Mkuu hiyo laana imetoka kwa baba yao mwenyewe aliyeitwa Yakobo(Israeli). Fahamu kwamba Yakobo ambaye alibadilishwa jina na MUNGU na kuitwa Israeli, alikuwa pia anatambulika kama Nabii. Sasa kama nilivyosema Nabii wa MUNGU akitoa laana, laana hiyo inakuwa imetoka kwa MUNGU mwenyewe, Vivyo hivyo na baraka pia.
Ukitaka kujua hiyo laana ilikuwa inatolewa kwa niaba ya MUNGU mwenyewe kupitia kinywa cha Yakobo, soma tena huo mstari wa saba hapo nilipoweka alama nyekundu; "7..........nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli". Hapa utona Yakobo ambaye ndiye Israeli anaongea kwa niaba ya..., kwa niaba ya MUNGU, ni MUNGU peke yake mwenye uwezo wa "kuwagawa na kuwatawanya". Hivyo laana hii ilitoka kwa MUNGU mwenyewe kupitia kinywa cha Yakobo ambaye alikuwa ni Nabii wa MUNGU.
Na ukitaka kujua kuwa huu ulikuwa ni Unabii ni pale ambapo utaona Unabii huu ulikuja kutimia, maana ni kweli kabisa kabila la Simeoni na Lawi yalitawanywa katika Israeli. (Soma YOSHUA 21:1)
Kama nilivyosema mwanzoni, ni BWANA MUNGU peke yake mwenye uwezo wa kuwalaani wana wa Israeli na laana hiyo ikatimia. BWANA MUNGU anaweza kuwalaani kwa kutumia kinywa cha Nabii, kama vile alivyotumia kinywa cha Nabii Yakob, Musa, Eliya, Isaya, Yeremia n.k.