Kwanini CHADEMA wameshindwa kumchunguza Heche?

Si kila tuhuma inatakiwa kuchunguzwa, ina maana mwehu yeyote akijisikia kusema chochote juu yako wewe unakurupuka kuchunguza utakuwa huna akili.

Mind you hii ni siasa kama kila tuhuma itachunguza ina maana kila siku chama kitakuwa kazi yake ni kichunguza tuhuma.
 
Hela za kwetu na timemruhusu azile. Wewe kinakuwasha nini? Matako yako!
 
Kinachonitia wasiwasi si tuhuma zenyewe, bali namna tunavyozijibu. Mara nyingi tunapokuwa na mapenzi makubwa kwa kiongozi au chama, tunakuwa wepesi kuamini kwamba kila tuhuma ni uzushi na kila anayezitoa ana nia mbaya. Huo ni mtazamo wa kibinadamu, lakini unaweza kuwa na madhara makubwa.

Tuhuma si hukumu. Mtu anayetoa tuhuma si lazima awe tayari ameshathibitisha kosa; ndiyo maana kuna taasisi na taratibu za kufanya uchunguzi. Vivyo hivyo, mtuhumiwa hapaswi kuhukumiwa na umma kabla ya uchunguzi kukamilika.

Ndiyo maana naamini njia bora si kutukanana wala kudhalilishana, bali kuruhusu uchunguzi wa haki na huru ufanyike. Uchunguzi ukionyesha tuhuma hazina msingi, kiongozi husika atasafishwa kwa ushahidi na mjadala utaisha. Lakini ukibaini kuna ukweli, hatua zinazostahili zichukuliwe bila kujali cheo au umaarufu wa mhusika.

Historia ya siasa zetu inaonyesha kwamba vyama vyote, vikiwa upinzani au madarakani, vimewahi kutoa tuhuma za ufisadi dhidi ya wapinzani wao na kudai uchunguzi ufanyike. Kwa hiyo, ni muhimu kutumia kigezo kilekile kwa kila mtu bila viwango viwili.

Nina imani kwamba uongozi unaojiamini haupaswi kuogopa uchunguzi. Kiongozi anayesimamia ukweli atakuwa wa kwanza kutaka jambo lichunguzwe ili ukweli ujulikane. Hilo ndilo linalojenga imani ya wananchi na kuimarisha utamaduni wa uwajibikaji katika siasa zetu.

Mwisho, tusifike mahali ambapo uaminifu kwa mtu au chama unakuwa sababu ya kukataa hata uchunguzi. Taifa lenye misingi imara ya uwajibikaji linapaswa kuhimiza ukweli ubainike, si kuuzima kwa matusi au hisia.
 
Ndiyo lengo kuu la CCM na chawa wao, kuwatoa CHADEMA kwenye reli. Speed wanayoenda nayo CHADEMA inawatisha sana Samia na mafisadi wenzake, wameamua kutumia chawa mitandaoni ambao hawajawahi kuhoji kuhusu ufisadi wa kodi za wananchi wala uhujumu wa raslimali za nchi.
 
Vieelezo gani kwa mfano ungehitaji kuviona ili roho yako isuuzike?
Ukasema kweli hapa uchunguzi umefanyika.
 
Huu ujinga ujinga wa ccm nani mwenye akili timamu atahangaika nao
 
Sisi CHADEMA tunamsubiri Humphrey Polepole aje kuchukua nafasi ya umakamu mwenyekiti ndani ya chama chetu,hapo Heche tutamuweka pembeni na uchunguzi utaanza mara moja.
Wako,
John Mnyika,
Katiba Mkuu,
CHADEMA.
 
Mimi binafsi sijamsikia Lema, Boni wala Sugu wakihoji zaidi ya kuwasikia takataka za CCM zikitema pumba,hivyo kwangu source bado ni CCM.

Lakini Kama ni kweli hawa wakina Lema wameliibua hili kwenye vikao halali vya chama,basis ni jambo jema tukasubiri vikao hivyo vikae tukiamini vitalisemea jambo hili.
Naamini utaratibu wa chama unafuatwa.
 
Naona mnateseka usiku na mchana
 
Kwa mchango huu, Uzi ufungwe sasa maana majibu yote na ya ziada yapo humu.
Kongole Sana ndugu Nguruvi3
 
Majibu ya takataka uliyo-post ni rahisi sana.
Lugha hii inatumika sana na baadhi ya mashabiki wa CCM dhidi ya tuhuma kutoka kwa mashabiki wa CCM.
Lugha nyingine ambayo haistahili. Hakuna mashabiki na viongozi waliokuwa perfect. Na kama chama kinashindwa kutembea na kutafuna chewing gum kwa pamoja basi kina matatizo makubwa.
Uongo mwingine. Lissu alishindwa kutoa ushahidi wa kumuunganisha Mbowe na Abdul. Ushahidi pekee uliokuwepo ni clip iliyomuonyesha Lissu akimshukuru Abdul na kumuahidi kuwa atakuwa rafiki yake daima kama atafanikisha yeye kupata stahili zake. Alipobanwa kuhusu ushahidi alisema kuwa aliyemthibitishia ni marehemu bila kumtaja jina. Aidha, kwa vile ilisemekana kuwa tuhuma hizo kuhusu Abdul ziliongelewa katika Kamati Kuu ilikuwa ni jambo rahisi kuweka dondoo za vikao hivyo zilizokuwa redacted hadharani ili kuthibitisha kuwa Mbowe alihusika na Abdul. Ukimya wao unathibitisha kuwa ni sumu waliyomwaga ili kumharibia Mbowe. Ni strategy ya siasa za Marekani na sasa imewarudia.
-Don't forget that CHADEMA ni chama kikubwa and when it comes to diehard supporters there is no party you can compare with so hao diehards hawawezi kukaa kimya wanapona dhahiri kuwa uongozi umekuwa compromised, they ain't stupid.
Hao unaowaita ni die hard supporters ni wakina nani? Wengi waliokuwa na guts za kusimamia kweli wamenyamazishwa au wamejiondokea. Sasa hivi waongeaji wakubwa ni waliokuja juzi juzi tu na hawakupitia katika tanuri la moto walilopitia hao wanao simangwa. Chadema ya sasa imekuwa kama cult ambayo Dear Leaders wake hawakosei. Hawana tofauti na wapinzani wao.
Ni kitu gani cha kushangaza kuwa CCM haki kitakii mema Chadema? Shida ni pale Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinapoona kila anaekikosoa kuwa ni msaliti anayetumiwa na mpinzani wake Mkuu. Tabia kama hiyo ya ubabe ni sawa kabisa na ya chama tawala. Ndio maana ninaamini uongozi huu wa Chadema ukishika dola hautatofautiana na jinsi CCM inavyoendesha nchi.
NB: Stop exposing your hypocrisy and let them be kwani chama ni chao na malengo, mikakati, direction na goals wamejipangia wenyewe.
Yale yale. Hypocrites ni nyie ambao mnalia sasa baada ya mbinu zile zile mlizozitumia dhidi ya uongozi wenu uliopita zinapotumika dhidi yenu. Obfuscation haitawafikisha mbali. Hii ilikuwa ni nafasi ya kujitofautisha na vyama vingine kama mlivyofanya katika uchaguzi Mkuu. Ni nafasi ya kumsafisha Heche mbele ya kadamnasi. Tamko la mtu ambae anakiri kuwa ni rafiki yake sio uthibitisho. Uchunguzi ufanyike ili ukweli ujulikane na chama kiweke guard rails ambazo zitazuia tuhuma kama hizi kuibuka tena. Tuhuma kuwa suala hili lilijadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu nazo zijibiwe. Matusi sio jawabu.

Amandla...
 
Kuna mtu unamuheshimu sana
Unajua ni Mjenga hoja na Msomi mzuri.

Ghafla unakuta ameanza kuandika upumbavu kama Pascal Mayala.

Nadhani tungejikita Kwenye Agenda nzito za nchi kuliko cheep propaganda,

1. Watanzania wanakamatwa kila kona ya nchi CCM na selikali yake wanasema ni Ugaidi wewe unaamini.

2. Watu wanataka maandamano ambayo ni haki ya kikatiba CCM wanasema waandamanaji wamepanga kukata watu vichwa wewe unaamini.

3. Lissu amepewa kesi ya uhaini na ugaidi wewe kwa akili zako hizo mgando unaamini.

4 Samia alisema walioandamana Octoba 29 sio Raia wa Tanzania.
Wewe unaamini.

5. CCM na selikali wamepigwa kwenye mikutano ya CHADEMA wewe ulivyokuwa mpumbavu unaamini

Sina muda wa kuandika lakini.

AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO.
PUMBAVU.
 
Ok, let's take it slow - 2 questions

1. Unaweza kunipa Ushahidi unaodhihirisha CCM ndio chanzo cha tuhuma hizi?
2. Lema, Sugu na Boniface ni CCM au kuna mtu kawatuma?
  • Mtu huyo nani?
  • Kwa nini hawajahojiwa?
Tupe ushahidi wako kwanza kwenye hizi tuhuma zako no 2, usiseme 'umesikia'
 
This is another nonsense. Kamchunguze wewe kama inakuuma sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…