Thom Munkondya
Member
- Feb 8, 2019
- 94
- 124
Kwa nini bei za viwanja vilivyopimwa ziko juu sana nchini Tanzania?
Na Thom munkondya.
Viwanja vilivyopimwa vinauzwa bei ya juu sana kwasababu upimaji ni gharama sana. Ukiona sehemu viwanja vilivyopimwa vinauzwa bei ya chini basi ujue hivyo viwanja havijapimwa ila vimetangazwa kama vimepimwa ili kuvutia wengi.
Mwaka 2003 kuna mbunge alilalamika bungeni juu ya bei kuwa kubwa ya viwanja vilivyopimwa vilivyokuwa vinauzwa na serikali,serikali ilijibu kuwa bei ni kubwa kwasababu ya gharama za upimaji. Hili limeandikwa kwenye gazeti la Daily News la 10/4/2003 ukurasa wa pili.
Miradi mingi sana ya viwanja nchini Tanzania inatangazwa kuwa viwanja vimepimwa lakini ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya miradi ya viwanja inauzwa ilihali viwanja havijapimwa kwasababu kampuni nyingi haziwezi kumudu gharama za upimaji ndiyo maana watu wengi wamenunua viwanja walivyoambiwa vimepimwa lakini mpaka sasa hawana hati miliki au wanasumbuliwa kupata hati miliki. Umenunua kiwanja kilichopimwa je una hati miliki..?
Je unajua kutambua kiwanja ambacho kimepimwa? Je unajua kutambua ramani halali inayotambuliwa na wizara ya ardhi ya kiwanja kilichopimwa..? Je unajua ukinunua kiwanja ambacho hakijapimwa huwezi kupata hati miliki? Je unajua ukinunua kiwanja ambacho hakijapimwa ila umedanganywa kuwa kimepimwa unaweza kuwa umenunua eneo la barabara au shule?
Kabla hujanunua kiwanja kagua vizuri ili usitapeliwe,usibomolewe baadae au kupata migogoro ya ardhi.
Karibu sana LAPEX kwa huduma ya uchunguzi kabla hujanunua kiwanja.
Soma Pia: Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa apiga marufuku uuzaji wa viwanja mitaani
Imeandikwa na;
Thom Meshack Munkondya.
(Mpima ardhi,Mtaalamu na mshauri wa masuala ya ardhi kutoka LAPEX).
0744336336.
Cc @lapexproperties