Makamanda huwa hamtaki kusikia kabisa kuhusu Kamanda wenu Mkuu kuwaachia kiti wengine! Huwa mnaamini yeye ndiye Chadema, na Chadema ni yeye. Ila amini nakuambia, muda wa Kamanda wa kukijenga na kukiimarisha chama ulishapita mara tu baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015!
Kuanzia pale uchaguzi mkuu tu ulipokwisha, alitakiwa akae pembeni na kuwaachia Makamanda wengine waendeleze pale alipoishia. Tunakoelekea, chama kitamfia mikononi mwake. Na uchaguzi wa mwaka huu 2020 ni ushahidi tosha! Mtafanyiwa kila aina ya figisu ili Wabunge wenu wote Makini wasirejee Bungeni.