Hatufiki hata asilimia 1 ya Congo Madini yao na rasilimali zao, unailinganisha sisimizi na Nyangumi mkuu.
Estimation ya Madini ya Congo ni $24 trillion, sijui hata nikuelezeje ila it's a lot of money. Kama hayo Madini yanauzwa kwa haki kwa pamoja basi Immediately Congo inakua Nchi ya pili Tajiri zaidi Duniani na GDP per capita inakuwa ya kwanza Duniani.
Na Madini yao sio tu urembo kama ya kwetu bali ni Madini ambayo yameshikilia Dunia, Cobalt inatumika na kifaa Chochote cha Electronic iwe Simu, laptop, gari Na mengineyo. Soko lake kwa Dunia linafika hadi $30B ila Congo wanapata tu visenti.
Congo imara ina maana watakaza, wao ni monopoly wanazalisha zaidi ya Asilimia 70 ya Cobalt hivyo wanaweza ku regulate bei, so ili watu wasifike huko inabidi nchi iwe undermined watu waendelee kuiba.