Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Maonesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji bidhaa ya China (CIIE) yanafanyika mjini Shanghai, na kuzishirikisha nchi za Afrika.
Kwenye maonesho hayo, Tanzania imekuwa mgeni wa heshima kwa mara ya kwanza, huku Benin, Burundi na Madagascar zikishiriki kwa mara ya kwanza katika maonyesho haya ya kimataifa. Katika kipindi cha miaka saba tangu kuanzishwa kwa CIIE, maonesho hayo yamezidi kuvutia nchi za Afrika.
Awamu hii ya CIIE itaendelea kutoa vibanda bure kwa nchi zilizoko nyuma kimaendeleo zaidi barani Afrika.
Takwimu zinaonesha kuwa, katika miaka 7 iliyopita, CIIE kwa jumla yametoa zaidi ya vibanda 500 bure kwa nchi zilizoko nyumba kimaendeleo zaidi barani Afrika.
Aidha, mwaka huu ni mara ya pili kwa maonesho hayo kuanzisha eneo maalum la bidhaa za Afrika. Ili kutekeleza makubaliano ya ushirikiano yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa Kilele wa mwaka 2024 wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, mara hii, eneo hilo limepanuliwa hadi mita 225 za mraba, kwa ajili ya kuonesha bidhaa za kampuni 25 kutoka nchi 13 maskini za Afrika, zikiwemo Madagascar na Msumbiji.
Kwa nchi zenye rasilimali chache za Afrika, kama vile Madagaska, Mauritania na Lesotho, CIIE yametoa uungaji mkono maalum ili kuzisaidia kuonesha bidhaa zao.
Tanzania imeshiriki katika CIIE kwa miaka sita mfululizo. Huu ni mwaka wa 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Tanzania, hivyo Tanzania ilichaguliwa kuwa mgeni wa heshima wa maonesho hayo.
China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Tanzania kwa miaka minane mfululizo, mwaka jana thamani ya biashara kati ya nchi hizo mbili ilifikia dola bilioni 8.78 za Kimarekani.
Na CIIE imetoa mchango muhimu kwa mafanikio haya. Katika miaka 7 iliyopita, bidhaa nyingi zaidi za Tanzania zikiwemo Parachichi, kahawa, divai nyekundu, asali, zimeingia kwenye soko la China kupitia CIIE. Mara hii, idadi ya kampuni za Tanzania zilizoshiriki kwenye maonesho hayo imevunja rekodi tena.
Licha ya bidhaa za kilimo, pia wameleta bidhaa za Sanaa za mikono zikiwemo Tingatinga na sanamu zilizotengenezwa kwa mikono.
Ethiopia pia ni mgeni wa kudumu wa CIIE. Safari hii, Ethiopia imeleta kahawa zake tena. Hivi sasa chapa za kahawa za Ethiopia kama vile Yirgacheffe zinajulikana sana katika soko la China. Tangu kushiriki kwake kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya CIIE mwaka wa 2019, umaarufu na mahitaji ya kahawa ya Ethiopia nchini China vimeendelea kukua.
Tanzania na Ethiopia ni mifano mizuri ya nchi za Afrika zilizopata mafanikio katika CIIE. CIIE ni kama daraja linalovuka umbali wa maelfu ya kilimota, na kuleta bidhaa za Afrika kwa wateja wa China.
Kwa imani ya waoneshaji wengi wa Afrika, kushiriki katika CIIE kunamaanisha kukumbatia soko kubwa la China na fursa za maendeleo zisizo na kikomo.
Kwani hapo awali, kampuni za Afrika zililazimika kupitia wafanyabiashara wa kati ili kuuza bidhaa zake nchini China. Lakini sasa kutokana na CIIE, wanaweza kuunganishwa moja kwa moja na wateja wa China na kupata oda kubwa ana kwa ana.