Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Binadamu yeyote ana hatua anazopitia, na watu hutofautiana namna wanavyozipitia hatua hizo na wakati wa kuzifikia.
Kuna watu huzeeka mapema na wengine huchelewa.
Lakini la muhimu zaidi ni kuwa kuna watu wanazeeka miili na mwonekano wa nje lakini akili zao hubakia kuwa Super. Mfano mzuri wa watu wa namna hiyo, kwa hapa nchini petu ni Mzee Jaji JOSEPH SINDE WARIOBA. Huyu mzee, akili yake haijawahi kuteteleka, na anawazidi akili na uwezo wa kutafakari na kuchbua mambo, watu wengi sana, wazee na vijana.
Lakini kuna watu, kwa bahati mbaya kabisa, wanapozeeka miili, wanazeeka na akili zao. Na mfano mzuri sana wa watu wa namna hiyo hapa nchini petu ni Mzee WASIRA. Ishara mojawapo ya haraka ya kujua kuwa mtu anazeeka haraka akili, ni huyo mzee kusinzia wakati wote. Na hiyo hutokea kwa sababu kila tendo katika mwili huongozwa na ubongo. Hivyo ubongo unapochoka, mwili unakosa uongozi. Nyote ni mashahidi, WASIRA kwa sasa, ni ngumu sana kumaliza hata masaa mawili akiwa amekaa bila kusinzia.
Watu waliomsikiliza WASIRA siku za karibuni watakuwa wamemsikia jinsi alivyo mropokaji. Kuna wakati anatoa majibu ya hoja ambayo haipo, hiyo ina maana hana hata ule uwezo wa akili kuweza kujua hoja inayojadiliwa.
CCM inajua kuwa mzee WASIRA, hayupo katika utimamu wa akili. Kwa kuwa wanaujua ukweli huo, kwa nini wameamua kumpa umakamu wa mwenyekiti wa chama? Kwa kumpa hiyo nafasi, na kumwacha awe anaropoka kila wakati, kutawafanya wananchi wote wajue kuwa mzee WASIRA sasa hayupo kwenye utimamu wa akili. Je, kufanya hivyo kunalenga nini, zaidi ya kumdhalilisha mzee WASIRA?
CCM ilistahili kumsitiri WASIRA kuliko kumdhalilisha. Wapo watu, ambao kwa bahati mbaya wana wazazi wao waliozeeka kupindukia, wengine kiasi hata cha kujisaidia bila kujitambua, lakini ili kuwasitiri, wakati mwingine hulazimika kuwahifadhi ndani hasa kunapokuwa na wageni. Sasa, mbona CCM imekosa hata hekima hiyo ndogo?