Bill
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 9,258
- 10,014
Mauaji yametokea Njombe kijana Mlelwa kauawa Chadema hawajalaani au kutolea kauli kuwataka wanachama wao kuheshimu sheria za nchi na kanuni za uchaguzi ili kudumisha amani.
Mauaji pia yametokea Tunduma kijana akipigwa tofali hakuna tamko la Chadema.
Watu wamekatwa mapanga msikitini Zanzibar Chadema kama chama kikuu cha upinzani chenye ndoto kuongoza nchi bado kimeendelea kukaa kimya.
Tukirudi nyuma mauaji ya kibiti, Chadema hawakuwahi kutoa kauli yoyote kulaani wananchi kuuana au kuuliwa kwa viashiria vya mauaji ya kigaidi. Pengine walikebehi jitihada za serikali kupambana na mauaji hayo lakini pia walijitokeza haraka kuuliza walipo vijana washukiwa wa mauaji hayo.
Msimamo wa chadema katika masuala ya amani ya nchi hii ukoje? Kwa ujumla ukifuatilia hata kauli za kiongozi wao anaejaribu kuingia Ikulu unaashiria mitafaruku na uvunjifu wa amani. Itoshe tu kusema, Chadema wamekuwa wakiandaa matukio na kutoa kauli ambazo zitasababisha chuki kwa serikali na vyombo vyake mfano tukio la kuchoma ofisi yao Arusha, mabomu ya Tarime na uzushi wa mambo mengi ya uongo kama vile Uwanja wa Chato, ndege kutokukaguliwa na CAG na ununuzi wa ndege kutoidhinishwa na bunge na kubwa zaidi Rais Magufuli kuwaita Dodoma wakurugenzi wa Halmashauri kuwapa maelekezo ya kufanya wakati wa kupiga kura.
Haya yote ni viashiria ovu kwa mustakabali wa amani ya nchi kutoka chama kinachotaka kuingia Ikulu.
Je, kinataka kuharibu amani ya nchi kisha kikiingia madarakani kiirejeshe? Je, kinataka kujenga chuki na kuwagawa waTanzania wakati huu wa kampeni kisha kikiingia madarakani kianze kazi ya kuwaunganisha?
Kwa ujumla mwelekeo wa chadema kisipobadili msimamo wake katika masuala ya amani na umoja hakitafanikiwa kutwaa dola. Amiri Jeshi Mkuu wa nchi anatakiwa aonekana kuwa ni mtu mwenye nia thabiti kuhakikisha amani na mshikamano wa wananchi vinadumu ndipo hapo vitu kama uhuru wa kujiamulia mambo utakuwepo, haki itatendeka kwa kila mmoja na maendeleo.
Hauwezi kuwa na uhuru, haki na maendeleo katikati ya Vurugu na kukosa mshikamano yaani amani na utangamano wa nchi vikiwa havipo.