Kwanini ccm hawawatimui mafisadi??

Kwanini ccm hawawatimui mafisadi??

MtazamoWangu

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2009
Posts
313
Reaction score
7
hili swali limekuwa linanitatiza sana...na pengine ndio maana wengine wanakiita CCM ni chama cha mafissadi...
kwanini kama wanachama wake wametajwa kwenye kashfa mbalimbali za ufisadi wasiwasimamishe uwanachama au hata kuwatoa katika nafasi za uongozi tu....kama mpaka kesi imefika mahakamio inamaana DPP amejiridhiza kuwa ipo kesi, na kama imefikia mtu akajiuzulu mwenyewe kwa kashfa zinazimkabili ina maana amekubali kuwajibika kwa kiasi fulani..sasa kwanini CCM haiwawajibishi hawa watu...
1. Chenge...pamoja na kutajwa kuhusika na rushwa ya radr bado ni kiongozi ndani ya CCM na ubunge..
2. Rostam Aziz...anatajwa sana na kashfa za richmond/dowans, kagoda..bado ni mjumbe muhimu wa chama na mbunge...
3. Edward lowasa....pamoja na kujiuzulu kwa kuhusishwa na richmond bado ni mbunge na mjumbe muhimu wa chama, tena ana mamlaka makubwa kwenye chama maana kuna hata dalili za kumzidi mwenyekiti wake maamuzi...
4. basili mramba...pamoja na kuburutwa madarakani,bado ni mbunge wa chama na mjumbe pia...

you can add to the list....

hili suala ndio litakalo mharibia JK mwakani kama asipofanya uamuzi..tena hawa watu wanajeuri ya kupanga kumvua uwanachama mtu kama SPIKA SITA...tena na mwenyekiti akaruhusu hili...kwanini NEC haijawahi kujadiri majina ya masifadi na kutoa tamko????

kuna mahusiano makubwa kati ya ufisadi na CCM....sio siri sasa hivi hata watoto wanajua na ndio kamba tutayowanyonga nayo hii...

...hata mjomba alisema...ukiona vipi timua wote, kwani kuanza upya sio issue...
 
The fact is all ccm leaders are corrupt through and through. No one raised to power including the president without corrupt means. Thats why at one tine they legalize "Takrima", showing corruption is part and parcel of their policy
 
Sio tu kumnyanganya Spika Kadi yake ya CCM, bali wanauwezo wa kumwondoa madarakani hata JK mwenyewe.
 
mkuu hao ndio wafadhili wa CCM sasa kama watawafukuza hao watu chama kinaweza kikayumba kwa kukosa ufadhili
 
The fact is all ccm leaders are corrupt through and through. No one raised to power including the president without corrupt means. Thats why at one tine they legalize "Takrima", showing corruption is part and parcel of their policy


That is the truth. All CCM leaders from top to bottom are corrupt.
 
Tangu iundwe CCM-chama cha mafisadi,kimejaribu kuua upinzani,ili kuendelea madarakani na kudanganya watu.
Ni pesa ngapi toka NPF and NSSF zimechotwa kwa ajili ya kuiendesha CCM!

Nchi yetu imeoza,hata mtu wa kumkimbilia kulinda maslahi !Rais hawezi kufanya lolote,atamaliza muda wake na kuwa na trip kila siku za kuja Ulaya.

Namkumbuka Mkapa ,alikuja hapa UK ,ilikuwa wakati wa Tony Blair,kuhusu masuala ya Third Wolrd.Walimhoji kwenye TV,akasema sio wote marais wa afrika wanaiba hela na kuweka ulaya.Niliposikia scandal zako ,nilishangaa sana.Tukumbuke Nyerere ndio alimchagua Mkapa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1

Hapa Uk,kuna baadhi ya mafisadi mamefanikisha kufungua matawi ya CCM!You cant believe mtu yuko Ulaya bado anaishabikia CCM!Nafikiri ni njia ya hawa jamaa kujipenyeza CCM ili wakirudi nyumbani wapate direct contacts.

Tunakwenda wapi jamani?Baraza la mawaziri na Wabunge wengi wana fake Phd ,nafikiri ni nchi pekee duniani ina cabinet na wabunge wenye fake Phds!Hata kwenye Jumuia ya East Afrika,tuna wabunge 2 wote wanf fake Phd!Aibu jamani!
 
ccm ndio mafisadi wenyewe wakiwatimua mafisadi ina maana wanajitimua wenyewe,

hawana ubavu wa kuwatimua waliotajwa hapo juu, kwa sababu wameshirikiana nao kufanikisha ufisadi wao, mwizi hawezi kuwajibishwa na aliyemsaidia kuiba, akimuwajibisha ataumbuliwa

asiye na ufisadi awe wa kwanza kuwatupia jiwe.....
 
Tangu iundwe CCM-chama cha mafisadi,kimejaribu kuua upinzani,ili kuendelea madarakani na kudanganya watu.
Ni pesa ngapi toka NPF and NSSF zimechotwa kwa ajili ya kuiendesha CCM!

...hivi haya mashirika hayafanyiwi any auditing kujua uendeshaji wake wa kazi? mimi nafikiri wananchi/wanachama wake wafanye uchunguzi wao wenyewe na kama ni kweli kuna ubadhilifu wa namna hiyo waje na lawsuit ya management yao na kudai pesa zao toka CCM zirudi,nina imani na judicial yetu kidogo inaweza kufuata haki hapo...its time haya mashirika yanayochukua pesa za wananchi yawe responsible kwa wananchi na sio chama cha siasa,hii inawezekana kabisa kuifilisi CCM kama kweli wamechukua hayo mabilioni!
 
Kutimua mafisadi CCM, ni kukata shina ulilokalia.

Kama utatimua mafisadi, chama kitabaki na nani?
 
Kama asilimia kubwa ni mafisadi au wamekua wakifadhiliwa na mafisadi kama wakiwatimua mafisadi nini kitabaki?Wote mafisadi!
 
Back
Top Bottom