Kwanini CHADEMA ina ushawishi zaidi mitandaoni

Asilimia kubwa ya watu wanaotumia mitandao wanashabikia cdm.
Asilimia kubwa pia ya watu wasiotumia mitandao pia wanaiunga mkono cdm.
Asilimia kubwa ya watz wanaunga mkono mabadiliko kwani ccm wameonekana matapeli na wanyonyaji
 
Mkuu huogopi kutukanwa?!!!
Ukiwa jf, unaweza kutoka mbio na kwenda kujificha vunguni mwa kitanda kama ni mwanachama wa Chama kingine. Njoo mtaani Huku Sasa; utachoka na kucheka. Nikijibu swali lako, kwa mtazamo wangu, hii inatokana na ukweli kuwa Wana muda zaidi huko au niseme wamewekeza zaidi huko. Mfano, humu Kila baada ya dakika Moja dada Erythrocyte au Lord Denning wanaanzisha mada ya kujihakilishia kushika nchi🀣🀣🀣
Ukisoma mada zao, kama upo karibu na ikulu unaweza kutoka nje ukachungulia maana unaweza dhani lissu yupo ikulu tayari na mama Samia anatoka mbio na miguu kama alivyownda Nape kuomba msamaha.
 
Mkuu huogopi kutukanwa?!!!
Ukiwa jf, unaweza kutoka mbio na kwenda kujificha vunguni mwa kitanda kama ni mwanachama wa Chama kingine
Unaogopaje maoni ya mtu mwingine kwenye jukwaa huru kama JF! Niko hapa toka 2008 sijwahi umizwa wala kukasirishwa na maoni tofauti na yangu.
 
Hakuna watanzania wengi mtandaoni
Watanzania walioko mitandaoni wako huru zaidi kutoa ukweli wa moyoni.
Hii inamaanisha kuwa hata wasio kwenye mitandao wengi wao wanaipenda CHADEMA.
CCM tubadilishe sera na mfumo wetu wa kuendesha chama.
 
Hoja zako ni kweli tupu
 
Utekaji, uonevu na unyanyasaji unaofanywa na watawala ndio chanzo kikuu cha nguvu kubwa kubaki mitandaoni.

Siasa za wazi zenye usawa kujinadi Kwa wananchi CCM haiwezi kutoboa ndio maana Kwa kuliona hili wamewekeza kwenye uhalamia wa kuumiza watu.
Watu wengi kwasababu ya uoga na kujali maisha yao wameamua kubaki mitandaoni.

Ni suala la muda tu, watu uoga utawaisha na ikifikia hii siku kama CCM hawatobadili mbinu kuna hatari yakutokea machafuko mabaya sana, CCM itambue tu hakuna uonevu wa milele na siasa ni science sio mabavu.
 
Mitandaoni ndio kuna jamii ya wasomi zaidi...utafiti wa TWAWEZA ulipata kurhibitisha kwamba CHADEMA inapendwa zaidi na wasomi kuliko ilivyo CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…