Kwanini Diamond Platnumz anavaa msalaba?

Msalaba na jumlisha Ni vitu viwili tofauti,sema ukiviangalia juu juu utaona Ni sawa, kwenye msalaba panapopishana zile alama Ni juu kidogo,wakati kwenye jumlisha Ni katikati
 
Hivi hujui kwamba kutokana na "udanganyifu" kuwa YESU alibeba "msalaba", leo hii Wakristo waliodaanganyika wanaabudu "msalaba"?

Lengo la Shetani lilikuwa ni kuwapotosha wanadamu ili waabudu sanamu pasipo wao kujua maana msalaba ni kama sanamu tu. Na lengo la shetani limetimia maana leo hii watu wanauabudu msalaba ambao ulikuwa ukitumika na dini za kishetani za kipagani.

Ni kweli kabisa kuwa Biblia itabaki kuwa kitabu kitakatifu lakini ni ile original ndiyo "takatifu" hizi zilizotafsiriwa tayari zimenajisiwa na Shetani.

Na yote hiyo ni sababu Wanadamu walio wengi wanaupenda sana uongo kuliko kweli. Na matokeo yake MUNGU ameruhusu wadanganywe na Shetani anawadanganya mno. Soma 2Wathesalonike 2:11-12
 
Narudia kukuambia tena, katika maandiko ya Agano Jipya hakukuwa na neno "msalaba" . Hapo kwenye hilo andiko neno sahihi ni "mti" au "nguzo" maana YESU alitundikwa "mtini".

Tutabishana mpaka kesho lakini UKWELI utabakia kuwa UKWELI. BWANA YESU hakubeba "msalaba" bali alibeba "nguzo".

Na isitoshe maandiko hayo ya 1Wakorintho 1:18 yanamaanisha "kitendo cha YESU kutundikwa mtini" na wala hayamaanishi watu wauabudu "mti" uliotumika.
Yaani watu wanaopinga kitendo cha YESU kufa mtini kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Kitendo cha YESU kufa mtini ndiyo hasa hiyo "message of the stauros" au "neno la nguzo au mti".
 
Maskini mtoto wa Ellen
Mimi ni mtoto wa BABA MUNGU.
Huyo ellen ndio nani?????
Kwani vitabu vya Agano Jipya, original manuscript ziliandikwa kwa lugha gani kama siyo Kigiriki??

Kama unajua Kiingereza hebu soma hii:

Language of the New Testament​



The New Testament was written in a form of Koine Greek,[1][2] which was the common language of the Eastern Mediterranean[3][4][5][6] from the conquests of Alexander the Great (335–323 BC) until the evolution of Byzantine Greek (c. 600).
 
Jibu swali, characters wa kwenye hivyo vitabu walikuwa Wagiriki au walikuwa wakitumia lugha ya Kigiriki?
What's so difficult about giving the straight answer?
Stop the blah blah and give the straight answer.
Hizo references zako si kila mtu anaziamini hivyo basi toa jibu la moja kwa moja kwa maswali hayo.
 
Mind you, nina maana the whole Bible siyo uje na references za New Testament peke yake. Nijue kama hata the likes of Abraham au Solomon au David au Moses kwa nao walikuwa wakitumia Kigiriki au original records za hadithi zao wakati wa enzi zao zilikuwa zinaandikwa kwa Kigiriki na hata kama Jesus pia alikuwa anatumia(anazungumza/anahubiri) Kigiriki.
View attachment 1860286
 
Unabishana na KJV haya.. [emoji38]
 
nadhani anavaa msalaba kama pambo tu, sio kwa imani, na sio kosa muislamu kuvaa cross au plus kwa kujipamba. Lakini tena sisi hatujui kama DIAMONDI msalaba anauvaa kutokana na imani au la! Na ingependeza zaidi aulizwe mwenyewe.
 
Msalaba ni aina ya adhabu ya wahalifu kutundikwa juu kupigiwa misumari, kabla ya Yesu kuzaliwa utawala wa kirumi ulikua ukitumiwa kwa kuwaadhibu wahalifu na Yesu alitabiri kuja kuadhibiwa kwenye msalaba na kufa juu yake tu.kwa hivyo msalaba hauna maana nyingine zaidi ya hiyo na ndio maana madhebu mengine ya kikristu kama WASABATO, hawauamini msalaba.
 
Nimekwambia soma comment namba #31 utaona nimeelezea kwa facts siyo mihemko.
Haujaelezea facts bali umeelezea hadithi ulizozisoma, ukazikariri na kuziami which in real sense is far from being facts.
 
Huo "ukweli" unaouamini ndiyo upotoshaji wenyewe wa ibilisi, hicho kigiriki hakiwezi kubeba tafsiri ya mwanzo ya matukio ya kibiblia kwa kuwa lugha muhimu ya kibiblia Ni kiebrania ( Hebrew) na siyo kigiriki Cha Athens!
Hili analijua, nia na madhumi yake ni;
a) Kutafuta justification ya kwamba Romans na Roman translations zilibadisha biblia wakati hata Greek version ni translation tena wala haikuwa first translation kutoka Hebrew.
b) Ku deceive watu waende na tune yake pasina kufahamu ya kuwa hawezi ku brainwash watu wenye akili zao na wanaotumia commonsense kwenye ku digest issues.
c) Imani aliyomezeshwa imempofusha hivyo hana uwezo wa kufikiri nje ya box.
 
yaani mbagala boy kwa snoop anaonekana mbilikimo nguchiro kabisa
 
You are good upstairs ,nimependa sana unavyojenga hoja zako with some reference
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…