Mlalamikaji daily
JF-Expert Member
- May 19, 2014
- 1,018
- 2,366
Wakuu hizi ni sababu kadhaa za kuaminika na zimefanyiwa kazi kwanini CCM watashinda kila wakati
1. Aina ya wapiga kura.
Hii ni sababu mojawapo, vijana wengi na wasomi ambao pengine ndio wangeweza kuitoa CCM madarakani sio Wapiga kura!! Kwahiyo CCM ina mtaji wa watu wengi hususani wazee na wakina mama kwa upekee wao ambao wako huko Vijijini na ndio huko CCM imeweka mizizi.
Ndio maana sio bahati mbaya wakati wa kujiandikisha utaona vijijini kuna vituo kila Sehemu lakini Huku mjini kujiandikisha ni VITA..
Sisiemu sio wajinga.
2. Suala la CCM,Tume ya uchaguzi, serikali na Dola kufanya kazi kama mapacha sina haja ya kulielezea..
Na hii ni kwamba hata kama hiyo namba moja hapo juu ikifeli bado hii namba mbili itakuwa aplikabo
3. Aina ya wananchi wenyewe wa Tanzania.
Kama alivyowahi kunukuliwa kiongozi mmoja alisema Wakenya wamelala usingizi muda wowote wanaamka, Waganda ni wagongwa ambao kama wakitumia dawa na kufuata ushauri wa daktari wanaweza kupona LAKINI watanzania ni maiti kamwe hawawezi kuamka. Kifupi sisi hata tukionewa bado tutamuachia Mungu tu..
4. Rushwa, Sisiemu inatumia pesa nyingi angalia idadi ya "walionunuliwa" toka enzi zile kwa kupewa uongozi au kupewa fedha watoke kwenye upinzani!
5. Kuwepo na matawi ya CCM
Tuliona wazi wazi mfano TLP, ilikua inaunga mkono wazi wazi CCM na sasa tunaona ACT na leo Hii wazee wa Ubwabwa (chauma) unaweza kujua tu ni nani anagharimia kinachoendelea
Habari ndio hiyo