Kwanini biashara nyingi zinakufa licha ya kuwa na mitaji ya kutosha?

Kwanini biashara nyingi zinakufa licha ya kuwa na mitaji ya kutosha?

Joined
Sep 15, 2016
Posts
18
Reaction score
9
Kwanini Biashara inafeli sana licha ya mtu kuwa na mtaji wa kutosha na hata mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto zake?
 
Kwanini Biashara inafeli sana licha ya mtu kuwa na mtaji wa kutosha na hata mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto zake?

Ni topic ndefu sana...inategemeana na sekta,aina ya biashara...

Hapa utapata majibu very general maana swali lako ni very general..Hapo ndio shida.

Kwa kukusaidia,labda uwe unasoma au kuangalia youtube ya startups za USA uone success na failures zao.

Utajifunza mengi sana.

Japo TZ na USA wana tofauti kubwa sana,ila it is worth it learning maana principles ni zile zile..
 
kwanza biashara lazima ujitangaze, japo hata kwa jamaa zako wa karibu ili wakuunge mkono kwa kununua sio kukopeshana.

lakini pia nidhamu ya fedha, ule mtaji unapaswa kuuheshimu kuliko kitu chochote. kama haujafanya uzalishaji wowote na ukapa tatizo linahitaji fedha kugusa mtaji ni last resort. jifunze kupitia waliopo kwenye biashara jinsi ya kutunza vyema taarifa zako za kila siku vs bidhaa zako.

biashara inahitaji kujitoa kwa dhati kiakili, muda na nguvu zako zote mara baada ya kuanzisha. wengi wetu tunajitoa sana kwenye KAZI ZA KUAJIRIWA lakini tunafanya kinyume chake kwenye shughuli zetu. AIBU

kujifunza na kuijua vyema aina ya biashara na sekta unayochagua kuifanyia kazi, mfano chakula binadamu au wanyama, dawa kilimo na mifugo au binadamu, nguo, urembo, vifaa vya ujenzi, viatu, mitumba, e money, na nk.
kila biashara ina mahitaji tofauti ya mtaji lkn pia mzunguko wa pesa yako

pia hakikisha unasajili biashara yako mamlaka husika, kulipa kodi na vurugu nyingine ili uwe na amani na biashara yako.

mwisho trust the process
 
biashara nyingi za kiAfrika zina mambo mengi sana.....

Kwa ufupi sana, nadhani hata kushindwa kufanya biashara zetu kuwa independent kunachangia. Hatutenganishi fedha ya biashara husika (duka, usafirishaji,...) na fedha kutoka vyanzo vingine.

Kwa mf; naweza kuwa na duka. Nikilima shamba, nikauza mazao hiyo fedha naichanganya kwenye mtaji waduka. Nikitaka kulipa ada ya mtoto, nachukua humo humo. Mwisho wa siku tunashindwa ku control financial flow
 
Hapo ndo penye shida
 
Kwanini Biashara inafeli sana licha ya mtu kuwa na mtaji wa kutosha na hata mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto zake?

katika biashara yeyote zingatia haya, (na usijaribu kuchanganya mpagilio. Namba 1 usiipeleke kuwa 3 or 4).

1. Plan
2. Location
3. type of customer
4. capital (cash)
 
90% ya biashara za wabongo wanawaachia vijana mabinti ndugu wasimamie na wao eti ni waajiriwa mahali.Unategemea nini?huyo unayemuamini nae anashida zake kibaya zaidi hajui faida katika biashara yeye anatumia tuu na pengine anakimbia na pesa kabisa.Mswahili yupo radhi arande rande mtaani kijiweni eti yeye bosi jioni akapate mahesabu badala ya yeye kushinda katika biashara yake.Majibu ya wateja kwa mfanyakazi tofauti na wewe muwekezaji.Tujifunze kwa Wahindi hawabanduki katika kazi zao.Week end ndiyo wanaenda kujirusha
 
Ukosefu wa Umakini/uzoefu wa usimamizi wa biashara husika ndio tatizo kubwa.
Umenikumbusha duka la wife la vipodozi, lilikua kutoka mtaji wa 2M hadi around 17M, sasa wife akajifungua na mimi nikahamishwa kikazi, shemeji akawepo dukani muda mwingi, duka likafa kibudu, mkopo nikawa naulipa kwa hela ya mfukoni.
 
Back
Top Bottom