kwanza biashara lazima ujitangaze, japo hata kwa jamaa zako wa karibu ili wakuunge mkono kwa kununua sio kukopeshana.
lakini pia nidhamu ya fedha, ule mtaji unapaswa kuuheshimu kuliko kitu chochote. kama haujafanya uzalishaji wowote na ukapa tatizo linahitaji fedha kugusa mtaji ni last resort. jifunze kupitia waliopo kwenye biashara jinsi ya kutunza vyema taarifa zako za kila siku vs bidhaa zako.
biashara inahitaji kujitoa kwa dhati kiakili, muda na nguvu zako zote mara baada ya kuanzisha. wengi wetu tunajitoa sana kwenye KAZI ZA KUAJIRIWA lakini tunafanya kinyume chake kwenye shughuli zetu. AIBU
kujifunza na kuijua vyema aina ya biashara na sekta unayochagua kuifanyia kazi, mfano chakula binadamu au wanyama, dawa kilimo na mifugo au binadamu, nguo, urembo, vifaa vya ujenzi, viatu, mitumba, e money, na nk.
kila biashara ina mahitaji tofauti ya mtaji lkn pia mzunguko wa pesa yako
pia hakikisha unasajili biashara yako mamlaka husika, kulipa kodi na vurugu nyingine ili uwe na amani na biashara yako.
mwisho trust the process