Tatizo ni tafsiri iliyofanywa. Vitabu vyote vya Agano Jipya viliandikwa kwa lugha ya Kigiriki isipokuwa tu ule Waraka kwa Waebrania.
Sasa waliotafsiri mwanzoni ndiyo walikosea au walifanya makusudi hiyo haijulikani.
Iko hivi :
Katika zile original manuscript za hivyo vitabu vya Agano Jipya hakuna neno "msalaba" kwa lugha ya Kigiriki isipokuwa lipo neno "nguzo". Waliotafsiri badala ya kuandika nguzo, wao wakaandika "msalaba".
Neno linalopatikana kwenye hizo manuscript ni "Stauros". Neno hili ni la Kigiriki likimaanisha "pole" or "stake" kwa Kiingereza au "nguzo" kwa Kiswahili.
Hata neno "kusulubishwa" lilitafsiriwa kimakosa pia. Kusulubiwa Kigiriki iliandikwa "sustauroo" na maana yake halisi ni "to impale" kwa Kiingereza au "kutundika mtini" kwa Kiswahili.
Hivyo kwa tafsiri sahihi na ya UKWELI, ni kwamba BWANA YESU alitundikwa mtini na siyo alisulubishwa msalabani.
Kuna udanganyifu mkubwa sana uliofanywa kwenye Biblia na wahuni wachache kwa lengo la kuwapotosha Wanadamu wasiojishughulisha kuitafuta KWELI ya MUNGU. Udanganyifu huo ni mbinu ya Shetani kuwafanya wanadamu waabudu "msalaba" ambao ni alama yake Ibilisi.
Wengi wenu mtanibishia sababu hamijui KWELI na hii KWELI imefichwa hata mkiambiwa hamwezi kuamini. Lakini wale wachache wanoijiua KWELI wanaelewa ninachokisema.
Kitendo cha YESU kutundikwa "mtini" kilikuwa kinaakisi kile kitendo cha Musa kumtundika "mtini" yule nyoka wa shaba. Musa hakutumia "msalaba" kumtundika yule nyoka bali alitumia "nguzo ya mti". Hebu soma hapa:
8 The Lord said to Moses, “Make a snake and put it up on a
pole;(
A) anyone who is bitten can look at it and live.” 9 So Moses made a bronze snake(
B) and put it up on a
pole. Then when anyone was bitten by a snake and looked at the bronze snake, they lived.(
C)
Kwa Kiswahili:
"Bwana akamwambia Musa, jifanyie nyoka ya shaba ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa aitazamapo ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba akaishi". Hesabu 21:8-9
Sasa hapo juu utaona neno lililotumika kwa Kiingereza ni "pole" (mti au nguzo) na siyo "cross" (msalaba).
Soma Matendo ya Mitume 5:30..
"MUNGU wa baba zetu alimfufua YESU ambaye ninyi mlimwua mkimtundika katika mti".
Hapa tunaona Mtume Petro anakiri wazi kabisa kuwa YESU alitundikwa kwenye "mti". Tena ukiendelea kusoma mstari wa 32, (Matendo 5:32) utaona Petro anasema yeye na Mitume wenzake ni mashahidi wa yaliyotokea. Yaani ni mashahidi kwamba walimwona YESU akitundikwa kwenye "mti" na siyo "msalabani".
Msalaba asili yake ni "upagani". Misalaba ilianza kutumiwa na wapagani wa kale tokea enzi za Tamuz kabla hata ya Israeli kuwa taifa.
MUNGU hafungamani na kitu chochote kile cha "upagani" wala MUNGU hawezi kamwe kumuunganisha Mwanae na mambo ya kipagani. Soma 2Wakorintho 6:15-16.