CCM ni tofauti sana na vyama vingine vya siasa nchini ambavyo vina usajili kamili chini ya sheria ya Vyama. Sifa pekee za CCM zinajidhihirisha wazi wazi katika masuala mazito ya kitaifa yafuatayo:-
(1) Azma ya kuhakikisha kwamba Muungano wa Tanzania na Mapinduzi ya Zanzibar vinaheshimiwa, vinalindwa na vinaendelezwa wakati wote.,
(2) Azma ya kuhakikisha kwamba ardhi inaendelea kuwa rasilimali kuu ya Taifa na inayoendelezwa kwa maslahi ya wananchi wote.
(3) Azma ya kutaka kuona kwamba Tanzania ni Taifa lenye Umoja, Amani, Utulivu na Mshikamano madhubuti wa kitaifa wakati wote;
(4) Azma ya kuhakikisha kwamba Utawala wa Sheria na Utawala Bora vinalindwa na kuendelezwa wakati wote;
(5) Azma ya kuhakikisha kwamba Watanzania tunajenga maadili na demokrasia ya vyama vingi katika mazingira ya amani, yanayokataa siasa za uchochezi, uzushi, kashfa, uzandiki, uongo, ubaguzi wa rangi, ukabila, umajimbo na udini, mambo ambayo ni kinyume cha Haki za Binadamu.
Wananchi kuichagua CCM maana yake ni kujihakikishia wao wenyewe kwamba wataendelea kula hayo matunda ya uhuru kwa ukamilifu.
(toka Kanuni za Uteuzi wa CCM)
Duu?? Labda nina tatizo la kunagalia kinume nyume, mbona mambo yote matano ulo yataja nayaona kinyume nyume jinsi yanavo tekelezwa?
mfano:
1)
'Mapinduzi ya Zanzibar vinaheshimiwa, vinalindwa na vinaendelezwa wakati wote' Hivi kuendelezwa kwake ndo mabavu mabavu hadi mauaji ya raia wasio kuwa na hatia? rejea mauji ya Pemba
2)
'ardhi inaendelea kuwa rasilimali kuu ya Taifa na inayoendelezwa kwa maslahi ya wananchi wote' Hii sijui hata nisemeje? Anzia wae wananchi wa Ihefu, wale wa Bulyankulu, achilia mbali wale wa GGM, tusisahu wale wananchi wanao fukuzwa kule karibia na kiwanda cha wazohill pia kama mnakumbuka tulisha ona picha humu JF za askari akimtandika mboko mama mmoja mkazi wa huko wazo walipokuwa wakijaribu kuandama kupinga kunyanganywa ardhi yao apewe muwekezaji, na sijui wale wahadzabe waliishia wapi? kwa hili nawapongeza kwa kuhakikisha wanahakikisha ardhi inakuwa mali ya muwekezaji !
3)
'kwamba Tanzania ni Taifa lenye Umoja, Amani, Utulivu na Mshikamano madhubuti wa kitaifa wakati wote' Kwa kisingizio hiki hiki wezi na wahujumu uchumi wanapeta mitaani, eti wakiguswa nchi itayumba na amnai itatoweka? kwa kisingizio hiki hiki sheria zimekuwa zikipindishwa na kuweka double standards! Sijui ni amani kweli ama ni woga! Kisingizio cha amani na utulivu tumeshuhudia vijana wetu vyuoni wakipigwa marungu na FFU bila sababu za msingi,vyuo vikigeuzwa makambi ya jeshi! tumeona watu kama Zito kabwe wakinyima haki yao ya msingi kutoa mada mbali mbali kwa intelectuals.. FFU wanamwagwa mitaani hovyo wanapiga watu eti wanalinda amani na utulivu! Siamini hiyo kama ni amani bali ni kujenga taifa la waoga!
4)
'Utawala wa Sheria na Utawala Bora vinalindwa na kuendelezwa wakati wote' Rejea hapo juu, kwa mafisadi sheria zinapindishwa, mashitaka yanapelekwa mepesi, mfano Yona pamoja na wizi wa kiwira, anashitakiwa kwa kakosa kadogo tu.. mengine yote yanafunikwa, mramba pamoja na ten percent zote na kutaka tule nyasi mashitaka malaiiiini, chenge, na Rashid, tunaona wanavo peta mtaani hata hawaguswi! Mpaka system ikuteme ndo sheria inaonekana, lakini kama wewe ni ndani ya system wala sheria haikugusi!
5)
'Azma ya...vyama vingi katika mazingira ya amani, yanayokataa siasa za uchochezi, ubaguzi wa rangi, ukabila, umajimbo na udini,......' Sijui hili CCM wamelitekeleza wapi? rejea walivo kibatiza CUF chama cha kidini, walivo eneza CHADEMA chama cha kichaga, rejea kauli za Sumaye ukitaka mambo yako yawe safi rudi CCM, rejea kudorola kwa maendeleo kwa kisiwa cha pemba, rejea kauli za Makamba TARIME, chagueni CCM ndipo mtaletewa maendeleo kwani ndiyo yenye pesa!, Oh, God bila kusahu wale wahanga wa kiteto.. picha zao tuliona humu ama kweli mazingira ya amani ya vyma vingi ccm imeyajenga!
Nashangaa kwakweli kama sera zao ni nzuri namna hiyo ila wamejikita kuzitekeleza kinyume nyume, pengine ni mtazamo wangu lakini ndivyo niaonavyo, na laiti wangetekeleza haki bin haki ningekuwa wa kwanza kuipigia debe!