Kwanini Chato iwe Mkoa kutoka kwenye Mkoa mchanga wa Geita ulioundwa 2012?

Hivi mbona mnaisena geita tu wakati inamegwa mikoa mitatu?? Hivi population ya Lindi ukiitenga si utaunda mkoa wa mapori tu??
Lengo la kufanya chato iwe mkoa ni zao la ubinafsi wa magufuli. Huwezi kujiengua kutoka mkoa mdogo sana wa Geita ukaunda mkoa mwingine tena huku ni kuharibu rasilimali za nchi.
 
Swadaktaaah, ubinafsi wa mtu mmoja, uigharimu serikali nzima ya watu mil60.
Mwendazake aendee tu!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
" The United States of America (U.S.A. or USA), commonly known as the United States (U.S. or US) or America, is a country primarily located in North America. It consists of 50 states, a federal district, five major unincorporated territories, 326 Indian reservations, and some minor possessions.[g] At 3.8 million square miles (9.8 million square kilometers), it is the world's third- or fourth-largest country by total area.[c] With a population of more than 331 million people, it is the third most populous country in the world. The national capital is Washington, D.C., and the most populous city is New York City".
Nimekuwa najifikiria sana tena sana ukubwa wa USA na nchi yetu nani zaidi? Sijasikia USA wakianzisha majimbo kwa kumega jimbo jengine kwa kigezo cha kusogeza maendeleo, sie hatulali kwa kufikiria kubuni mikoa. AIBU tupu.
Uko sahihi kabisa. Kwa nini kusifanyike utaratibu wa nchi nzima wa kusogeza hayo "maendeleo" huko wilayani, katani nk. Ili wale walioko huko wilayani wasiwe na haja sana ya kufuata maendeleo makao makuu ya mikoa, iwe ni pale itakapobidi sana lakini mahitaji makubwa yawe huko huko wilayani.
 
Chato kuwa mkoa haijakaa vyema. Hii ilipaswa kuachwa kama wilaya ndani ya mkoa wa Geita.

Kwanini chato iwe mkoa kutoka kwenye mkoa mchanga wa Geita?

Ikumbukwe Geita ilitengwa kua Mkoa mwaka 2010 kipindi cha Jakaya tena iweje mkoa mchanga utoe mkoa mwingine wa Chato? Soma Kikwete atangaza mikoa, wilaya mpya

Serikali ingepaswa kuangalia mikoa mingine mikubwa ndio iweze kuikata kuzaa mikoa mingine, mfano mikoa inayostahili inaweza kua Tabora, Morogoro, Tanga, Singida, Ruvuma, n.k

Kuna haja gani ya kuunda mkoa Mpya wa Chato? Serikali iliangalie hili lasivyo kutakua na utitiRi wa mikoa kwa kila Rais ajae.

View attachment 1800958
_______________________________
Rejea Taarifa hizi

Geita yaridhia kuanzishwa Mkoa wa Chato. RCC yatoa mapendekezo. Baadhi ya maeneo kutoka mikoa jirani. RC Geita Mhe Rosemary Sitaki awashukuru Wananchi kukubaliana kwa hekima bila ushabiki.

Kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa - REGIONAL CONSULTATIVE COMMITTEE (RCC), Kilichokaa kama kikao Maalum leo kwaajili ya Mapendekezo ya kuunda Mkoa Mpya wa Chato, Kimependekeza yafuatayo:

1. Mkoa Mama wa Geita ubakiwe na Wilaya tatu ambazo ni Wilaya ya Geita, Mbogwe na Wilaya ya Nyang'hwale.

2. Imependeleza iombwe Wilaya ya Sengerema ambayo ipo Mkoa wa Mwanza, ili iweze kukamilisha Wilaya nne za Geita pamoja na Wilaya Pendekezwa ya Busanda.

3. Mkoa wa Chato imependekezwa kwa iundwe na Wilaya za Geita ambazo ni Chato yenyewe, na Wilaya ya Bukombe.

4. Pia imependekezwa kutoka Kigoma, iombwe eneo kutoka Wilaya ya Kakonko, pia kutoka Kagera imependekezwa ziombwe Wilaya mbili ambazo ni Biharamulo na Wilaya ya Ngara.

Mapendekezo haya yamekamilika na yamekubaliwa na wajumbe wote wa RCC.

Sasa yatapelekwa kwenye Wizara husika ili yaweze kufanyiwa kazi.

Nini maoni yako kwenye hili?

Nimetazama ramani, inakuwaje mtu atoke Buseresere kwenda kufuata huduma Chato badala ya Geita

1622483162256.png
 
Ujumbe huu kutoka Facebook kwenda kwa Mhe.Tibaijuka na wenzake !

MKOA WA CHATO NA SIASA ZA KANDA YA ZIWA NYUMA YA PAZIA
1622538043139.png
Nimesoma maandiko kadhaa kuhusiana na kuundwa kwa Mkoa wa Chato. Huwezi kuelewa vzr kinachoendelea sasa bila kujua siasa za Kanda ya Ziwa zilizopo nyuma ya pazia. Labda niwaeleze kidogo mambo ambayo yako nyuma ya Pazia na huwa hayaelezwi katika forum rasmi ili maamuzi ya busara yafanyike katika hili.

Kwanza kabisa nataka niwajulishe jambo moja. Chato ipo katikati ya Bukoba na Mwanza. Kutoka Chato hadi Bukoba ni takribani km 200 kama ilivyo kutoka Chato hadi Mwanza km 200. Kusini mwa Chato kabla ya kulifikia Jiji la Mwanza kuna mji wa Geita yapata kama km 100. Na Kaskazini mwa Chato kabla ya kuifikia Bukoba kuna mji wa Muleba yapata km 132. Mashariki mwa Chato mwanzo mwisho kuna Ziwa Victoria na Magharibi mwa Chato kuna Biharamulo yapata km 61, na Ngara yapata km 130.

Ukweli ni kwamba wilaya ya Ngara iko mbali sana na Bukoba ni km 300 ! Pia wilaya ya Kakonko iko mbali sana na Kigoma ni km 284 ! Haya ni maeneo ambayo zamani yalikuwa mapori lakini kwa sasa yana makazi mengi ya watu wanaohitaji huduma ya karibu.
Ukiangalia kwa makini hasa kwa masuala ya huduma, Runzewe ni kama imeunganika na Nyakanazi. Na Nyakanazi kihuduma imeunganika na Kakonko kuliko Kakonko na Kibondo. Nyakanazi pia imeunganika na Lusahunga. Lusahunga imeunganika na Biharamulo. Runzewe imeunganika na Bwanga. Bwanga imeunganika na Biharamulo. Maeneo yote hayo pamoja na Ngara yako mbali na mikoa yao yaani Kigoma, Kagera na Geita ukilinganisha na Chato ambayo iko katikati ya maeneo hayo. Idadi ya watu Kanda ya Ziwa imekuwa inakua kwa kasi sana na kuzaliwa kwa Mkoa wa Chato kunatoa solution ya umbali wa huduma ya mkoani kati ya Kakonko kwenda Kigoma na Ngara kwenda Bukoba.

Sasa mzizi wa tatizo linaloibuka kuhusu ukinzani wa kuanzishwa Mkoa wa Chato nyuma ya Pazia umegubikwa na sababu za kikabila hasa ugomvi wa kiasili kati ya Biharamulo na Chato. Na pili watu waliojeruhiwa na Mwendazake Mwendazake wanahakikisha hakuna kizuri cha Mwendazake kinakatisha bila kukitia nyongo. Hawataki Mwendazake "apate furaha yoyote" huko aliko wakidhani ni fursa yao ya kulipiza kisasi.

Kwanza ieleweke kwamba Chato ilikuwa mojawapo ya tarafa za wilaya ya Biharamulo ambayo ni wilaya iliyoko Mkoa wa Kagera. Wakazi wa wilaya ya Biharamulo ni Wasubi ambao kutokana na kuwepo Mkoa wa Kagera kwa muda mrefu wamekuwa wakichukuliwa kama jamii ya Wahaya. Ukiwa nje ya Mkoa wa Kagera watu hujua Wahaya tu. Migration ya Wasukuma kutoka Geita iliwafanya waijaze Chato kiasi kwamba baadaye Chato ikawa kama Sukumaland. Japo Chato kuna makabila mengi (Wasukuma, Wasubi, Wahaya, Wazinza na Wajita) lakini kabila ambalo limekuwa dominant ni Wasukuma.

Ukiwa pale Chato mjini lugha kuu ni Kisukuma. Ukiingia kwenye Kata za Chato Kisukuma ndio lugha kuu kasoro kata moja iliyoko karibu na Biharamulo inayoitwa Kasenga. Sasa baada ya Wasukuma kuwa dominant Chato, wakawa wanaona shida kwenda mkoani Bukoba. Walitamani kuwa sehemu ya Mwanza lakini Mwanza ilikuwa kushoto kwao kwa sababu ili ufike Mwanza lazima uvuke maji. Ulipoanza mkoa wa Geita, Chato ikapumua kwamba "tumetoka Uhayani". Lakini Hayaland wakaona eneo Lao limemegwa kwenda sukumaland.

Mtakumbuka kwamba mkoa wa Kagera awali ulikuwa na wilaya tano za Bukoba, Biharamulo, Muleba, Ngara na Karagwe. Wilaya zote hizo zilionekana kama ni Hayaland. Mwendazake alipambana kuwa Mbunge wa Biharamulo kuanzia mwaka 1990 lakini alishindwa kwa sababu hizo za "anatoka usukumani". Katika uchaguzi wa mwaka 1990 Mwendazake alishinda kata zilizoko Mashariki mwa Biharamulo (Chato) ambako kuna Wasukuma wengi waliohamia kutoka Geita.

Hata asili ya Mwendazake ni kwenye visiwa vya Nkome vilivyopo Kaskazini Magharibi mwa Geita ambavyo vinapakana na visiwa vya Rubondo kuliko na Hifadhi ya Taifa. Biharamulo wanatoka Wasubi ambayo ni kama jamii ya Wahaya. Ni watu conservative sana. Ikaonekana ili Mwendazake apate jimbo lazima Biharamulo igawanywe. Ile Sukumaland ya Biharamulo iitwe Biharamulo Mashariki. Na baadaye ikaitwa Chato. Kipindi cha utawala wa Mzee Mwinyi, Biharamulo ikagawanywa na kupatikana Biharamulo Mashariki ambayo ndio Chato. Ulipofanyika uchaguzi 1995 Mwenzazake akashinda kirahisi hilo Jimbo. Hayaland wakaona eneo lao limetekwa usukumani na kubadilishwa jina kuitwa Chato. Kukawa na uhasama wa maneno ya kisiasa kati ya Chato na Biharamulo. Mwendazake alivyoingia tu madarakani kama Mbunge 1995 akawa Naibu Waziri wa Ujenzi. Wakati huo vuguvugu la Chato Biharamulo lilikuwa limepamba moto.

Baada ya kukosa kura 1990 na kushinda 1995 na hasa alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi ukaibuka uvumi kuwa Mwendazake kawaapia watu wa Biharamulo kwamba lami wataisikia tu kwenye radio. Ni uvumi ulioenea kwa kasi sana. Kwamba Mwendazake aliongea kwa Kisukuma. Eti alisema "Butabaaba du eebiharamulo mutaleebona elami" (Haki ya Mungu nyie watu wa Biharamulo lami mtaisikia tu).
Eti pia aliwaapia kwamba Chato itasonga mbele kwa kasi kubwa kuliko Biharamulo kwa sababu Wasukuma ni watu wa kazi. Wasubi na Wahaya ni wavivu walikuwa wanawachelewesha Wasukuma.

Uvumi huo ulitamalaki zaidi hasa baada ya Mwendazake kuanza kujenga barabara ya lami inayopitia Chato kutoka Bukoba badala ya kupitia Biharamulo. Ili muweze kunielewa vzr labda kwanza niwaeleze jiografia ya barabara inayounganisha Tanzania na Kanda ya Ziwa Magharibi yaani barabara anayetoka Kahama hadi Kagera. Ni kwamba ili ufike Kagera kutokea Kahama unaweza kuamua upitie Chato au Biharamulo. Ukipita Chato unapita Ziwani kama Dar Chalinze kupitia Bagamoyo na Ukipita Biharamulo unapita "Bara" kama Dar Chalinze kupitia Kibaha&Mlandizi. Junction ya kufanya maamuzi ya kupitia Chato au Biharamulo iko kwenye mji mmoja unaitwa Runzewe ambao uko karibu na Nyakanazi.

Sasa ukiamua kupitia Biharamulo maana yake ni kwamba kutoka hapo Runzewe utaenda mpaka Nyakanazi-Lusahunga-Biharamulo-Kyamyorwa-Muleba-Bukoba. Na ukiamua kupitia Chato kuanzia hapo Runzewe route itakuwa Runzewe- Bwanga - Chato -Kyamilyorwa-Muleba-Bukoba. Sasa, sehemu kubwa ya route ya Biharamulo barabara hiyo inapita porini katika pori la hifadhi la Biharamulo ambalo kwa sasa imekuwa Mbuga ya Burigi Chato, Lakini ukipitia Chato unapita ukanda wa Ziwani ambao ndio una miji mingi ya watu.
Kutokana na hilo, Mwendazake wakati akiwa Waziri wa Ujenzi na kutokana na ushawishi wake alianza kujenga barabara inayopitia Chato ambayo sio barabara ya Kitaifa. Barabara ya kitaifa ni ile inayopitia Biharamulo.

Hoja ya Mwendazake ni kwamba ni Bora kuanza kujenga lami kwenye makazi mengi ya watu kuliko kuanzia "porini" maana jukumu la serikali ni kuwasogezea huduma wananchi. Hiyo hoja watu wa Biharamulo hawakuielewa kwa kuwa kama Taifa kipaumbele kilitakiwa kuwekwa kwenye barabara ya kitaifa badala ya barabara ya Mkoa. Baada ya barabara hiyo kujengwa gari nyingi sana za Mwanza - Bukoba zikawa zinapitia Chato. Mji wa Chato ukakua kwa kasi ukilinganisha na Biharamulo.

Kutokana na uwingi wa watu unaoongezeka kwa kasi kanda ya Ziwa upo umuhimu wa kuanzisha Mkoa wa Chato lakini changamoto zinazoibuliwa zina harufu ya ukabila kwamba kwanini Wahaya kutoka Ngara na Bukoba wahamishiwe usukumani.
Ni kweli Mwendazake alikuwa anapapenda sana nyumbani kwake. Na alitamani pawe na maendeleo makubwa. Nadhani haya pia ni matamanio ya mwanasiasa yoyote mwenye akili timu. Lakini uamuzi wa kupeleka maendeleo kwake kwa nia ya kuanzisha Mkoa wa Chato ameujengea hoja zinazoingia akilini.

Why Mkoa wa Chato ni muhimu. Utasababisha kuyaunganisha maeneo ya Kakonko, Nyakanazi, Lusahunga, Ngara, Biharamulo, Bwanga, Runzewe na kupata huduma ya mkoani karibu kwa umbali chini ya km 150 badala ya kulazimika kusafiri mpaka km takribani 300 unaenda mkoani.
 
Chato ilikuwa kijiji ndani ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.
Baadaye ikawa wilaya ikimegwa kutoka Biharamulo.
Ulivyoundwa mkoa mpya wa Geita mwaka 2012 Chato ikawekwa mkoa huo mpya, ikiondolewa kutoka mkoa wa Kagera.

Hakuna haja wala hoja kabisa ya kuanzisha mkoa mpya eneo hilo. Ni mtu alitaka kulazimisha tu.

Hali ibaki ilivyo, wilaya za Biharamulo na Ngara zibaki Kagera, wilaya ya Kibondo ibaki Kigoma, na wilaya ya Bukombe ibaki Geita.
 
Ujumbe huu kutoka Facebook kwenda kwa Mhe.Tibaijuka na wenzake !

MKOA WA CHATO NA SIASA ZA KANDA YA ZIWA NYUMA YA PAZIA
View attachment 1804588

Umetulia sana kutoa uzi huu ingawa nikusahihishe kidogo kwamba Nkome siyo kisiwa bali ni mji mdogo katika mwambao wa Ziwa Victoria ulioko Tarafa ya Bugando Wilaya Geita. Aidha nikukumbushe tu kwamba karibu robo tatu ya Wilaya Biharamulo kwa sasa wakazi wake ni wasukuma. Wasubi wamebaki kama visiwa vidogo katika bahari ya usukuma. Si hivyo tu hata hizo kata za shimwanyi na hapo Kyamuyorwa zilizoko wilaya ya Muleba ni wasukuma watupu. Na sasa wameshaanza kuhamia Karagwe kwa wingi sana.
 
Asante sana mkuu kwa maelezo nimekuelewa vyema.
Ila huu mpango wa Chato inatakiwa ufeli ibaki kuwa wilaya tu.
 
Chato ilikuwa kijiji ndani ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.
Baadaye ikawa wilaya ikimegwa kutoka Biharamulo.
Ulivyoundwa mkoa mpya wa Geita mwaka 2012 Chato ikawekwa mkoa huo mpya, ikiondolewa kutoka mkoa wa Kagera.

Hakuna haja wala hoja kabisa ya kuanzisha mkoa mpya eneo hilo. Ni mtu alitaka kulazimisha tu.

Hali ibaki ilivyo, wilaya za Biharamulo na Ngara zibaki Kagera, wilaya ya Kibondo ibaki Kigoma, na wilaya ya Bukombe ibaki Geita.
Chato inataka kuwaz na kisimati yaani kutoka kijiji-kata-wilaya na sasa iwe mkoa mwisho watakuja kusema iwe nchi.
 
Back
Top Bottom