Kwanini chuki kubwa inapelekwa kwa Wachina japokuwa hawakututawala?

wazanaki

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2020
Posts
1,092
Reaction score
808
Wakuu hebu leo tuongelee hili swala. Katika mitandao ya kijamii tunaweza ona anti China movement ni nyingi kuliko anti west movements. Au ni kwa sababu wachina wako simple. Kwanini tuna attack sana wachina japokua wote tunajua historia na tunajua ni nini tulifanyiwa, nani alitufanyia na tunaendelea kufanyiwa katika mfumo tofauti.

Hii chuki kwanini ina concetrate sana kwa wachina ambao hatuna historia mbaya nao.

Hii inanikumbusha pia South Afrika (xenophobia) kwamba, wa South Afrika wanafukuza waafrika wenzao wageni wakati waliowachapa viboko miaka 400 na wakachukua ardhi yao wapo wanachekelea.

Ni kwamba waafrika wameumbwa kujichukia kiasi hicho. Pia kwann tunaonesha unafiki linapokuja swala la kutenda haki kwa wote, kwa nn tunaangalia kundi lisilo na power ndo tunashambulia.

Hii ni kama story ya club. Kwamba watu wawili wamesababisha bia yako kumwagika, ila kati ya wale watu 2 mmoja ni baunsa, unanyanyuka unampiga yule ambae sio baunsa afu baunsa unamuacha. Hii ni moronic behavior sijawahi ona.
 
Siku ukibahatika kuishi/ kufanya nao kazi na Wachina ndiyo utarudi kuja kubadilisha huu uzi wako hapa.

Nakwambia; Afadhali ya WaArab kuliko Wachina.

Hilo swali lako kawaulize Vijana au MaEngineer wanaofanya kazi na Wachina hapa kwetu. Utapata jibu zuri sana na litakalokufungua Macho.

Kuna 'Mambo' mengi yanayoendelea hapa nchini yanayofanywa na hawa tunawaita eti ni 'Marafiki' au sijui 'Wawekezaji' na 'Wanaotudai kwa Mikopo yao' yakiumiza Wazawa na hakuna kitu Serikali inafanya.
 
Ndio. Lakini mbona tunavunga kusahau kuhusu waliotutawala. Kwa sababu hata mchina anachofanya anamuiga yuleyule aliemtawala. Kumbuka european pia walimtawala mchina
 
Leo sehemu yoyote watuulize wadau wa ujenzi kati ya European countries na Chinese yupi wa kufanya nae kazi utapata majibu.mchina analipa ujira mdogo
 
European wepi waliomtawala Mchina? Ni sehemu tu ndogo ya China yaani Kisiwa cha Hong Kong ndio ilitawaliwa na Britain lkn hadi leo angalia tofaiti ya wachina wa Hong Kong na wale wa Mainland China
 
Waafrika wamekuwa watumwa wa historia kila siku ukoloni ukoloni ukoloni

Ukiwa mtumwa wa historia hautaweza kusonga mbele, cha muhimu ni kuangalia kwa sasa kati ya China na West ni nani anayekupa better terms? Kama ni West basi nenda na West kama ni China nenda na China, sio kuanza ku judge mambo kwa historia, utakuwa kipofu
 
Leo sehemu yoyote watuulize wadau wa ujenzi kati ya European countries na Chinese yupi wa kufanya nae kazi utapata majibu.mchina analipa ujira mdogo
Technically unasema kua mchina hakunyonyi vizuri, yani anakunyonya bila hata kukudanganya ili usistuke, ila mzungu anakunyonya vizuri, kwa sababu anakufanya usistuke kua unaliwa

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Mchina Ni mpupambufu San haajali haki za binadamu Wala kuangaika na maisha ya mtu mweusi ktk khaki hao watu siyo POA kbsabora mzungu Mara Mia apewe kandarasi za Barbara na migodi kuliko
Ni kwasababu mzungu anatumia akili kukunyonya, so ni bora adui ambaye hajifichi au adui anaeweza kukulaghai ww usiweze kumtambua kama ni mbaya, yupi ni adui ambae ni mbaya zaidi.
Ni kwamba tu mchini yuko hinest hataki kukudanganya kua yuko fair, waafrika tunapendwa sana kudanganywa kama mwanamke anaependa uongo wa mwanaume na ukimwambia ukweli mnakosana

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
European wepi waliomtawala Mchina? Ni sehemu tu ndogo ya China yaani Kisiwa cha Hong Kong ndio ilitawaliwa na Britain lkn hadi leo angalia tofaiti ya wachina wa Hong Kong na wale wa Mainland China
Kumbe walitawaliwa, mbona hata afrika ethiopia haikutawaliwa, kubali kuwa hata mchina alitawaliwa. Kubali tu

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Ni kwasababu mzungu anatumia akili kukunyonya, so ni bora adui ambaye hajifichi au adui anaeweza kukulaghai ww usiweze kumtambua kama ni mbaya, yupi ni adui ambae ni mbaya zaidi.
Ni kwamba tu mchini yuko hinest hataki kukudanganya kua yuko fair, waafrika tunapendwa sana kudanganywa kama mwanamke anaependa uongo wa mwanaume na ukimwambia ukweli mnakosana

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
Kwa kifupi wachina wako honest, kama anakuchukia haoneshi unafiki. Ni kama waarabu, ni bora niishi na mtu wa hivo kuliko mnafiki

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Tunatofautiana nao jamaa mazingira yao ni kazi, kazi, kazi, kazi
Sisi tumejizoeza na umaskini wetu kazi kidogo BATA jingi!

Siyo Wachina Tu. Wakorea, Wafilipino, Wajapan ndiyo kabisaah kazi mpaka wao serikali inatoa amri majengo yazimwe taa. Watu wakalale, wapumzike!

Wakija Bongo, mbongo anapigiwa simu oyaah nakuja, dereva kachelewa,
Secretary anakuambia haji kibaruani kwa sababu Jana kulikuwa na kigodoro!
Wengine wakija hawatimizi majukumu!

Wizi, dereva anaiba mafuta, SGR Mwanza, madereva wanapiga nyoka mafuta, mpaka unajiuliza sasa nchi itajengeka kweli!?
 
Back
Top Bottom