Kwanini CCM Zanzibar haipambanii Dkt. Ali Mohamed Shein kuongezewa muda kama huku bara?

Kifurukutu

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2013
Posts
4,641
Reaction score
6,694
Ukianzia na Bunge, UVCCM na baadhi ya makundi ya watu wachache hasa wanaccm wako mstari wa mbele kabisa kupaza sauti na kupambana Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibadilishwe ili tu kuweza kumpa Magufuli nafasi ya kuongoza kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano.

Wengi wa wanaodai aongezewe muda wana sababu zao kwamba amefanya vizuri hivyo aendelee tu

Je, huko visiwani Zanzibar, Ali Mohamed Shein amefanya vibaya?

Kwanini huko nako asipigiwe kelele za kuongezewa muda ili uchaguzi wa mwaka huu apewe nafasi tena kama ambavyo huku bara imeaminishwa mkulu atalazimishwa baada ya 2025?
 
Headmaster yupo bara Zanzibar kuna kaka mkuu wa shule kwahiyo anasubiri tu walimu na mkuu wa shule wanasemaje.
 
Kachemsha pamoja na kushinda kwa mbeleko ya Jecha,miaka 5 bado wazanzibar wanaishi chini ya umasikini ulio topea.
 
Kachemsha pamoja na kushinda kwa mbeleko ya Jecha,miaka 5 bado wazanzibar wanaishi chini ya umaskini ulio topea.
Angalia huku bara...hakuna mtu anae ishi chini ya dola kumi kwa siku.
 
Kuhusu Doctor Shein ,kimya yeye ndio anamaliza kipindi chake cha pili cha urais Zanzibar,mbona wanaotaka Magufuri aongezewe muda hawasemi Doctor Shein aongezewe muda au yeye hakufanya vizuri au yeye hafanani na Yesu Kristu?
Labda hafanani na mtume Mohd.
 
Ukianzia na Bunge, UVCCM na baadhi ya makundi ya watu wachache hasa wanaccm wako mstari wa mbele kabisa kupaza sauti na kupambana Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibadilishwe ili tu kuweza kumpa Magufuli nafasi ya kuongoza kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano.

Wengi wa wanaodai aongezewe muda wana sababu zao kwamba amefanya vizuri hivyo aendelee tu

Je, huko visiwani Zanzibar, Ali Mohamed Shein amefanya vibaya?

Kwanini huko nako asipigiwe kelele za kuongezewa muda ili uchaguzi wa mwaka huu apewe nafasi tena kama ambavyo huku bara imeaminishwa mkulu atalazimishwa baada ya 2025?
PIGA KELELE
 
Back
Top Bottom