Kwanini Bashiru anashambuliwa na anatetewa? Kuna mahali tunapishana: Look!

Kwanini Bashiru anashambuliwa na anatetewa? Kuna mahali tunapishana: Look!

Tatizo la viongozi wa nchi hii ni unafki na kujipendekeza.

Bashiru ni miongoni mwa wanafki na watu walioishi kwa kujipendekeza wakati wa utawala wa kayafa jiwe.

Kiongozi aina ya bashiru ni ngumu sana kumuamini akisemacho kutokana na historia yake ya nyuma.

Ni mbabe mpenda sifa mvunja sheria muunga mkono matendo ya hovyo ya jiwe mpenda vyeo asiyerizika nk

Haya yote yana ushahidi wala asingiziwi.

Mtu kama huyu akijifanya kuhoji jambo sio kwa sababu aba uzalendo na ufia nchi sana.

Hapana ni kwasababu ya kukosa fursa na recognition tu kwenye utawala huu.

Akipewa fursa wala hutamsikia akinyanyua mdomo kuhoji anayoyahoji sasa hivi.

Kuna utawala uliokuwa unamiminiwa sifa za kipuuzi kama utawala wa jiwe?

Mpaka kunyesha kwa mvua na kupatwa kwa jua alikuwa akisifiwa magufuli ndiyo msababishaji mbona hatukumuona akikemea hayo?

Ni ngumu sana kwa nchi kupiga hatua kwa kutegemea watu wanafki na wachumia tumbo aina ya bashiru.

Tunahitaji watu ambao wanasimamia ukweli wa mambo na sio kumsimamia kiongozi aliyo madarakani.

Mtu kama Assadi ni miongoni mwa watu ambao angalau atakachosema leo awe madarakani au asiwe ni hiko hiko atakachosema kesho awe madarakani au asiwe.

Watu kama hao ndiyo tunawahitaji kwa wingi nchini.

Sio wachumia tumbo kama bashiru na polepole.
 
Back
Top Bottom