kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
"CWT yataka serikali tatu"
Rais wa CWT, Gratian Mukoba.
Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kimependekeza kuwepo kwa Serikali tatu katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na kuundwa kwa Tume ya utumishi wa walimu ambayo itahusika na ajira ya walimu, kuwalipa mishahara na mambo muhimu yanayohusu walimu.
Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema uamuzi huo mefikiwa baada ya kupitia katika vituo vyake zaidi ya 21,500 na mwamba walimu walikubaliana na kuwasilisha maoni hayo kama CWT.
Sambamba na maoni hayo, chama hicho kimeitaka Serikali kuboresha hali za walimu kwanza, kabla ya kuboresha mpango wa matokeo makubwa sasa (Big Result Now) wa kuinua kiwango cha elimu nchini kwani watekelezaji wakuu wa mpango huo ni walimu.
Mukoba alisema jana kuwa katika mpango huo walimu ni watekelezaji wakuu japo hawaelewi au kupewa semina elekezi ya nini hasa ¡®Big Results Now¡¯.
¡°Mpaka kufikia mwezi uliopita madai ya walimu yaliyowasilishwa kwa katibu mkuu, Ofisi ya Rais ni madeni ya Sh. bilioni 40 ambayo walimu tunaendelea kuidai Serikali ambayo bado haionyeshi dalili ya kutulipa kutokana na kutaka kupeleka ripoti kila mara bila kuzifanyia kazi,¡± alisema Mukoba.
CHANZO: NIPASHE