Kwanini CHADEMA wameshindwa kumchunguza Heche?

Wewe na mwenzako juma, hapo udom munapaswa kustafishwa kwa nguvu, muna Fanya ushezi TU hapo chuoni munafikiri serikali haijui ?
 
Ccm mmejaa mipasho by the way ifike 2030 bila katiba mpya ndio mtaelewa vizuri labda mkimbie nchi tofauti na hapo jiandaeni kisaikolojia.
 
Kwamba hoja inayofadhiriwa na ccm iaminiwe ni wapumbavu pekee ndio wanaweza kufanya hivyo.
 
Wekeni basi ushahidi hata robo tu, tuone pa kuanzia.

Naona MNAACHAMA tu.
 
Ccm mmejaa mipasho by the way ifike 2030 bila katiba mpya ndio mtaelewa vizuri labda mkimbie nchi tofauti na hapo jiandaeni kisaikolojia.
CCM wataendelea kuwatawala kwa sababu wanajua mnapata kizunguzungu mkisoma sentensi zaidi ya moja. Mnangoja muambiwe na wengine nini cha kuamini.

Amandla...
 
lema, sugu,boni walisema wapi?
 
wanachukua mkondo ule ule ambao miaka yote wamekuwa wakiwatuhumu viongozi wa CCM kwa Ufisadi ambao Viongozi wa CVM pia waliendelea kudai hakuna Ushahidi.
Ok, tuhuma lukuki zimeelekezwa mara nyingi kwa watawala wa ccm. Je, huwa wanachunguzwa?
 
Mkuu,
Heche hakusema hivyo.
Alisema kuna watu wanataka kumchangia yeye. Anawaomba hiyo Michango wachangie chama.
Hilo la wasimchangie Michango yoyote kuanzia sasa ni la kwako umechomekea tu.
Samahani, hao watu walitaka wamchangie Heche kwa sababu gani? Kiongozi hawezi kuamka tu akasema hadharani msinichangie wakati hakuna michango ilowahi kwenda kwake. Kama michango ilikuwa kwa.ajili yake lazima kuna hitaji la fedha hizo! Hitaji gani alokuwa nalo Heche mpaka awatake Wanachama na sii familia au marafiki?

Kuna watu wanataka nitoe Ushahidi wa Lema, Sugu na Lissu kama kwamba wao wana Ushahidi wa Samia na Abdul mkononi. Tembeleeni mitandao yao ya X na Insta ni maneno yao wao, mimi nitaupata wapi Ushahidi nikiwa nje ya nchi?

Nilimsikia Polepole nikayachukua kama yalivyo nikitegemea CCM na rais watazijibu tuhuma zile! Haikutokea! Badala yake akatekwa!

Nitakosaje kuamini tuhuma za Polepole na kwamba Polepole alitekwa na Utawala wa rais Samia! Na tukio hilo moja tu linanifanya niamini Madai ya watu wote waliotekwa kuwa wametekwa na Serikali. Ukiniuliza mimi Ushahidi, hiyo ni kukwepa Hoja kihuni..
 
Ccm mlijaribu kuweka mtego wenu ila kwa sababu chadema sio chauma mtawadanganya kwa ubwabwa wakachomoa
 
Ni majibu kama haya ndio huwa tunapewa na CCM miaka yote! Kwenye uongozi wa Wananchi hakuna kitu kibaya kama tuhuma, uongo ukiuachwa utembee hugeuka kuwa Ukweli.
Na trust me, this will cost them big time.. Tupo hapa..
Hakuna tuhuma we mwehu, unajifanya hujui kuwa hizo tuhuma zimepikwa na mboga mboga, hizo pesa zimetoka wapi wakati mumekalia ruzuku, sasa ulidhani Heche na timu yake watafanya kazi kwa kutoa pesa yao binafsi?Mbona wewe huhoji matumizi mabaya ya pesa haramu wanazokusanya mboga mboga? nenda kahoji Mbogamboga jinsi wanavyotumia hizo hela pia kahoji ripoti ya Mkagauzi Mkuu wa Mahesabu wa Serikali kuhusu ufujwaji wa pesa za umma.
 
Mkuu wangu, maelezo yako.mengi ni nukuu ambazo umezipata mitandaoni kama mimi, hunanUshahidi zaidi ya tuhuma zote kuzisikia na majibu yakotolewa ukayapokea kama yalivyo.

Kule mtandao wa X , Lema na Sugu walisema yao, mimi siwezi chukua maneno yale kama ushahidi wangu maana sikuwepo katika kikao cha Kamati Kuu.

Na kama unakumbuka hata zile kesi za Zitto na kila Kitila tuliaminishwa walitaka kupindua Uongozi wa Chama! Sina Ushahidi huo, Kuna baadhi viongozi walihama chama wakati wa Magu kwenda CCM tuliaminishwa wamelipwa hela, Kina Kitila, Sina Ushahidi huo.

Isitoshe hata hawa wanaosemwa wamelipwa hela na CCM sidhani kama unao Ushahidi? Yawezekana hata yule alojifanya Katibu wa Chama ni mchezo wa Chadema wenyewe, asimame mtu asokuwa Katibu aweke madai hayo ili kesho yake aje kiongozi halisi amkane!

Kisheria mtu huyu alitakiwa akamatwe, afunguliwe mashtaka na Chadema lakini naona kimyaa!

Mbona kuna watu hujifanya watumishi wa Umma iwe Polisi au Afisa Usalama hukamatwa na wakafunguliwa mashtaka! Leo wanatumikia kifungo?

Huyu alojifanya Katibu wa Chadema, anaachwa kwa sababu gani ikiwa nia yake ni kukivuruga Chama? Tena Chadema ina Mawakili kibao ambao hawawezi kukaa kimya kwa upuuzi kama huu usambae kukivuruga Chama.
All I can say, something isn't right!
 
Sasa kwani alimtuhumu ni Chadema?sasa wenyewe hawana mashaka naye majirani ndiyo mnaleta mashaka hii ni akili ya wapi?
 
Kule mtandao wa X , Lema na Sugu walisema yao, mimi siwezi chukua maneno yale kama ushahidi wangu maana sikuwepo katika kikao cha Kamati Kuu.
Point! Point1
Na usichukue habari za Mchange, Selasini, Odero, Balile, Lembrus Mchome , Msigwa n.k. kuwa basis ya kutaka uchunguzi ufanywe. Unajua fika hawa wana kazi maalum, don't venture into their territory.

Ndio maana tunakuuliza , kwanini Heche na si Katibu mkuu Mnyika! huna jibu.
Tunakuuliza tone tone na maridhiano vinahusiana vipi, huna jibu.
Tunakuuliza kwanini tone tone na si Trilioni Moja ya tambuu, kashata, vitumbua na makaimati Ofisini! huna jibu.
Na kama unakumbuka hata zile kesi za Zitto na kila Kitila tuliaminishwa walitaka kupindua Uongozi wa Chama! Sina Ushahidi huo
Unamkumbuka Samson Mwigamba! unakumbuka Laptop. Unakumbuka Kitila alisema nini wakati deal limebumburuka!
, Kuna baadhi viongozi walihama chama wakati wa Magu kwenda CCM tuliaminishwa wamelipwa hela, Kina Kitila, Sina Ushahidi huo.
Lema alisema katika mkutano alifuatwa na Watu kwa amri ya Magufuli kwamba akubali awe Mbunge wa Arusha. Lema anatoa ushahidi. Unataka upi zaidi? Unakumbuka Arusha madiwani 7 kuhama kwa mpigo.
Unamkumbuka Ali Bananga na alichosema Lema kabla hajaenda CCM!
Isitoshe hata hawa wanaosemwa wamelipwa hela na CCM sidhani kama unao Ushahidi?
Tundu Lissu kasema alifuatwa na kiongozi na Abdul wakiwa na maburungutu. Leo tunajua alikuwa Wenje
Unataka ushahidi gani zaidi ya ule wa aliyetakwa kuhongwa! Wenje hajakanusha m bado unatafuta ushahidi
I mean wata deal na wapuuzi wangapi?

Kuna video ya Mwenyekiti wa BAWACHA kanda ya kati akizungumza na Sheikh mmoja. Mwenyekiti alirekodi na kuvujisha mazungumzo hayo! Sheikh hajakana! unataka ushahidi upi tena!
Mbona kuna watu hujifanya watumishi wa Umma iwe Polisi au Afisa Usalama hukamatwa na wakafunguliwa mashtaka! Leo wanatumikia kifungo?
Public service na shughuli za vyama ni tofauti. Watu wanakamatwa kwa kutumia nembo za Taifa jambo lenye hatari kiusalama. Matumizi ya nembo ya CHADEMA yana athari gani! Kuna mashtaka yanayoweza kufikishwa mahakamani na CHADEMA kama kughushi mengine ni kupoteza muda.
All I can say, something isn't right!
You could be right! na nadhani unaomba iwe hivyo kwasababu wewe ni Lissu-phobia, Xeno-Heche.
Hilo si kosa ni msimamo na mtazamo wako na tuna uheshimu.

Muhimu ni kwamba, tafuta sababu na mada legit si hizi za kina Mchange! Bro! Stand for what is right

Tusirudishwe kule kwa CUF, NCCR . Tumekuwa derailed na CCM , tunajadili Tone tone ya sh Miioni 20 tumeacha kujadili Trilioni Moja ya kununua chips dume, visheti, makaimati, vitumbua, katlesi kwa viongozi wakiwa Ofisini.
Tunataka uchunguzi wa Tone tone ! kwamba ni tatizo la Taifa, please Mkandara

i'm out
 
Unaniuliza maswala ambayo hayahusiani na Mada hii. Sijasema mahapa popote nayachukua maneno ya kina Habib Mchange ambaye kwanza sijawahi kumsoma wala kumsikiliza. Na hao wengine wote tuhuma zao nimeziona awali yao walitangilia Lema na Sugu kule X nitaanza kutia shaka nikitegemea Chadema watalifanyia kazi.

Badala yake naona utetezi usoridhisha kama wa CCM kwa viongozi wao. Nikaishangaa hii hulka ya kujitetea kwa sababu tuhuma zinatoka upande wa pili. Mnataka zitoke wapi?

Hapa Canada kuna tuhuma za Viongozi wa vyama katika.matumizi mabaya ya fedha za Umma kukaa mahotelini wakati wa vikao wakati wanaishi maeneo hayo. Imekuwa zengwe kubwa kila mmoja wao amelazimika kujitetea. Hatujaonyesha ushahidi bali ni tuhuma zimeibuliwa.

Huo ndio Utaratibu walojiwekea wenzatu wakati sisi tunakataa hata kujieleza kwa sababu ati ni tuhuma kutoka mahasidi wa Chama. Kweli mlitegemea Mnyika
Aseme nini? Mbona kwa.Mbowe alikaa kimya na mkaamini ingawa Mbowe alijitetea!

Anyway, nimeweka Uzi mwingine unaitwa IPI DHIMA YA MIUNDOMBINU...Twendeni kule tujadili maono yangu.
 

..mimi nadhani hata wanaotoa madai nao wachunguzwe.

..kwa mfano kuna waliodai tajiri wa Kihindi Nilesh Suchak kampa fedha Heche.

..Nilesh kajitokeza na kukanusha. Pia kasema alimchangia Samia mil 500.

..Pia Shekhe Alhadi kajitokeza na kumtetea Nilesh kuwa hawezi kuchangia Chadema.

..Kwa mtiririko huo wa matukio nadhani kuna ulazima wa kuwachunguza hawa wanaomshutumu Heche, ili kujua nani yuko nyuma yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…