Kwanini Congo DRC?

South Africa wana madini, Tanzania tuna madini, Ghana, Burkinafaso n.k why Congo DR?
Boss na kujibu comment ya mwisho maana naona kichwa chako kigumu sana kuelewa.

Thamani ya Madini ya Congo ni Trilioni 24 za Kimarekani sawa na hela za madafu Shilingi Quadrilion 60 ama sawa na Kina MO dewji 24,000

South Africa ni kama 1/10 ya Congo thamani ya Madini yao Trilioni 2.5 za Kimarekani, Tanzania sisi ni kama kitone tu, tupo kwenye Vi billion bado.

Unachouliza hapa ni kwanini Majambazi wanaiba bank ama Banda La Mpesa kwanini hawaibi kwenye Genge la Nyaya ama mama muuza mboga.
 
China ndio anachakua 70% ya Cobalt yote ya Congo. China inamiliki migodi 15 kati ya migodi 19 ya Cobalt huko DRC.
 
Wachina ndio wanunuzi wakubwa wa Cobalt ya Congo, kati ya 70% hadi 80% ya raw Cobalt yote ya DRC inaenda China. Pia China inazalisha theluthi mbili ya processed Cobalt duniani.
 
China ndio anachakua 70% ya Cobalt yote ya Congo. China inamiliki migodi 15 kati ya migodi 19 ya Cobalt huko DRC.
Analipa na wewe unaongelea Cobalt ya kihalali sikatai, na hii hoja yako Ina prove my point kwamba Cobalt ikiuzwa kihalali Mchina ama Mrusi wangeinunua kwa wingi kuliko western powers. Kifupi west hawataki kulipa wanataka njia za mkato ikiwemo hata kuua na kusababisha machafuko ili wapate hayo Madini.

Tunachoongelea hapa ni yale Madini yanayoibiwa. Mfano nimeweka juu link ya EU kusign mkataba na Rwanda kununua Madini kwa ajili ya Magari ya Umeme na solar panel, Rwanda ana haya Madini? Hana yanatoka wapi kama hana? We mwenyewe unajua yanatoka wapi

Kila siku tunaambiwa Rwanda ana support machafuko Congo na tunaona Rwanda anawauzia Nchi za Magharibi haya Madini.
 
Vita vinasaidia supply ya Madini west kuongezeka (wanahusika na smuggling) Amani inasaidia Maslahi ya Congo kuongezeka wataweza kuuza kwa wanayemtaka.
Mbona Kazakhstan, Brazil, Chile, Peru na Australia hakuna vita vya wenyewe kwa wenyewe??
 
Western powers wanunue Cobalt nyingi kuliko China wapeleke wapi wakati viwanda vikubwa vinavyohitaji hiyo Cobalt kwa sasa viko China??

China, Taiwan, Korea Kusini na Japan ndio wazalishaji wakubwa zaidi wa electronics na magari duniani.
 
Mbona Kazakhstan, Brazil na Australia hakuna vita vya wenyewe kwa wenyewe??
Australia ni kama Usa Wanaongoza wao siku kukiwa hakuna serikali inayo wasuport utaona, na Kazakhstan siku nyingi kuna puppets inajulikana, hata Congo kipindi kuna puppet wao (Mobutu) waliridhika, Brazil ana Madini mengi ila sio muhimu kwamba anategemewa Brazil tu. Issue ya Congo ni Unique huwezi kui replicate kokote pale, Cobalt ndio Madini muhimu sasa hivi, muhimu kushinda hata mafuta, Bila cobalt hakuna Magari ya Umeme, hakuna iphone, hakuna Laptop, hakuna, redio, hakuna AC hakuna kifaa chochote cha electronic.

Haya makampuni makubwa Duniani

Apple, Nvidia, Microsoft, Alphabet (Google), Amazon, Meta, Broadcom, Tesla, Tsmc, Samsung na wengine wengi wote Value yao ina Revolve around Cobalt,

Kama leo Congo inastopisha Cobalt na kufunga mpaka yote yanatetereka hayo na Tunaanza kutafutana humu, that's how important Cobalt is. Utafananisha na Nchi gani na Dini gani?
 
Ni upumbavu wa Wacongo wenyewe, mengine yote ni excuse za kipumbavu.
Mtu nchi yake iko vitani yuko somewhere ughaibuni hana hata uchungu unamsikia "papaa nikufege juu ya nini, mie ni myuzisiee". Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa za Banga ndiyo alisababisha watu kutokuwa na uzalendo, alifanya watu wakapoteza uzalendo kwa jinsi alivyoiongoza nchi kiubinafsi kama Tanzania inapoelekea watu wanapoteza uzalendo kwa jinsi nchi inavyoendeshwa kiubinafsi.
 
Vita ya Congo haijaanza leo, vita vya DRC vimeanza kabla hata ya uwepo wa smartphones, laptops na magari ya umeme.
 
Huu ndo ukweli ambao watu wengi wanajifanya hawaujui
 
Inaonesha unapenda fujo sana wewe...! Lianzishe kwenye familia yako itatosha, sio lazima Tizedi nzima iingie vitani
 
Western powers wanunue Cobalt nyingi kuliko China wapeleke wapi wakati viwanda vikubwa vinavyohitaji hiyo Cobalt kwa sasa viko China??

China, Taiwan, Korea Kusini na Japan ndio wazalishaji wakubwa zaidi wa electronics na magari duniani.
Kampuni kubwa inayo Tengeneza Vifaa vidogo vidogo vya Ndani vya Electronic Broadcom ni ya Marekani, kuna Apple, Tesla na wengine wengi, sababu wana manufacture China (Assembly) haimaanishi eti from scratch imetengenezwa China,

Kuna lawsuit kibao za haya Madini

Hii Congo wanawashtaki Apple kwa kununua illegal mineral ya Congo kupitia Rwanda



Hapa Whistleblower ametoa ushahidi kuhusu Apple wanavyo Smuggle na Apple wakakakataa ku comment.

Unaona utofauti hapa? China ama Migodi na Analipa Congo, anawasaidia hadi kutengeneza miundombinu kama Barabara zaidi ya Trilioni 10 kawekeza, Ila Apple kampuni kubwa zaidi Duniani ina nunua Cobalt Rwanda na kwa Waasi, bado unataka ushahidi?
 
Kama leo Congo inastopisha Cobalt na kufunga mpaka yote yanatetereka hayo na Tunaanza kutafutana humu, that's how important Cobalt is. Utafananisha na Nchi gani na Dini gani?
Nickel na Manganese ni mbadala wa Cobalt, hata Congo isipokuwepo leo wafanyabiashara wa battery na electronics wataendelea na biashara zao kama kawaida na kuendelea kupiga pesa, Waafrika acheni ujuha wa kujifikiria nyie ni alpha na omega, dunia ni kubwa sana na kila kitu kina mbadala wake.
 
Ni hivi, ni rahisi zaidi Waafrika kuwafungulia mashitaka kama hayo wazungu kama Apple, BAE systems n.k kwa sababu wanaonekana kujali. Wachina hawajali mambo ya illegal mining, blood diamonds, human rights,
child labour n.k na huwezi kupata chochote kwao hata ukidai. Wachina hapo DRC hawachoti madini tu, hadi magogo wanavuna kiharamu kwenda kutengenezea furniture kwao China. Halafu Wachina wao wanaingia front kabisa kuvuna rasilimali tofauti na Western wanaoutumia third parties.
 
Nchi gani ina Madini yenye thamani kama $24 trillion?
Nchi inayo ongoza kwa Rare earths ni China lakini haina hali iliyo nayo Congo toka kupata uhuru wake 1949

Tanzania wizi wetu wa madini upo kimikataba ya hovyo tunayo saini sioni kwa namna gani unaweza kuitetea Congo na Wacongo.
 
South Africa reserve yao ya Madini $2.5 Trilioni, Congo $24 Trilioni. Mbinguni na Ardhi.

Hakuna Africa Hii nchi yenye Madini hata robo tu ya Congo,
Wacongo ni watu wa ajabu kwanza wanajeshi la hovyo sana
 
Maelezo mengi lakini hauja jibu nilicho uliza ,zaidi umekwenda mbali kwa kuonesha wanufaika wa Mali ya DRC.

South Africa Kuna mali mbona kumetulia,shida ya Congo iko kwa Wacongomani wenyewe.
Wewe nae ukasome unataka kutafuniwa kila kitu alaahh😀😀😀

Sasa huo utajiri wa South ni cha mtoto au huo wa Angola au Tz bado sana hiyo cobalt CONGO DR inachangia 70% na kuendelea huko katika matumizi ya utengenezaji wa vifaa vya kielectronic na madini mengine mengi mengi yapo hapo shamba la bibi ni kwa wenye nguvu kujichotea.

Msijisifu sana kuwa nyie mko poa smuggling inayoendelea hapo Afganistan ukifatilia kupitia report mbalimbali hamna cha kuwashinda Congo DR😀😀

Ukiwa na Mali nyingi sana kuwa na stable government ni impossible watakusaliti tu.Case study nchi zote za kiarabu zenye mafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…