Kwanini Comedians wa MIZENGWE wanapotezewa sana?

Kwanini Comedians wa MIZENGWE wanapotezewa sana?

Tena wako more natural kuliko hawa bongo movie celebrities ambao utafikiri kuna ubao umeandikwa mahali ndio wanasoma
 
Ni vizuri kusikia wanafuatiliwa kwani hata mimi nimfuatiliaji ndio maana nimeona niainishe yale ninayodhani ni mapungufu yanayoonekana wazi yapo ndani ya uwezo wao iwapo tu watatulia.

Na ningetamani nione wamekuwa wakubwa na kujulikana mbali kuliko ilivyo sasa.

Wasijifungie tu na kukubali sifa za kuwa wao hawajishughulishi kutafuta umaarufu/audience...sio sifa nzuri hata kidogo hiyo..asikwambie Mtu msanii yeyote moja ya sifa yake kuu ni kujulikana/kupendwa na kuwa midomoni mwa Watu wengi kadri inavyowezekana, na hilo ni jukumu lao na si la mwingine yeyote kwani hata manufaa watakayopata yatabaki kuwa ni ya kwao.
umeongea vyema. nafikiri wanaye meneja wao. hawa kwa aina ya uigizaji wao wangeweza kuwa na venue ya kuperform kila week na hata kuzunguka mikoani.
 
umeongea vyema. nafikiri wanaye meneja wao. hawa kwa aina ya uigizaji wao wangeweza kuwa na venue ya kuperform kila week na hata kuzunguka mikoani.
Walau mpo mnaonielewa, ni bora kuwa na wachache wanaoelewa kuliko kupotosha wengi.

Mizengwe wana fursa ya kufika mbali, na wakumbuke kuna wengi mtaani wanatamani fursa kama waliyonayo wao, ni jukumu lao kuhakikisha wananufaika 'to the fullest' kwa vipaji vyao.

Ni msanii gani ulimwengu huu hatotamani kuwa famous? Pilipili hafanyi makubwa sana lakini jina lake ni kubwa kuliko anachofanya, jamaa nao lazima 'wauze' kundi liwe namba moja nchini wapate manufaa zaidi.
 
Hv hawa wasanii huwa wanakuwa funded vipi ? Wanalipua kisa mtaji sasa mitaji inapatikana vp ?
Sijui wanafanyaje kazi na ITV, lakini kamwe sivutiwi na uduni wa production kwa Watu waliopo kwenye fani miaka kumi sasa au zaidi...wapambane wasibweteke.

Ningetamani leo hii nione kazi zao zinashindana na zile za Citizen tv Kenya ,Papa Shirandula, Habibu n.k.
 
Sioni kwanini nipoteze muda na Wewe wakati hata ID yako tu inatosha kueleza kuwa hata nifanyeje huwezi kunielewa hasa ukizingatia kuwa Wewe ni ' fyatu ' kweli.
Huna lolote ndugu, Mtu akipingana na unachoamini wewe unatukana hovyo, iwapi busara kwako?
 
Wale jamaa noma ,kabla tv yangu haijaaribika (mwishoni mwa utawala wa jakaya) nilikuwa sikosi kuwaangalia hao jamaa
 
Huna lolote ndugu, Mtu akipingana na unachoamini wewe unatukana hovyo, iwapi busara kwako?

Busara ipo ' Mbinguni ' tu na hapa duniani ni ' mbele kwa mbele ' na ' kanyaga twende '.
 
Hawa jamaa wana uwezo mkubwa sana..yaan robo saa tu wanafikisha ujumbe effectively na wanaeleweka sana..big up sana kwao
 
Habarini Wadau,

Mbona waigizaji wa Mizengwe ni wazuri sana na wana vipaji ila hawapewi recognition sana kama comedians wengine?

Japo kipindi chao cha jumapili kinachorushwa na ITV ni kifupi ila watu kama SUMAKU, MKWERE, MARINGO 7 na wengineo ni waigizaji wazuri kweli, haswa Sumaku.

Pia michezo yao ina mafunzo kwa jamii.

Kwanini wanasahaulika?
katika ulimwengu wa sasa msanii asipowekeza kwenye platifomu ya social media hufiki popote,nguvu ya mitandao ya kijamii ni kubwa sana,bahati mbaya wale wa mizengwe siwaoni mitandaoni kabisaaa
 
Kwani tanzania kuna Comedian?
hahaaaaa wajifunze kwa wenzao basi
sio kuchekesha maneno bali vitendo. kama maneno kwa asiejua lugha hiyo je?
hawaoni wanavochekeaha wenzao kina Mr Bean kina Chaplain au Kelvn Hart...
ndomaana me siangaliagi utumbo huo wa Mizengwe nk.
Huyo Kelvin Hart anachekesha kwa kutumia nini kama siyo maneno?
 
Back
Top Bottom