Kwanini CCM inachukiwa wakati imeleta maendeleo?

Tatizo ni uongozi wa chuki na ubinafsi eti maendeleo hayana vyama
 
Kumchagua kiongozi au kukipenda chama kisa ujenzi wa miundombinu au manunuzi ya vitu muhimu na vya msingi... Ni dalili za upungufu wa akili...
 
Watanzania asilimia 80 wako vijijini, na hata hawajui fulayi ova, stigilazi goji ni nini, wengi maisha ni magumu sana hata msosi tabu, wewe unamwambia habari za bombardia au Dirimulaina, atakuelewa? Haya ongeza na hii habari ya kuuwa watu hovyo eti kisa tuu tofauti za kisiasa kweli?
 
πŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸ½
 
Maendeleo ya Tozo?
 
CCM kingekuwa kinaleta "maendeleo" kingekuwa kimeshatoka madarakani zamani sana.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Unaishi Tanzania, gani ? Kama wewe unaichukia CCM kwa hiyo ndio Tanzania yote? CCM ipo leo na itaendelea kuwapo kesho na milele.

Chama bora kabisa Africa, na inafahamika duniani kote.
 
πŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸ½
 

Maendeleo yapi? Labda porojo za maendeleo.

Hayupo mtu (wakiwamo wao CCM) anayeweza kufurahishwa na ukosefu wa:

1. Haki
2. Usawa
3. Uhuru
4. Utawala wa kidemokrasia

Haya yakimsibu yeyote hata aliye mnufaika wa kutokuwepo haya kwa wengine leo, hakutakalika.
 
Je, kwanini wananchi wameacha kuthamini miradi inayoendelea na kuwachukia wanaowaletea hayo
Ni kwa kuwa wanatawala bila ridhaa ya umma wa watanzania.

Sandaku la kura haliheshimiwi kabisa.

Wapo madarakani kimabavu kwa ridhaa ya NEC na vyombo vya dola.

Tofauti yao na WAKOLONi wa mwanzo ni rangi ya watawala tu.. maana hata wale wa mwanzo kuna miradi walijenga, mfano reli ya kati.
 
Hata Hitler alichukiwa japo alileta maendeleo makubwa kwa Germany!

Kwa hiyo jipange tena kabla hujauliza hili swali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…