Umewahi kukumbana na tabia hii; uko ktk foleni mbele ndo unalifikia dirisha, mtoa huduma wa benki anamwona rafiki yake ktk foleni nyuma yako, anachukua karatasi/kadi yako anaishika,kisha anamwita rafiki/mshikaji wake toka nyuma yako anamhudumia halafu ndo anarudi kwako, anakuuliza swali, ehe kaka unataka huduma gani vile? Bongo si mchezo.
Siku moja nilikuwa huko wilayani, nahitaji kumwona meneja wa benki saa tatu asubuhi,naambiwa kenda kunywa chai, nilisubiri hadi saa tano, jamaa ndo anarudi ofisini. Kukoroma sikuweza kwa sababu kule wilayani huna mbadala, hasa hizi wilaya zetu za pembeni mwa nchi.
Huduma ni mbovu hadi kulipia kodi nako taabu, mpaka uzungushwe.