Kwanini Diamond Platnumz anavaa msalaba?

Kwanini Diamond Platnumz anavaa msalaba?

Tatizo ni tafsiri iliyofanywa. Vitabu vyote vya Agano Jipya viliandikwa kwa lugha ya Kigiriki isipokuwa tu ule Waraka kwa Waebrania.

Sasa waliotafsiri mwanzoni ndiyo walikosea au walifanya makusudi hiyo haijulikani.
Iko hivi :
Katika zile original manuscript za hivyo vitabu vya Agano Jipya hakuna neno "msalaba" kwa lugha ya Kigiriki isipokuwa lipo neno "nguzo". Waliotafsiri badala ya kuandika nguzo, wao wakaandika "msalaba".

Neno linalopatikana kwenye hizo manuscript ni "Stauros". Neno hili ni la Kigiriki likimaanisha "pole" or "stake" kwa Kiingereza au "nguzo" kwa Kiswahili.
Hata neno "kusulubishwa" lilitafsiriwa kimakosa pia. Kusulubiwa Kigiriki iliandikwa "sustauroo" na maana yake halisi ni "to impale" kwa Kiingereza au "kutundika mtini" kwa Kiswahili.

Hivyo kwa tafsiri sahihi na ya UKWELI, ni kwamba BWANA YESU alitundikwa mtini na siyo alisulubishwa msalabani.

Kuna udanganyifu mkubwa sana uliofanywa kwenye Biblia na wahuni wachache kwa lengo la kuwapotosha Wanadamu wasiojishughulisha kuitafuta KWELI ya MUNGU. Udanganyifu huo ni mbinu ya Shetani kuwafanya wanadamu waabudu "msalaba" ambao ni alama yake Ibilisi.

Wengi wenu mtanibishia sababu hamijui KWELI na hii KWELI imefichwa hata mkiambiwa hamwezi kuamini. Lakini wale wachache wanoijiua KWELI wanaelewa ninachokisema.

Kitendo cha YESU kutundikwa "mtini" kilikuwa kinaakisi kile kitendo cha Musa kumtundika "mtini" yule nyoka wa shaba. Musa hakutumia "msalaba" kumtundika yule nyoka bali alitumia "nguzo ya mti". Hebu soma hapa:

8 The Lord said to Moses, “Make a snake and put it up on a pole;(A) anyone who is bitten can look at it and live.” 9 So Moses made a bronze snake(B) and put it up on a pole. Then when anyone was bitten by a snake and looked at the bronze snake, they lived.(C)

Kwa Kiswahili:
"Bwana akamwambia Musa, jifanyie nyoka ya shaba ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa aitazamapo ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba akaishi". Hesabu 21:8-9

Sasa hapo juu utaona neno lililotumika kwa Kiingereza ni "pole" (mti au nguzo) na siyo "cross" (msalaba).

Soma Matendo ya Mitume 5:30..
"MUNGU wa baba zetu alimfufua YESU ambaye ninyi mlimwua mkimtundika katika mti".
Hapa tunaona Mtume Petro anakiri wazi kabisa kuwa YESU alitundikwa kwenye "mti". Tena ukiendelea kusoma mstari wa 32, (Matendo 5:32) utaona Petro anasema yeye na Mitume wenzake ni mashahidi wa yaliyotokea. Yaani ni mashahidi kwamba walimwona YESU akitundikwa kwenye "mti" na siyo "msalabani".

Msalaba asili yake ni "upagani". Misalaba ilianza kutumiwa na wapagani wa kale tokea enzi za Tamuz kabla hata ya Israeli kuwa taifa.
MUNGU hafungamani na kitu chochote kile cha "upagani" wala MUNGU hawezi kamwe kumuunganisha Mwanae na mambo ya kipagani. Soma 2Wakorintho 6:15-16.
Unataka kutuambia kwenye biblia kuna mkono wa shetani ?, what a ridiculous comment !! Kama ni hivyo hakuna maana ya kuiita biblia kuwa ni takatifu ili Hali shetani ashaichezea tayar
 
Nimekuuliza swali wewe moja unaniletea mashairi sijui ya gazeti gani.

Nini kinayapa ujasiri na ukweli maneno yako mpaka sisi tuyaamini?

Kwanini tuamini maneno yako?

Jibu kinagaubaga usilete viroja na maneno meeengi yaliyojaa mambo ya kutungwa tu
Sina muda wa kubishana na watu wasiotaka kushughulisha akili zao
 
The Cross means many things to many people. Some have it displayed on their mantel, others wear it around their neck.The Cross means LOVE.
 
Unataka kutuambia kwenye biblia kuna mkono wa shetani ?, what a ridiculous comment !! Kama ni hivyo hakuna maana ya kuiita biblia kuwa ni takatifu ili Hali shetani ashaichezea tayar
Amini nakwambia kilichoandikwa kwenye Biblia ile original kilikuwa sahihi kabisa, lakini waliofanya "tafsiri" (translation) ndiyo waliopotosha maana halisi.

Lakini hawakuweza kupotosha kila neno na ndiyo maana leo hii wapo watu wachache wanaoujua UKWELI. Wengi wenu mpo "gizani".

Na ni kweli wala usishangae, Shetani ameweka mkono wake kwenye Biblia. Ndiyo maana kwenye Biblia kuna mstari unasema hivi:
"jaribuni mambo yote, lishikeni lililo jema na jitengeni na ubaya wa kila namna". 1Wathesalonike 5:21-22

Kama Biblia ingekuwa haijachezewa na Shetani basi Paulo asingesema, "jaribuni mambo yote, lishikeni lililo jema".

Usidanganyike, YESU KRISTO hakubeba "msalaba" bali alibeba "nguzo" na alitundikwa juu ya nguzo na siyo msalaba kama ulivyoaminishwa.
 
Unaelewa msalaba ni nini?

Je, unajua kuwa asili ya msalaba siyo "Ukristo??"

Je, unajua kuwa YESU KRISTO hakubeba msalaba (+) bali alibeba nguzo (I)?

Je, unajua kuwa kanisa la KWELI la MUNGU halitumii "msalaba" maana asili ya msalaba (+) ni upagani?

Ukijua hayo hutaona ajabu kwa Diamond Platinumz kuvaa msalaba.
Mkuu acha kudanganya watu.
 
Nini kinayapa ujasiri na ukweli maneno yako mpaka sisi tuyaamini?

Kwanini tuamini maneno yako?
Maneno yangu ni ukweli mtupu. Nimekwambia Agano Jipya liliandikwa kwa lugha ya Kigiriki cha kale kinachoitwa Koine Greece. Katika maandiko yale original ya Agano Jipya hakuna neno msalaba bali neno lililotafsiriwa kama msalaba ni Stauros na neno hili linamaana ya nguzo na siyo msalaba.

Ukweli ndiyo huo na watu wote waliojifunza theology wanaujua ukweli huu. Na wewe unaweza pia ukaujua ukweli huu na ukathibitisha maneno yangu ikiwa tu utaishughulisha akili yako kidogo kuutafuta UKWELI.

Na isitoshe Biblia yenyewe inakuelezea kuwa YESU alitundikwa "mtini" kama vile ambavyo Musa alimtundika yule nyoka wa shaba mtini. Musa hakutumia "msalaba" vivyo hivyo YESU hakutumia msalaba.

Na tena historia ya mambo ya kale inaelezea wazi kabisa kuwa msalaba ulikuwa ukitumiwa na Wapagani wa kale kabla hata YESU hajazaliwa duniani. Biblia nayo inakwambia wazi kabisa kuwa MUNGU hafungamani wala hana shirika na upagani.

Yote hayo yapo wazi lakini bado wewe unabishana na mimi.
 
Amini nakwambia kilichoandikwa kwenye Biblia ile original kilikuwa sahihi kabisa, lakini waliofanya "tafsiri" (translation) ndiyo waliopotosha maana halisi.

Lakini hawakuweza kupotosha kila neno na ndiyo maana leo hii wapo watu wachache wanaoujua UKWELI. Wengi wenu mpo "gizani".

Na ni kweli wala usishangae, Shetani ameweka mkono wake kwenye Biblia. Ndiyo maana kwenye Biblia kuna mstari unasema hivi:
"jaribuni mambo yote, lishikeni lililo jema na jitengeni na ubaya wa kila namna". 1Wathesalonike 5:21-22

Kama Biblia ingekuwa haijachezewa na Shetani basi Paulo asingesema, "jaribuni mambo yote, lishikeni lililo jema".

Usidanganyike, YESU KRISTO hakubeba "msalaba" bali alibeba "nguzo" na alitundikwa juu ya nguzo na siyo msalaba kama ulivyoaminishwa.
Sasa kuna haja gani kutumia kitu ambacho kimechezewa na shetani , kama kina mkono wa shetani hakifai kuitwa kitakatifu na hakiaminiki tena, mkuu mbna umeandika ujinga Sana aisee , Biblia ni takatifu , changamoto ni tafsri basi , na anayetafsir maandiko Kwa usahihi ni roho matakatifu Kwa njia ya maombi na kujinyeyekeza , tofaut na hapo utaishia kujitafasria na kujiwekea conclusion wewe mwenyewe, Biblia inasimama Kwa ukamilifu wake na inajitosheleza Kwa mahitaj ya binadamu , hakuna ujinga wwte shetani ashawahi kuingiza kwenye maandiko matakatifu ili kupotosha na hawezi....Issue ya msalaba na mtini hzo ni tafsiri , na hyo ipo pote , maandiko ya Kwanza kabisa yalijitosheleza Kwa lugha yake , tafsir kutoa lugha original kuja kingereza kuna ufanisi fulan ulipungua, kutoka kingereza kuja Kiswahili na other local language pia kuna ufanisi ulipungua na hzo ni changamoto za lugha ya kibinadamu , ugumu ambao hata Yohana aliupata kipind anaandika kitabu cha Ufunuo , Mbali na changamoto hzo bado maandiko yanabaki kuwa matakatifu ...!!!

Iwe alitundikwa mtini au msalabani maana au lengo la kitendo hcho halibadiliki na hakuna effect yyte Ile kiroho , ni ujinga kubishana et msalaba na mtini ,..... Concept ni kuwa Yesu alikufa msalabani ( wewe unaita mtini) ili kuokoa Ulimwengu Kwa kuwapa wanadamu second chance ya toba,...ili kila amwaminiye apate uzima wa Milele , sasa hayo mambo ya kuanza kuchunguza sjui msalaba , mara mtini mara free mason hyo ni ya kwenu sasa na yakikutoa kwenye reli hakuna mtu atahusika .....
 
Unataka kutuambia kwenye biblia kuna mkono wa shetani ?, what a ridiculous comment !! Kama ni hivyo hakuna maana ya kuiita biblia kuwa ni takatifu ili Hali shetani ashaichezea tayar
Hiyo ni point moja, ya pili ni kwamba anajua ni wapi shetani kachakachua wapi kaacha?
Kwahiyo Mungu anayetuambia Biblia ni neno lake lililo hai, lenye makali kuwili na lenye kupasua nafsi na mafuta, LIMECHAKACHULIWA na Ibilisi?

Jamaa kachemka kweli..
 
Thibitisha uongo wangu.
Unachotuambia ni kwamba Yesu hakutundikwa msalabani? Haya hebu tutoe neno msalaba kwenye hii verse, tuweke neno mti au nguzo halafu useme inaleta maana gani..

Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
1 Kor 1:18 SUV

For the message of the cross is foolishness to those who are perishing, but to us who are being saved it is the power of God.
I Corinthians 1:18 NKJV
 
Unaelewa msalaba ni nini?

Je, unajua kuwa asili ya msalaba siyo "Ukristo??"

Je, unajua kuwa YESU KRISTO hakubeba msalaba (+) bali alibeba nguzo (I)?

Je, unajua kuwa kanisa la KWELI la MUNGU halitumii "msalaba" maana asili ya msalaba (+) ni upagani?

Ukijua hayo hutaona ajabu kwa Diamond Platinumz kuvaa msalaba.

Maskini mtoto wa Ellen
 
Amini nakwambia kilichoandikwa kwenye Biblia ile original kilikuwa sahihi kabisa, lakini waliofanya "tafsiri" (translation) ndiyo waliopotosha maana halisi.

Lakini hawakuweza kupotosha kila neno na ndiyo maana leo hii wapo watu wachache wanaoujua UKWELI. Wengi wenu mpo "gizani".

Na ni kweli wala usishangae, Shetani ameweka mkono wake kwenye Biblia. Ndiyo maana kwenye Biblia kuna mstari unasema hivi:
"jaribuni mambo yote, lishikeni lililo jema na jitengeni na ubaya wa kila namna". 1Wathesalonike 5:21-22

Kama Biblia ingekuwa haijachezewa na Shetani basi Paulo asingesema, "jaribuni mambo yote, lishikeni lililo jema".

Usidanganyike, YESU KRISTO hakubeba "msalaba" bali alibeba "nguzo" na alitundikwa juu ya nguzo na siyo msalaba kama ulivyoaminishwa.
You're so brainwashed na unashindwa kutumia commonsense, yaani yale uliyokaririshwa unadhani wote humu JF wako kama wewe.
Unachagua versions za kuamini kama ulivyokaririshwa, pity you. Kigezo kipi kinakufanya uone Greek version ndiyo sahihi? Wahusika kwenye hizo story za kwenye Bible walikuwa Wagiriki au walikuwa wakiongea Kigiriki? Kama si hivyo kwanini uamini translations from the original language to Greek?
Wengine tuna akili timamu hivyo tunauwezo wa kuchambua mambo.
IMG_20210719_151158.jpg
 
Back
Top Bottom