Mkuu
mitale na midimu.....hoja yako ya kuwa Nuhu hakumlaani Ham sababu ya Baraka aliyopewa na Mungu ina mashiko pia nafkiri inaweza saidia kutatua kizungumkuti hiki ILA nikiuliza mbona kuna instance nyingi ambazo Mungu anabariki na baadae analaani mfano wana wa israel walibarikiwa sana kwa maneno ya Mungu mwenyewe na baadae wakaja kulaaniwa na Mungu huyo huyo.... Hata Mungu alibariki uzao wa Abraham ila tunaona Yakobo alimlaani mtoto wake aliyelala na hawara yake na laana ilisimama !! Je kama huku kwa Yakobo mambo yalikuwa hivo je kwanini hayakuwa hivo kwa Nuhu pia as far as Genesis 9:1 is concerned
mkuu nakupata, ngoja tuendelee kufikili kibibiliabibilia zaidi wakati tunasubiri wasomi wa kiyahudi,kimushaf,kijubilee na kikaldayo.
Kuhusu Operation za laana za Mungu ninamaoni kadhaa.
yakijengwa katika mstari huu pia..
Kumb 30:19 ''Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa
nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;''
ni suala la UCHAGUZI, Kama Mungu anatuambia tuchague nadhani anajua huwezo huo wa kuchagua laana au baraka tunao.
Baadhi ya commentary zinasema, ahadi za Mungu ni conditional na reversible.
Ikiwa...... Nita....
pia kumbukumnu la torati 28 kuna laana na baraka pale ambazo chochote utakachochagua matokeo yake hayaepukiki.
Kwa Mungu unaweza kuchagua laana leo, kesho ukaghaili ukachagua Uzima na baraka na bado akakupokea.
Hasa sisi tunaoamini Mauti ya Yesu ambayo kwayo kwa neema tutairithi nchi suala la baraka na laana liko wazi.
Chagua Yesu -ubate baraka na ondoleo la laana ya uchaguzi uliofanya na adam na hawa na zaidi ya yote uzima wa milele na kuketi pamoja nae katika kiti cha enzi mahala ambapo shetani alitamani kukaa kwa hilana kiburi yakamkuta ya kumkuta.
Chagua Kuufuata Mwili (kubaki katika laana ya asili ya adamu ),Dunia na Shetani utakula matunda yake pia.
Hivyo nadhani Mungu sio kigeugeu bali hughaili bale tunapobadilika. Mfano mzuri Daudi mtoto wa Yese.
maoni mkuu. nadhani kuna chembechembe ndani yake zinaweza kuwa na mashiko.