Kwanini biashara ya kuuza vitu vya ndani Dar inakua sana kipindi hiki?

Fundi_Mjasiriamali

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2018
Posts
748
Reaction score
1,340
Habari zenu wanajamvi wenzangu???

Mimi ni mtumiaji mzuri wa mitandao ya kijamii hasa facebook na jamiiforums.

Hivi karibuni nimejikuta kwenye mshangao mkubwa sana kila nikiperuzi kwenye mtandao wa facebook nakutana na post za watu kutoka DAR ES SALAAM waanauza vitu vya ndani vitanda, gas, tv na vitu vingine vya ndani, kwa kisingizio kwamba wana hama mkoa.

Nimekuwa niikijiuliza maswali mengi sana kwanini watu hawa wanauza na kuondoka huko na post zimekuwa nyingi sana za kuuza vitu vya ndani.

Naomba mliopo huko mnijibu maswali haya
. Je ni kwamba watu hawa wamepata kazi nje ya dar ndo maana wanauza vitu vyao?

Kama ni hivyo mbona hamna wanaouza kutoka mikoani??

Je maisha yamekuwa magumu ndo maana wanarudi makwao??

Au kuna sababu zingine??

Nawasilisha kwenu wadau
 
Hata ulaya na marekani jambo hilo ni la kawaida tu kubadili vitu vya ndani...huwezi kukaa na vitu vya ndani miaka 20 unatumia tu wenzetu kila mwaka wanabadili vitu nadhani sasa na huku kwetu tumeanza kubadili vitu vya ndani na kuendana na nyakati
 
Wafanyakazi wengi wa Serikali wamehamishiwa Dodoma, Makao Makuu ya nchi.
 
Mkulu anashaur asaiv ukienda dukan kununua nguo nunua undersize mana january itakutosha, m juz nilitoka kumodoa soksi
 
Mkulu anashaur asaiv ukienda dukan kununua nguo nunua undersize mana january itakutosha, m juz nilitoka kumodoa soksi
Hahahahaha[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kweli irons haijawahi muacha mtu salama
 
Matunda mazuri ya awamu ya tano, uza vya zamani nunua vipya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…