Kuna benki moja ya biashara yenye makao makuu yake Pugu Road yenye asili ya ki Nigeria iko kwenye hali mbaya sana kifedha na wateja walioshtuka wameanza kukimbiza amana zao kwa kuhofia usalama wa pesa zao.
Hii sio mara ya kwanza kwa benki ya ku Nigeria kufilisika na kuleta usumbufu mkubwa sana kwa wateja wao.
Meridean Biao ilianza kufa sasa inafuata hii benki ambayo inayatumia majengo ya Yusuf Manji yaliyopo sehemu mbalimbali za jiji kama matawi yake.
Mkuu hujaatendea haki kabisa haa jamaa, Hii ni bank iliyoanzishwa na waafrika kutoka Ghana, ina matawi zaidi ya Mataifa 30, inakuwaje wewe unaiita bank ya ki-nigeria, cha msingi unatakiwa utambue, biahsara ya kibank, kwa nchi za ulimengu wa tatu ni ngumu saana, kama hauko affliated labda na mafisadi, serekali, nchi na makampuni huwezi pata biashara hata kidogo. WeWe mbona hujiulizi kwanini EXIM bank inakuwa kwa kasi saana? Hakuna Mhindi mwenye madili makubwa anaweza peleka pesa yake Akiba bank atapeleka EXIM, Hakuna kampuni kutoka south africa inaweza peleka pesa yake CRDB badla yake watapeleka NBC, Hakuna mkenya au kampuni kutoka kenya wanaweza fungua account kwenye bank nyingine isipokuwa Kenya commercial bank
Tambua Taifa linapoenda kuwekeza mahali linafuatwa na vitu vingi, Angalia kampuni za kenya zilipokuja hapa Tanganyika mara moja zilifuata na Kenya commercial Bank, Insurance companies, KQ, security companies NK, hii ndio ilivyo. Hawa jamaa wa ECO BANK wanajitahidi tena saana, tatizo hawako affliated na mafisadi tu, Tambua account ya kampuni moja inaweza ikawa na mtaji wa hivi vibank vidogodogo, so wape muda naamini wataweza. hata wakifilisika wanamtaji
Kumbuka hata STANBIC-TZ kuna kipidni walifilisika ikabidi makaburu wawaongezee mtaji
Cha msingi waafrica tusaidiane wenyewe kwa wenyewe, hii ndio njia itakayo tukomboa na WIVU WA KIKE dhidi ya wenzetu wanaojitahidi