Kwanini biashara za mastaa wa bongo hazidumu?

Madimba jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2017
Posts
1,577
Reaction score
3,146
Hivi inakuaje mastaa wa bongo wanapojaribu kufungua biashara huwa hazidumu?
1. Wema alikuja na lipshine,zikabuma
2.Jaydee na ile kitu yake Nyumbani lounge,imeshapotea,
3.Chibu pafyumu &Diamond Karanga hazipo tena,
3.Jokate na bidhaa zake jiii,
4.Mofaya hii ndio ilishafeli kabla hata ya kuingia sokoni,
5.Body spray ya Mwana FA zilianza kwa mbwembwe sasa hivi zinakufa kibudu,
5.pafyumu ya Manara imbakia kwenye picha tu...
6.Vee Money na viatu vyake vya watoto havijulikani hata vilipo
7...........
8...........
9...........
10.........
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Nimecheka sana hapo kwa manara[emoji1787][emoji1787][emoji38]
 
Nadhani kikubwa ni poor management na wengi hawana maono ya mbali wanaanza biashara kwa kudhani umaarufu wao utawasaidia biashara kusimama siku zote pasipo kupambana na soko...

Wana amini wakisha tumia instagram na media ndio biashara inatembea na unaaanza kula faida..watembee field kujionea , sa unakuta msanii yeye huyo huyo anataka awe director ,market man anger,mtu wa finance
 
Diamond karanga zipo,
 
Wana amini wakisha tumia instagram na media ndio biashara inatembea na unaaanza kula faida..watembee field kujionea , sa unakuta msanii yeye huyo huyo anataka awe director ,market man anger,mtu wa finance
Hapo ndipo wanapofail,wanafikiri majina yao ndio yatabeba bidhaa zao sokoni,waajiri watu pro wauze bidhaa zao.
 
Zinakufa kwa sababu kiwanda hakionekani;tunaona bidhaa tu.
Mkuu umemaliza kila kitu, hawa wasanii hawaoneshi ile product line. Wao wanaishia kwenye uuzaji tu. Nadhani wanatumia majina yao tu, production line haiwahusu. Wao wako kwenye label na brandy name tu.

Sasa utajua vipi producer katoa bidhaa kadhaa? Mzigo unafyatuliwa China huko, msanii yuko bongo hapa hata container moja hajawahi kulipia ushuru bandarini yeye kazi yake kurusha picha tu IG. Ndio maana wana fail mapema.

Kuna wajanja wanapiga hela Sana kupitia hawa wasanii maana hawajielewi. Wanapenda umaarufu kuliko pesa. Mikataba yao sijui wanasainishwa vipi?
 
Joh Makini alisema anakuja na mradi wa Condoms.
Sijui iliishia wapi programme yake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…