SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Wengi tumejikita kwenye habari za kanuni na mabaunsa ila ngoja nipanue kidogo mjadala wa kwa nini derby ya Simba na Yanga haikuchezwa tarehe 08/03/2025.
Msichukulie huu uzi serious sanaaana ila unaweza kusaidia kupanua mawazo kidogo wakati huo huo ukitoa burudani ya hapa na pale. Tujadili bila makasiriko.
Labda ya 1: Samia Cup.
Tukumbuke ligi ya wanawake ikiwa inaelekea kuchezwa mechi ya derby ya Simba na Yanga ya wanawake, ghafla iliahirishwa ili kupisha Samia Cup kule Arusha.
Simba huwa inapata ugumu sana kujiingiza moja kwa moja kwenye siasa za uchawa. Ingekuwa ngumu sana kukubali kuahirisha derby ya wanaume kwa sababu hii na ukizingatia ina ratiba ngumu ya CAF na viporo siyo vizuri katika hatua hii. Kwa Simba kutotoa ushirikiano, wakapewa ugumu waliokutana nao. Kwa lugha nyingine, derby ikaahirishwa kwa lazima. Sasa hivi focus ipo Samia Cup.
Labda ya 2: Kifo cha Prof. Sarungi.
Hii utahitaji D mbili na walau C moja kuweza kulinyambua hili. Ngoja nipime kama kuna majiniasi watusaidie kulidadavua hili.
Halafu, hivi mbona Simba hawakuvaa vitambaa vyeusi walipocheza na TMA kwenye CRDB Confederation Cup?
Labda ya 3: Majeruhi ya Che Malone na Camara.
Simba waliona bila wachezaji hao wawili na wakati huo huo striker tegemeo Ateba akionekana kusuasua kipindi hiki, kuna dhahma ilikuwa inakuja mbele. Ukasukwa mpango mkakati.
Labda ya 4: Vita ya Kisaikolojia.
Ni wazi Simba ilikuwa inaingia kama underdog katika mechi hii. Kwa kuona ugumu wa mechi hii na umuhimu wa ushindi katika mbio za ubingwa, walichofanya Simba ni kuwashtukiza Yanga kwa kwenda kufanya mazoezi. Taarifa ilitolewa mapema ila hakuna aliyedhani Simba kweli ingeenda kufanya mazoezi. Hata kama kanuni inaruhusu, kawaida hizi timu hazikanyagi uwanja wa mechi kufanya mazoezi siku moja kabla. Huo utamaduni umekuwepo na hata uwepo wa mabausa kulinda uwanja ni sehemu ya utamaduni huo. Kuna video zilisambaa siku kadhaa hata kabla ya tukio zikionyesha mabaunsa wakilinda uwanja. Wanaowakana mabaunsa wa Yanga wameanza kushabikia mpira juzi juzi.
Wataalamu wa Simba walijua kuna mojawapo kati ya mambo mawili yangeweza kutokea ambayo yote yangekuwa faida kwa Simba.
Kwanza, Simba ingekubaliwa kufanya mazoezi baada ya mabishano na mvutano mkubwa pale getini. Kwa sababu ya element ya surprise waliyofanya Simba, kesho yake Yanga ingeingia kinyonge na hiyo kidogo ingeifaidisha Simba. Kumbuka, watu wa Yanga wasingeruhusiwa kuingia uwanjani wakati Simba inafanya mazoezi. Hata kama Simba ingeruhusiwa kufanya mazoezi, lazima vurugu zingetokea kubwa zaidi ya zile tulizoshuhudia, ama wakati wapo bado ndani au wakati wanaondoka baada ya mazoezi. Kiufupi, Yanga wangekataa kuingia kwenye mechi hii kinyonge. Hizi vurugu za wakati au baada ya mazoezi bado zingeweza kusababisha mechi kutochezeka.
Pili, Simba kukataliwa kufanya mazoezi na hata kufanyiwa fujo na hivyo kukataa kucheza mechi na kudai pwenti 3. Hili ndiyo lililotokea.
Ongezea labda nyingine ambazo sijazitaja.