Kwanini Bara la Afrika linajulikana kama sehemu ya kwenda kuiba mali?

Status
Not open for further replies.

MAKA Jr

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2016
Posts
267
Reaction score
209
Ni kwa nini duniani kote inajulikana kuwa Bara la Afrika ni sehemu ya kwenda kuiba au kuchukua vitu pasipo na wenyeji wake kuonyesha kujitetea?

Hii hali inazidi kuwa kubwa kadri siku zinavyosonga. Tulifikiri uhuru utaondoa hili, lakini wapi.
Tulifikiri Elimu na teknolojia vitaondoa hili, lakini wapi.
Kila hatua ambayo Afrika inapitia ni hatua ya kuzidi kurusu UTAWALA MPYA WA BARA LA AFRIKA. Ni kwa nini na ni nini kifanyike ili kuondoa hili?
 
Attachments

  • 1728645797771.jpg
    1728645797771.jpg
    456.2 KB · Views: 4
Ni kwa nini duniani kote inajulikana kuwa Bara la Afrika ni sehemu ya kwenda kuiba au kuchukua vitu pasipo na wenyeji wake kuonyesha kujitetea?

Hii hali inazidi kuwa kubwa kadri siku zinavyosonga. Tulifikiri uhuru utaondoa hili, lakini wapi.
Tulifikiri Elimu na teknolojia vitaondoa hili, lakini wapi.
Kila hatua ambayo Afrika inapitia ni hatua ya kuzidi kurusu UTAWALA MPYA WA BARA LA AFRIKA. Ni kwa nini na ni nini kifanyike ili kuondoa hili?
Kwakua watu wake ni empty headed
 
Chanzo ya hivyo vyote ni colonialism, wazungu walivyo kuja kututawala walitufanya tuwe dependents kwao kwa kila engo ya maisha kiuchumi, kisiasa na kijamii, hivyo hata baada ya uhuru hatukuweza kujisaidia sisi kama Sisi kwa sababu tulikuwa bado tupo duni kiuchumi na hilo halitakuja kubadilika labda tu viongozi wa Afrika wawe wazalendo.
 
Weak institution(s) and corrupt minded politicians....

Ni Africa pekee wanasiasa ni matajiri kuliko Wafanyabiashara.. nenda Kenya... Na nchi moja ya Afghanistan naona wameanza kuiga huo mchezo..

Maduka ya Wanasiasa Africa ni Office zao.. na taasisi zetu bado sio imara sana...

Kama huamini nenda India au China karungue duka la mangi uone .. ila huku hewala... na mitaji wanapewa
 
Chanzo ya hivyo vyote ni colonialism, wazungu walivyo kuja kututawala walitufanya tuwe dependents kwao kwa kila engo ya maisha kiuchumi, kisiasa na kijamii, hivyo hata baada ya uhuru hatukuweza kujisaidia sisi kama Sisi kwa sababu tulikuwa bado tupo duni kiuchumi na hilo halitakuja kubadilika labda tu viongozi wa Afrika wawe wazalendo.
Kwa ufupi tu wewe muafrika hauko huru, uhuru ulionao ni wa bendera tu basi

Na wewe utaendelea kuwa mtumwa au binadamu wa daraja la pili(kiakili na kiuchumi) hapa duniani, na mtu wa daraja la kwanza(mzungu) anakutumia wewe kukiibia kizazi Chako(rasilimali) hili yeye aende akatengeneze maisha ya kizazi Chake.

Ndio maana aina hii ya viongozi tunaowaona leo hii wanaopenda Rushwa na ufisadi wasiokuwa na vision Wala akili ya kuleta maendeleo hapa Afrika, ndio hao hao hata ikifika mwaka 2050 utawaona, wakati huo wenzetu mwaka huo huo watakuwa na akina Benjamin Netanyau wengine na wenye akili zile zile kubwa kama za Hawa akina Netanyau wa Sasa hivi, na kama kawaida watakuwa wanawapa misaada na kuwapangia nini Cha kufanya viongozi wetu wa kiafrika kama tu ilivyo kwa Sasa hivi
 
Ni kwa nini duniani kote inajulikana kuwa Bara la Afrika ni sehemu ya kwenda kuiba au kuchukua vitu pasipo na wenyeji wake kuonyesha kujitetea?

Hii hali inazidi kuwa kubwa kadri siku zinavyosonga. Tulifikiri uhuru utaondoa hili, lakini wapi.
Tulifikiri Elimu na teknolojia vitaondoa hili, lakini wapi.
Kila hatua ambayo Afrika inapitia ni hatua ya kuzidi kurusu UTAWALA MPYA WA BARA LA AFRIKA. Ni kwa nini na ni nini kifanyike ili kuondoa hili?
Sijasoma mada yako. mbali ya kichwa cha mada yenyewe.
Jibu ni rahisi.
Kwa sababu kuna wajinga wengi sana, hasa viongozi wake, wengi ni wapumbavu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom