Kwanini Chrome inatumia data nyingi kuliko hata Youtube

Kwanini Chrome inatumia data nyingi kuliko hata Youtube

Am For Real

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2023
Posts
323
Reaction score
770
Nimekuwa Nikipata tatizo naweka bando ndani ya muda Mchache naambiwa nimefika asilimia 70 ya kiwango Cha matumizi.

Nikaanza kupunguza matumizi ya YouTube na App zingine za video ila Cha ajabu nilipokuja kufuatilia nini kinaendelea kuhusu MB zangu Kwa kutumia data plan naweza Kuta Chrome imetumia hata MB 300kwa dakika kumi wakati YouTube Kwa dakika hizo nakuwa nimetumia MB 50.

Wakulungwa na wataalam wa JF NISAIDIENI.
 
ni pc au simu, kama ni pc huenda labda umeinstall plugin za crypto minning bila kujua. ila pia Chrome is a memory hungry beast.
 
ni pc au simu, kama ni pc huenda labda umeinstall plugin za crypto minning bila kujua. ila pia Chrome is a memory hungry beast.
Ni simu Kaka naweza nisiangalie muda mwingine hata video nikashinda JF napo Kwa kuibia ibia ila nikashangaa MB 500 Nimenunua naambiwa Salio ghafla linakaribia kuisha hapo sijaangalia video yoyote nimejinyima kabisa.
 
Nitjuaje sasa kama website haipo secured
website yeyote inayoanza na http: haiko secured, Secured web zote zinaanza na https:

Sasa ukiaccess hizo website data zako haziwi secured, Hackers bots wanaona then wanachange website automatic unakuta imedirect sehemu nyingine..

Wanaweza pia wakainstall automatically data za site zao kwenye simu yako ambapo zinakua zinafanya kazi kimyakimya na kulamba bando yako.

kadiri unaaccess hizo site browser yako inazidi kua uchi, unazidi kushambuliwa, Badae browser inakua dhaifu kabisa hata uki access secured sites bado itaelekeza kwingine, Unakua Hacked na hizo bots Tayari ...

SOLUTUION: Delete browsing data , futa kila kitu for all time then Nenda kwenye Privacy settings ; Switch to enhaced Security..

Baada ya hapo tafuta tena kitu kinaitwa Thirdpart cookies , chagua option yeyote inayosema Block Thirdpart cookies...

Then usi access tena Website yeyote inaanzia na Http: Sababu sio secured kama ni ya mhimu basi Tumia vpn mda wowote unapoaccess hizo sitess..

Mfano wa hizo unsecured sites ni Porn sites ,Dating sites , Illegal Shopping sites , kwasababu zinataka uweke Personal information kama credit information , Picha zako, passwords kiasi kwamba inakua rahisi kuibiwa au Kufatiliwa (kuwa hacked), au Taharifa zako kutumika kwenye uhalifu ...

Mimi mwenyewe nina Bot yangu nimeitengeneza special kublock chochote kinachohusu ngono na betting, Kuna siku bot ya kampuni X ya ngono ilileta pop up, Bot yangu ikaanza kupigana aisee nilipigika, Servers za hawa jamaa ni hatari....
 
Kama unatumia android nenda settings - App management - fungua app moja moja nenda Mobile data&wifi - Background data iweke OFF, Fanya hivyo kwa apps zote. Wakati umewasha data hivyo vi apps vina run kimyakimya na kula data. Ndo chanzo cha kulaumu Voda, tigo etc wezi wa bando kumbe settings za simu. Wale wa iphone mtajijua wenyewe.
 
Nipe elimu kidogo hapa ndo inakuaje
Kuna nyakati wajanja wanatumia simu au computer yako kumine cryptos via extensions au plugins au apps we wadhani umeinstall hiki kumbe resources za pc yako zinatumika kumnufaisha mtu na unakuta watu wengi wameinstall bila kujua so kwa pamoja anakuwa na system moja yenye nguvu ya kumine. Mara nyingi huitwa cryptojackers
 
Back
Top Bottom