Kwanini biashara nyingi zinakufa baada ya baba au kichwa cha familia kufariki?

Kwanini biashara zinakufa moja ya sababu kukuu ni ukosefu wa elimu ya biashara,kama kampuni ipo chini ya sheria na ina strong managemnt basi haitaki nguvu kubwa kuendesha biashara hiyo maana amekufa mtu na sio kampuni.

Ila kuna sababu ndogo ndgo znapelekea kufa kwa biashara ni pale ndugu wanapoitaji mirathi wanakuwa tayari kuthaminsha mali za kampuni na hata pesa yakuendeshea biashara iyo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la biashara kufa sio tanzania tu ni dunia nzima. Kwa takwimu za USA ni kwamba 67% ya biashara za familia( family business) hufa katka second generation na 90% ya zilitoboa hufia third generation.

Shida kubwa ipo kwenye Succession plan.
 
Mimi nahisi sababu ya malezi yetu wa Africa, watoto wa kiume wanalelewa kuchukua majukumu ya kiume na wa kike hivyo hivyo, tukiwafundisha watoto wetu wakajifunza different roles,watakua na attitudes na confidence ya kuchukua role yeyote
 
Sio Asia tuu ni nchi za pamoja na nchi za ulaya kuna watu Wana biashara ina miaka zaidi ya 100 na bado ipo inadunda tuu. Yaani kama Africa tungekuepo hivo nasisi tungeshakuwa na makampuni makubwa mengi angalia company kama ya mengi inavyokaribia kipotea kizembe zembe
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto wengi hawaandaliwi kuongoza biashara za familia. Labda ni ukosefu wa kuaminiana kwenye familia.

Ni muhimu sana kuwaandaa watoto kwenye biashara za familia. Wazazi wanatakiwa wajue siku itafika umri utakataa kuendana na pirika za kuendesha biashara. Kwahio ni muhimu kuwapa muongozo mapema hili wakikosea warekebishwe kuliko kuwaachia peke yao hapo mbeleni bila maandalizi.
 
Hii nmeishuhudia kwenye biashara za familia kadhaa.
 
Ni kweli kabisa mkuu. Familia zetu nyingi kila mtu anajifikiria yeye binafsi na sio familia.
 
Kama una biashara washirikishe wanao kwa kuwafundishi thamani ya hela na maisha ya kiuhalisia
Wafunze kukaa na wewe pindi wanapotoka shule na kujua kuendesha biashara
Hii itawasaidia kujua na kuendeleza baishara baadae kwa ufanisi zaidi na kujua ndio maisha yao hayo



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Hivi kibongo bongo hili linawezekana kweli?
Kuwepo na kitu kinachoitwa family business maana ukianzisha biashara warithi ni watoto wako ila kazi za umma au binafsi ukifa anawekwa mwingine mambo yaendelee.
 
Marehemu huondoka na MALI ZAKE..
Mzee mwenyewe ndo anajua siri za utajiri wake ni ngumu kuuendeleza utajiri aliokuachia mtu.
Wachache wanaweza.

Sent using Jamii Forums mobile app
...Labda awe amekushirikisha katika kujua namna ya hata alivyoupata...Kuzika Kondoo...kulala juu ya Kaburi Usiku kucha...nk! ...ukimrithisha na haya, biashara inaweza ikadumu hata Wewe Mwenyewe Ukitangulia Kufa!![emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata uangalizi wa maboma magari msimamo wa familia n.k.
Ni shida..
 
Wazazi wa kiswahili waache kukumbatia biashara kana kwamba wataishi nayo milele, wawashirikishe watoto wao

Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo watoto wa kiswahili wakipewa kusimamia hachelewi kuiba na kuhonga, ndio maana mwisho unakuta baba anafanya yake na hawashirishi tena
Tofauti na waliohamia kwenye nchi husika
Hapo mtoto wa kiswahili akiona mzee anazungua ndio wanaanza kutafuta uchawi au kummaliza kabisa
Mwisho wanashindwa kuendeleza biashara maana hawajui A-Z ya biashara na wanaamua kugawana fito na baada ya mwaka au miwili unawakuta mitaani choka mbaya
Halafu tunaanza kusema laana hizo zimewapata
Kumbe walianza laana za kuiba angali bado wadogo


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Hapa ndipo tunapokosea sana kama wazazi. The least ni kuwaandaa kupata elimu ya biashara kuweza ku-add value katika biashara ya familia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…