Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

Yes aliyefanya kosa ni HAM ila laana ikaenda kwa CANAAN ndio nmetoa sababu kadhaa kwanni ikawa hivo soma nadharia #1 utapata mwanga
Hii pia inatoa mwanga wa pale Mungu anapokasirika na kutoa laana kwa kosa lililotendwa na kizazi cha kwanza.. Laana hiyo huenda mpaka kizazi cha tatu na cha nne! Let's try to connect the dots
 
Mkuu mitale na midimu.....hoja yako ya kuwa Nuhu hakumlaani Ham sababu ya Baraka aliyopewa na Mungu ina mashiko pia nafkiri inaweza saidia kutatua kizungumkuti hiki ILA nikiuliza mbona kuna instance nyingi ambazo Mungu anabariki na baadae analaani mfano wana wa israel walibarikiwa sana kwa maneno ya Mungu mwenyewe na baadae wakaja kulaaniwa na Mungu huyo huyo.... Hata Mungu alibariki uzao wa Abraham ila tunaona Yakobo alimlaani mtoto wake aliyelala na hawara yake na laana ilisimama !! Je kama huku kwa Yakobo mambo yalikuwa hivo je kwanini hayakuwa hivo kwa Nuhu pia as far as Genesis 9:1 is concerned
 
mkuu nakupata, ngoja tuendelee kufikili kibibiliabibilia zaidi wakati tunasubiri wasomi wa kiyahudi,kimushaf,kijubilee na kikaldayo.

Kuhusu Operation za laana za Mungu ninamaoni kadhaa.

yakijengwa katika mstari huu pia..
Kumb 30:19 ''Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;''

ni suala la UCHAGUZI, Kama Mungu anatuambia tuchague nadhani anajua huwezo huo wa kuchagua laana au baraka tunao.

Baadhi ya commentary zinasema, ahadi za Mungu ni conditional na reversible.
Ikiwa...... Nita....
pia kumbukumnu la torati 28 kuna laana na baraka pale ambazo chochote utakachochagua matokeo yake hayaepukiki.

Kwa Mungu unaweza kuchagua laana leo, kesho ukaghaili ukachagua Uzima na baraka na bado akakupokea.
Hasa sisi tunaoamini Mauti ya Yesu ambayo kwayo kwa neema tutairithi nchi suala la baraka na laana liko wazi.

Chagua Yesu -ubate baraka na ondoleo la laana ya uchaguzi uliofanya na adam na hawa na zaidi ya yote uzima wa milele na kuketi pamoja nae katika kiti cha enzi mahala ambapo shetani alitamani kukaa kwa hilana kiburi yakamkuta ya kumkuta.

Chagua Kuufuata Mwili (kubaki katika laana ya asili ya adamu ),Dunia na Shetani utakula matunda yake pia.


Hivyo nadhani Mungu sio kigeugeu bali hughaili bale tunapobadilika. Mfano mzuri Daudi mtoto wa Yese.

maoni mkuu. nadhani kuna chembechembe ndani yake zinaweza kuwa na mashiko.
 
Hapa na Mimi nilitaka kuuliza hiv hivi
Mkuu nakuelewa sana.......INA...kama kumchungulia baba Ni kulala na mkewe.....jee.....kumfunika inaweza kuwa na tafsiri gani?
Tusubiri majibu
Mkuu ambacho nataka kieleweke ni kwamba Nuhu kweli alilewa pamoja na mkewe alafu Ham kuona mama yake yupo kihasara akamuingilia hivyo hapo ndipo ALIFUNUA UCHI WA BABA YAKE hivyo wakifunika UCHI itakuwa kinyume chake labda walienda kumzuia HAM kuendelea kufanya kitendo hicho kwa Mama yao so kwakuzuia WAMEFUNIKA UCHI WA BABA YAO ndio maana wakabarikiwa

Najaribu kufikiri tu ngoja wataalam watakuja nisahihisha
 









Mwanzo 9

22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.

Inapingana na hiyo Dhana ya kumzuia asimzini
 
aiseee"" hawakumpiga hata makofi huyo ham ""?...jinga kabisa
 
NAOMBA NIWEKE BOLD.
Mkuu ndani ya Qur-an ipo hoja kama hio au mfano wa hio,,ingawa simulizi yako bado haijatiririka kama ilivyo ndani ya Qur-an.
Kwa kifupi yupo mtoto wa Nuhu aliekufa kwenye gharika,,wakati anahangaika(anatapatapa) ndipo Nuhu akamwambia mola wake Ee mola wangu uliniahidi kwamba wanangu hawataangamia.Mwenyezimungu akamwambi "Huyo si katika Ahali yako(watu wa nyumbani kwako),na usiuombe jambo ambalo hauna elimu nalo"...soma maneno hayo between line ili ujazie utafiti wako.
 
Nashukuru mkuu kwa Ilimu yako bila shaka yatoka kwenye Quran takatifu surat Hud..... Huyo mtoto kwenye sura hii anaitwa Kanaan pia naanza kupata picha kubwa zaidi....

Barikiwa mkuu
 
aiseee"" hawakumpiga hata makofi huyo ham ""?...jinga kabisa
Hahahahahaha asee ingekuwa uswahilini kwetu huku ujiji ama kigogo sambusa lazima wangemgawana vipande
 
Chief ktk hoya No.2 hapo wakati Nuhu anamlaani Kanaani, kanaani alikua ameshazaliwa au alimlaani kupitia mgongo wa Ham?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…