Maelezo mengi lakini hauja jibu nilicho uliza ,zaidi umekwenda mbali kwa kuonesha wanufaika wa Mali ya DRC.Hao wanaoiba Madini ni kutoka nchi za Magharibi, in short vifaa vyote tunavyotumia kutype hapa vimejaa damu za Wacongo. Bila cobalt hutengenezi battery na circuit za motherboard, na Congo ndio ina supply Asilimia zaidi ya 70 ya Cobalt duniani, wanaochimba hio cobalt ni watoto wadogo mno na ni kama serikali ya Congo haifadiki na chochote.
Kukiwa na Congo imara ina maana watakuwa na say na Cobalt yao. Bei itapanda na wanaweza wakamuuzia yoyote, China, Urusi na wengineo, na tukiwa tunaelekea ulimwengu wa Magari ya Umeme umuhimu wa cobalt unazidi kuwa Mkubwa.
So solution ni hio ku distabilize nchi ili watu wajichotee hizo Mali,
Mwanajeshi halimi, hafanyi biashara wala haingizi kipato chochote na ana Gharama kubwa mno, kuanzia kumvisha, kumlisha, kumnunulia Silaha, kumtrain etc hakuna popote pale Duniani ambapo kuna muasi asiye supportiwa na nchi nyengine, hakuna, huwezi endesha jeshi kwa ulimwengu wetu wa sasa bila Supply na Logistic za hao mabwana wakubwa.
South Africa Kuna mali mbona kumetulia,shida ya Congo iko kwa Wacongomani wenyewe.