Kwanini Congo DRC?

Kwanini Congo DRC?

Hatufiki hata asilimia 1 ya Congo Madini yao na rasilimali zao, unailinganisha sisimizi na Nyangumi mkuu.

Estimation ya Madini ya Congo ni $24 trillion, sijui hata nikuelezeje ila it's a lot of money. Kama hayo Madini yanauzwa kwa haki kwa pamoja basi Immediately Congo inakua Nchi ya pili Tajiri zaidi Duniani na GDP per capita inakuwa ya kwanza Duniani.

Na Madini yao sio tu urembo kama ya kwetu bali ni Madini ambayo yameshikilia Dunia, Cobalt inatumika na kifaa Chochote cha Electronic iwe Simu, laptop, gari Na mengineyo. Soko lake kwa Dunia linafika hadi $30B ila Congo wanapata tu visenti.

Congo imara ina maana watakaza, wao ni monopoly wanazalisha zaidi ya Asilimia 70 ya Cobalt hivyo wanaweza ku regulate bei, so ili watu wasifike huko inabidi nchi iwe undermined watu waendelee kuiba.
mining-of-rare-earths-by-country.png
 
Wewe nae ukasome unataka kutafuniwa kila kitu alaahh😀😀😀

Sasa huo utajiri wa South ni cha mtoto au huo wa Angola au Tz bado sana hiyo cobalt CONGO DR inachangia 70% na kuendelea huko katika matumizi ya utengenezaji wa vifaa vya kielectronic na madini mengine mengi mengi yapo hapo shamba la bibi ni kwa wenye nguvu kujichotea.

Msijisifu sana kuwa nyie mko poa smuggling inayoendelea hapo Afganistan ukifatilia kupitia report mbalimbali hamna cha kuwashinda Congo DR😀😀

Ukiwa na Mali nyingi sana kuwa na stable government ni impossible watakusaliti tu.Case study nchi zote za kiarabu zenye mafuta.
Congo wapuuzi na anayetetea upuuzi upuuzi naye yupo kwenye kundi moja sehemu nyingi tu duniani zina mali nyingi na zina amani
mining-of-rare-earths-by-country.png
 
Boss na kujibu comment ya mwisho maana naona kichwa chako kigumu sana kuelewa.

Thamani ya Madini ya Congo ni Trilioni 24 za Kimarekani sawa na hela za madafu Shilingi Quadrilion 60 ama sawa na Kina MO dewji 24,000

South Africa ni kama 1/10 ya Congo thamani ya Madini yao Trilioni 2.5 za Kimarekani, Tanzania sisi ni kama kitone tu, tupo kwenye Vi billion bado.

Unachouliza hapa ni kwanini Majambazi wanaiba bank ama Banda La Mpesa kwanini hawaibi kwenye Genge la Nyaya ama mama muuza mboga.
Dogo anakichwa kizito alafu sijui mtu unasmart phone na kuna ma AI kibao ila bado mtu unakuta yuko slow namna hii,bure kabisa!!!
 
Cobalt ndio Madini muhimu sasa hivi, muhimu kushinda hata mafuta, Bila cobalt hakuna Magari ya Umeme, hakuna iphone, hakuna Laptop, hakuna, redio, hakuna AC hakuna kifaa chochote cha electronic.
Usije ukazungumza huu ujinga mbele ya watu wenye akili, watakuona kilaza sana.
 
Vita ya Congo haijaanza leo, vita vya DRC vimeanza kabla hata ya uwepo wa smartphones, laptops na magari ya umeme.
Ni same Madini, Electronic sio simu tu. Cobalt inatumika kwenye circuit za motherboard na battery, hadi redio za kizamani zimetumia cobalt. Kifupi Cobalt imeanza kuchimbwa since enzi za ukoloni hata kabla hawaja pata uhuru ubelgiji walikua wanachimba.

Mobutu aliwekwa madarakani kwa sababu Congo walikuwa wanauza Cobalt USSR walivyopata Uhuru. akawekwa yeye wauze West.
 
Ni upumbavu wa Wacongo wenyewe, mengine yote ni excuse za kipumbavu.
Mtu nchi yake iko vitani yuko somewhere ughaibuni hana hata uchungu unamsikia "papaa nikufege juu ya nini, mie ni myuzisiee". Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa za Banga ndiyo alisababisha watu kutokuwa na uzalendo, alifanya watu wakapoteza uzalendo kwa jinsi alivyoiongoza nchi kiubinafsi kama Tanzania inapoelekea watu wanapoteza uzalendo kwa jinsi nchi inavyoendeshwa kiubinafsi.
Punguza jazba leta hoja zenye mashiko acha kutupa lawama hovyo.

Wewe unajua kuwa Tanzanite ipo Tz pekee ila leading seler ni India😀😀😀

Dunia haina haki,mwenye nguvu mpishe!!!
 
Cobalt ndio Madini muhimu sasa hivi, muhimu kushinda hata mafuta, Bila cobalt hakuna Magari ya Umeme, hakuna iphone, hakuna Laptop, hakuna, redio, hakuna AC hakuna kifaa chochote cha electronic.
Huu ni ujinga.

Umekazania Cobalt Cobalt
 
Ni same Madini, Electronic sio simu tu. Cobalt inatumika kwenye circuit za motherboard na battery, hadi redio za kizamani zimetumia cobalt. Kifupi Cobalt imeanza kuchimbwa since enzi za ukoloni hata kabla hawaja pata uhuru ubelgiji walikua wanachimba.

Mobutu aliwekwa madarakani kwa sababu Congo walikuwa wanauza Cobalt USSR walivyopata Uhuru. akawekwa yeye wauze West.
Umekazania cobalt cobalt kama vile Congo pekee ndio inahodhi hayo madini
 
Kazakhstan ina madini yenye thamani ya $46 Trillion.
Mainly Mafuta na Uranium, yana bei ila sio Nchi moja inayohodhi, assume Kazakhstan angekua na yeye ana 70% ya production ya Mafuta/Uranium halafu anauza Urusi kungekalika pale?

Mfano mzuri angalia Venezuela ama Urusi wana mafuta ila wamepigwa pini kwanini? Sababu wana sehemu nyengine wanaweza pata hayo mafuta, mfano Nchi za kiarabu, ila kusingekua na Nchi za kiarabu na mafuta kahodhi tu Venezuela kingenuka siku nyingi tu pale.
 
Cobalt sio rare, ni abundant, watu wana okota juu juu, it's just Congo ana zaidi ya asilimia 50 ya reserve yote Duniani na yupo responsible kwa 70% ya Supply ya Dunia.

Rare earth mineral ni kitu chengine nacho kina kazi yake hasa kwenye semiconductor industry na leading edge nodes.

Nani kasema cobalt ni rare earths.

Rare earths ndio muhimu kwa duniani ya sasa na inayokuja mpaka kupachikwa jina la gold of the 21st century na huyo Congo unayemtaja hayupo kwenye charts kubwa
 
Kuna nchi zilishawahi kuingia katika misukosuko ya kisiasa lakini hatimaye zilikuja kutukia. Rwanda ni mojawapo.

Kwanini imekuwa tofauti nchini Congo DRC?

1. Tatizo ni uongozi? Angepatikana huko kiongozi kama NYERERE, au KAGAME au MAGUFULI angeweza kuituliza?

2. Wasababisha machafuko ya Congo DRC wana nguvu kuliko wazuiaji?

3. Hulka ya raia wa Congo DRC inachangia?
Swali la msingi kabisaa
Kwa nn Congo?
Maana almost zaidi ya miaka 40 sasa hakuna utulivu kabisaa
 
Mainly Mafuta na Uranium, yana bei ila sio Nchi moja inayohodhi, assume Kazakhstan angekua na yeye ana 70% ya production ya Mafuta/Uranium halafu anauza Urusi kungekalika pale?

Mfano mzuri angalia Venezuela ama Urusi wana mafuta ila wamepigwa pini kwanini? Sababu wana sehemu nyengine wanaweza pata hayo mafuta, mfano Nchi za kiarabu, ila kusingekua na Nchi za kiarabu na mafuta kahodhi tu Venezuela kingenuka siku nyingi tu pale.
Korea Kaskazini na Cuba wamepigwa pini kwa sababu wana nini??
 
Back
Top Bottom