sikuwaza kwamba ntaulizwa maswali, khaaaa!!! tailor akaniuliza eti hizi pesa umetoa wapi! nikapandwa na hasira sababu nilishasota karibu saa nzima kwenye foleni, nikamwuliza vipi mmeibiwa kiasi km hiki mnatafuta mwizi? akajichekesha eti sio hivyo benkii ukiweka pesa nyingi lazima uulizwe zimetoka wapi. nikamwambia wewe nikikuambia nimeokota kwa vile ni sababu utaridhika! akasema basi yaishe! wanakera mnoooooo jamani sijui tuingie na viboko mle!
Kweli customer service kwenye mabenki mengi ni mbovu hasa lugha zinazotolewa na watoa huduma utafikiri amelazimishwa kufanya kazi kumbe kaiomba mwenyewe na wengine hata uchi wametoa kupewa hizo kazi