Jamaa wanajitahidi sana...haswa Sumaku ni moja Waigizaji wanaonivutia ndio maana huwa nafuatilia huu mchezo, ila nadhani Sumaku hatumiki fully kwa uwezo alio nao.
Huwa namsikia hata kwenye michezo mingi ya redio kwenye redio tofauti tofauti...kwa sasa kuna mchezo wa redio RFA namsikia unaitwa 'kumekucha' I think.
ILA UKWELI LAZIMA USEMWE JAPO NI MCHUNGU
Hawa jamaa wananikera sana...wapo hewani kwa muda mrefu, zaidi ya miaka kumi sasa kama sikosei lakini sioni maendeleo yoyote haswa kwenye sanaa wanayoifanya...production bado ni poor na ya kimasikini sana.
Inakera kuona kipindi kikongwe na waigizaji wakongwe wa kiwango kile kutengeneza mchezo unaohitaji kuonyesha tukio la siku tofauti na Waigizaji wanashindwa hata kubadili nguo..ile sio stage play, ingawa hata stage play wanafanya zaidi ya hapo.
Production kwa sehemu kubwa inafanywa nje (outdoor) kwa lengo kubwa la kukwepa gharama, haya si ya kufanywa na kundi kama lile tena wanaofanya kazi na TV kubwa kama ITV. Tatizo ni nini? vifaa? sasa kama wao inawashinda hao underground wataweza vipi iwapo watasema tunataka kuwa kama Mizengwe?
Kuna mdau hapo juu naona ameshauri waongezewe muda...nadhani ameshindwa kunotice kwamba jamaa hawana 'content' inayotosheleza, ubunifu unagotea hapo na kwamba wanategemea sana uwezo wa Muigizaji binafsi kusukuma muda, ndio maana utaona huwa wanavuta muda sana kabla kuanza kipindi ili walau wafikie muda..kile kipindi ni cha nusu saa kutoka tatu kamili au na dakika mpaka tatu na nusu, lakini hawajazi huo muda wewe unasema waongezewe.
Sasa sijui tatizo lao haswa ni nini, huwa mpaka najiuliza kama Mzee mengi kweli huwa anajali ni nini kinafanyika kwenye kampuni yake. Labda wanakosa washauri wazuri au wao wenyewe hawana cha kushauriana na kampuni yao (ITV)
Sifa kuu ya binadamu/kazi/biashara yoyote ni kukua kutoka ulivyokuwa awali, hata binaadamu asiye 'grow' hana lolote la kufunza wengine.....Wanaofuatilia Isidingo hapa hebu waniambie jinsi inavyoenda ikibadilika, sio lazima waigizaji wabadilishwe lakini walau production, mandhari n.k.