Kwanini CAG hatoi Ripoti ya Matumizi ya Tume za Uchunguzi?

Kwanini CAG hatoi Ripoti ya Matumizi ya Tume za Uchunguzi?

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,935
Imekuwa utamaduni wa kila siku,kusikia zikiundwa tume kuchunguza matukio kadhaa, yanayoleta kadhia mbalimbali ambazo huikumba jamii.

Tume hizo huteuliwa na viongozi wa ngazi mbalimbali tofauti, kuanzia ngazi ya taifa hadi mikoani.

Hii ikiwa ni kwa mamlaka wanayokuwa wamepewa kwa mujibu wa sheria, au toka kwa mamlaka za juu za uongozi kitaifa.

Pamoja na kuwa na nia au lengo zuri.
Lakini mara nyingi au karibu zote. Serikali hiyo hiyo, huwa haizifanyii kazi ripoti za uchunguzi toka kwa tume inazokuwa imeziunda na kutumia mamilioni ya pesa za walipa kodi wa nchi hii.

Tumeona kila siku tukitangaziwa kuundwa kwa tume za uchunguzi.
Tena kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Lakini pale zinapokamilisha kazi na majukumu yake iliyotumwa. Huwa hatutangaziwi kama ilivyokuwa wakati wa kuundwa kwa tume.

Jambo ambalo linapelekea kuonekana kuwa hizi tume, huwa ni kiini macho cha serikali kutumia ili kuficha udhaifu wake, katika kusimamia masuala mbalimbali muhimu kwa wananchi moja kwa moja.

Lakini pia tatizo kubwa kabisa,ni bajeti kubwa ambazo hutumika katika kuhakikisha tume husika imekamilisha majukumu yake.

Hii ikihusisha vitu kama.
*Posho kubwa kubwa kwa wajumbe husika.

* Usafiri wa uhakika kwa wajumbe kuwasafirisha ili kufika na kukutana ili kuanza kazi yao.Na pia wakati wa kurudi makwao ambako ni sehemu mbalimbali tofauti za nchi hii.

* Usafiri na malazi kwa wajumbe wa tume wakati wa utekelezaji wa majukumu yake.

* Usafiri na malazi kwa wale watakaohitajika kufika kutoa maelezo na pia kuhojiwa na tume.

* Gharama za uendeshaji vikao na watumishi wa tume kama makatibu pamoja na madereva wao kwa gharama za kujikimu.

Na mengineyo meengi ambayo ni ya kitaaluma zaidi.

Kutoutumia au kuitoa taarifa husika kwa wananchi kunapoteza umuhimu na manufaa ya tume husika kwa Umma.

Hivyo kupelekea kuwa matumizi mabaya ya mali za umma na walipakodi wa nchi hii.

Wakati hayo yakiendelea,kunakuwa pia na mgongano wa kisheria au kikatiba, kwani baadhi ya mambo ambayo hupelekea tume kuundwa huwa ni ya kijinai, na yalipaswa kushughulikiwa na vyombo husika, vilivyopo kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nikimaanisha taasisi kama TAKUKURU, POLISI, nk.

Inapoteuliwa tume kuchunguza jambo ambalo ni la kijinai. Technically ni kwamba taasisi husika zinakuwa zimepigwa pingu kutolishughulikia au kulichunguza jambo hilo.

Na pale inapotokea tume ikakabidhi ripoti yake, tena baada ya kuwa imetumia muda na gharama kubwa.ilimradi tu. Jambo hilo litoweke masikioni kwa Umma ulioumizwa na jambo hilo.

Pia aina ya wajumbe wateuliwa,mara nyingi unakuta ni wastaafu wa serikali na chama cha CCM, bao tayari wamepigika.

Na ni rahisi kwao,kuweza kushawishiwa na hatimae kupokea milingula toka kwa watenda kosa linalochunguzwa.

Pia kwa upamde wa pili,wanakuwa wanyonge kuogopa kutoa Maoni huru, pale ambapo imeonekana kidole kikiinyookea serikali kwa kusababisha tukio husika aidha kwa namna moja au nyingine.

Wanaohopa kwa kuhofia kumuudhi mteule wao, sababu kwao kuteuliwa kule walikuona kama ni fadhila.

Kwa kuwa tume hizi hutumia pesa nyingi sana za walipa kodi. Ni vema sasa CAG awe akitoa hadharani ripoti ya matumizi ya tume hizo ili wananchi wajuwe kama zina tija yoyote,kwa maendeleoa chanya kitaifa.

Alamsikhi!
 
Back
Top Bottom