Nilikuwa napenda kujua ni kwanini Bunge la Jamhuri ya nchi ya Kenya wanatumia Kiingereza kwenye dibeti zao?
Mkuu, umeuliza swali nzuri sana. Kwa muda mrefu nimetamaani kuleta mjadala kuhusu tofauti ya mchango wa Kenya na ule wa Tanzania katika ukuzaji wa Kiswahili, lakini mi hutatizwa sana wakati mjadala unageuka na kuwa ule wa "dudu langu ndefu kushinda lako."
Jambo la kwanza ambalo lafaa ujue ni kuwa kumekuwa na sera tofauti ya lugha, elimu, na siasa kwa hizi miaka ambazo zimepita. Tofauti na vile
lawmaina78 anavyosema, Kiswahili kilikuwa lugha rasmi (official language) hata kabla ya katiba mpya kupitishwa. Ktika miaka ya sitini na sabini, hata Kiswahili kuchukuliwa kama lugha ya taifa ilikuwa vigumu sana. Mtu ambaye alikuwa ni kana kwamba anawaabudu wazungu - Charles Nonjo, alipinga sana. Lakini Mwaka wa 1974, Kenyatta mara moja akaamua na kusema Kiswahili kiwe lugha rasmi ya Bunge. Hii ilikuja ikatolewa baadaye na mchezo mwingi ukafanywa. Hivi leo, Lugha Rasmi ya High Court, Court of Appeal na Supreme Court, ni Kiingereza tu.
Tatizo ni kuwa, elimu ya kale haikumlazimisha mtu kusoma Kiswahili baada ya darasa la nne. Kwa hivyo, watu wengi waliosoma enzi zile hawakukielewa kiswahili kamwe. Moi alipoingia madarakani na kuileta mfumo wa 8-4-4, alilazimisha Kiswahili kifundishwe katika shule za upili hadi Kidato cha 4. Lakini, Kizazi hiki kilikuwa kimezoe sheng. Tofauti na vile
flyingcrane anavyosema, hakuna yeyote atakayekudharau ukiongea Kiswahili sanifu bungeni; sijui hili amelitoa wapi. Tofauti na hilo, watu watakushangilia sana ikiwa utaongea kwa ufasaha.
Mdakuizi Umekosea unaposema kuwa katika bunge la taifa unakubaliwa kuchanganya ndimi. Kuna kanuni zinazofuatwa kuhusu lugha. Mara nyingi utampata Mbunge wa Tanzania anasema "Hili jambo la corruption ni lazima tulitatue once and for all." Jambo kama hili halikubaliki katika bunge la Kenya. Hili ndilo linafanya wabunge wanabaki kwa kiingereza.
Saa zingine, Kiswahili hutumika kuwakejeli wengine. Kama mnavyojua, mambo mengi ya Kiswahili yana maana mbili tofauti. Kwa mfano, Kuna mbunge mmoja aliyekuwa na tatizo na Raila Odinga ambaye alikuwa waziri mkuu. Kwa hivyo, akamwita Shoga - ambalo liko na maana tofauti. Hebu tazama video hii.