Kwanini CWT inataka serikali tatu?

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
"CWT yataka serikali tatu"


Rais wa CWT, Gratian Mukoba.

Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kimependekeza kuwepo kwa Serikali tatu katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na kuundwa kwa Tume ya utumishi wa walimu ambayo itahusika na ajira ya walimu, kuwalipa mishahara na mambo muhimu yanayohusu walimu.

Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema uamuzi huo mefikiwa baada ya kupitia katika vituo vyake zaidi ya 21,500 na mwamba walimu walikubaliana na kuwasilisha maoni hayo kama CWT.

Sambamba na maoni hayo, chama hicho kimeitaka Serikali kuboresha hali za walimu kwanza, kabla ya kuboresha mpango wa matokeo makubwa sasa (Big Result Now) wa kuinua kiwango cha elimu nchini kwani watekelezaji wakuu wa mpango huo ni walimu.
Mukoba alisema jana kuwa katika mpango huo walimu ni watekelezaji wakuu japo hawaelewi au kupewa semina elekezi ya nini hasa ¡®Big Results Now¡¯.

¡°Mpaka kufikia mwezi uliopita madai ya walimu yaliyowasilishwa kwa katibu mkuu, Ofisi ya Rais ni madeni ya Sh. bilioni 40 ambayo walimu tunaendelea kuidai Serikali ambayo bado haionyeshi dalili ya kutulipa kutokana na kutaka kupeleka ripoti kila mara bila kuzifanyia kazi,¡± alisema Mukoba.


CHANZO: NIPASHE
 
Tatizo la Mkoba nikujifanya mwanaharakati huku ni mnafiki WA kutupwa nani kamwambia sisi walimu tunataka serikali tatu? Sisi tunataka maslahi yetu na serikali 2.
 

Wala historia haikutumhusu kujenga Zanzibar iwe Taifa. Uhuru wa kutoka kwa mkoloni ulipatikana tarehe 10 Desemba, 1963: na Mapinduzi ya kung'oa usultani wa Mwarabu yalifanywa tarehe 12, Januari 1964. Hatukujenga nchi mbili.


Katika UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA Mwalimu J.K. Nyerere alimulika mengi ila machache niliyom-quote walau yanafaa kusomwa na watu wa aina ya Mkoba!
 
Kama kweli sisi tumeunda, basi kwanini serikali mbili wala si serikali moja? Nadhani hapa ndo wengi tunajikwaa! Endapo tungeunganisha zote (complete mix), basi kila mara tusingekuwa tunaona serikali mbili, wala mtazamo wa kuwa huyu akitoka bara, basi yule atoke Zanzibar. Maana wote ni wamoja, lengo letu ni moja, basi tutekeleze serikali moja, rasilimali ziwekwe pamoja, wabara wakienda zenji wasibaguliwe kufanya biashara au kununua ardhi, na hakuna kusema serikali mbili tena. Otherwise, uhuru waliopigania wazee wetu kina Kinje, Rumanyika na wengine haukuwa na maana kama miaka michache baada ya uhuru , UHURU huo huo uliuzwa kwa muungano usioeleweka tena kwa bei ya kutupa!
Katika UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA Mwalimu J.K. Nyerere alimulika mengi ila machache niliyom-quote walau yanafaa kusomwa na watu wa aina ya Mkoba!
 
Tulikuwa Nchi Mbili, lakini kwa hiari yetu wenyewe, tukaamua kuwa Nchi Moja. Kwa sabaabu ambazo nimezieleza mara nyingi, na kama hapana budi nitaendelea kuzieleza, tukakubaliana kuwa ni Muungano wa Serikali Mbili.

J.K. NYERERE

Pamoja na matatizo mengi bado naendelea kukubaliana na mwalimu kwamba tukikubali kufufua Tanganyika basi tutakuwa tumeiua rasmi Tanzania!
 
J.K. NYERERE

Pamoja na matatizo mengi bado naendelea kukubaliana na mwalimu kwamba tukikubali kufufua Tanganyika basi tutakuwa tumeiua rasmi Tanzania!

Ni jukunu la wazanzibar kuuenzi muungano huku wakikumbuka dhana ya mapinduzi. Tanganyika sasa yaonelea ni heri kujitenga nao maana hawataki kuenzi mapinduzi au wale waliokuwa kabla ya mapinduzi wanataka kurudi. Serikali tatu ndio suluhisho la kero za muungano sio mbili ya sasa. Ama wale waletao hija ya serikali mbili ni heri wajikite kwenye utatuzi wa mgogoro wa muungano ama wakae kimya mpaka katiba ipite.
 
serikali 3 ndo suluhisho la migogor iliopo, iwe ya kisiasa na pia ya kiuchumi,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…