Kwanini biashara za mastaa wa bongo hazidumu?

Kwanini biashara za mastaa wa bongo hazidumu?

Hii ndo point ya msingi. Moreover, bongo hatuna utamaduni wakununua bidhaa sababu tu ni ya msanii, tunanunua tokana na Bei na upatikanaji wake tofauti na mbele ambako mtu unaweza agiza online bidhaa ya his/her fav celeb

Aidha wengi wanaingia kwenye masoko bila ya kuyasoma, utamuuzia nani perfume laki1 bongo.
Lack of middle class inafanya biashara nyingi bongo zistruggle sio wasanii pekee yao
 
Tatizo si biashara zao, wengine walihongwa mdau alipopita akasepa na mtaji wake
 
Karanga zinasuasua,hiyo mofaya haijawahi kuonekana dukani hata supermarket kubwa kma shoppers,village etc hazipo.
Labda toka amezindua mpka leo mzigo uko njiani haujafika bongo,kwenye harusi yake sijui alipewa vikatoni kadhaa alete tz
DIAMOND KARANGA ZIPO MTAANI SIJAJUA HUKO KWENU HATA MOFAYA ZIPO BEI 3000
 
Karanga zinasuasua,hiyo mofaya haijawahi kuonekana dukani hata supermarket kubwa kma shoppers,village etc hazipo.
Labda toka amezindua mpka leo mzigo uko njiani haujafika bongo,kwenye harusi yake sijui alipewa vikatoni kadhaa alete tz
Mfanyabiashara yeyote anapotaka kuingiza bidhaa mpya sokoni ni lazima afanye utafiti wa kutosha. Jina haliuzi bidhaa, kinachouza bidhaa ni ubora wake na bei. Kuingiza sokoni bidhaa mpya kama perfume na ikakubalika siyo mchezo kwani kuna perfume zenye ubora kutoka kwa wazalishaji wazoefu. Ni nani atakayekimbilia kununua perfume ya ''mchina'' ambayo hatujui hata usalama wake kwa matumizi ya muda mrefu kina ina jina la Diamond?
 
Biashara inahitaji nidhamu ya hali ya juu upande wa pesa,so wengi wao hawana nidhamu hiyo kwani wanapenda maisha ya ghali kuliko wanachokiingiza kwenye biashara zao.
 
Biashara sio Sanaa, Ni utaalam.

Biashara haihitaji maigizo, Kiki na upuuzi mwingine waliozoea, unapaswa kua Real
 
Back
Top Bottom