Kwanini Diamond Platnumz hatunukiwi PHD ya heshima au tunasubiri hadi siku akitutoka

Kwanini Diamond Platnumz hatunukiwi PHD ya heshima au tunasubiri hadi siku akitutoka

issa ramadhani

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2014
Posts
1,319
Reaction score
260
Ametoa mchango mkubwa sana katika ukuzaji wa lugha adhimu ya kiswahili barani Afrika na dunia kwa ujumla. Vyuo vya Tanzania mulikeni hili hasa hasa chuo kikuu cha Dar es salaam idara ya kiswahili mchango wa huyu ndugu yetu.
 
Hapa celeb tulisha mpa heshima zote.
 
Kweli mtoa mada we ni lofa tena akili zisizo na akili.mtu kaishia darasa last saba afu huo mziki wa kihuni anaimba baada ya kuvuta bangi atunukiwe PHD? Ignorance is bliss
 
Akili za Nyumbu hizi apewe Phd kwa lipi labda?
 
Kaimba na wasanii kibao wa kimataifa kwa kutumia lugha ya kiswahili katika song zake na za featuringishwa.Mufano Bracket ft Baba tifa-alive.
anatendea haki kabisa kwenye
UHAKIKI WA FASIHI SIMULIZI
na
LITERATURE IN ENGLISHMAN
na ametumia Flashback Narration kwa uzuri kabisa kwenye #JE UTANIPENDA??
kwa kweli jamaa anaweza.
Na naishauri serikali tutumie mashairi ya Dangote kujibia Mitihani ya NACTE ya madogo wetu wa pramari,skonga na yuniveziti.
keeping it just up!! Chief bin Wasafi Dangete.
 
Kweli mtoa mada we ni lofa tena akili zisizo na akili.mtu kaishia darasa last saba afu huo mziki wa kihuni anaimba baada ya kuvuta bangi atunukiwe PHD? Ignorance is bliss

We ndio lofa kweli, hivi muziki wanaoimba ungekuwa si wa heshima kama unavyodai Wagombea urais wangekuwa wanawatumia kwenye kampeni??? Diamond alitumika na lowassa na JPM wote walielewa mchango wake wakaamua kusafiria nyota yake

Afu inaonekana ni mgeni kabisa kwenye suala la utoaji wa Phd ya heshima, hata kama hujasoma vidudu utapewa kutokana na mchango wako kwenye jamii

Unadharau wasanii, unafikiri kwanini kuna wizara inayohusu wasanii? je tokea tumepata uhuru Tanzania imepata heshima kwa kiwango kipi, na nani amehusika?
 
Naunga mkono hoja..

Ila tusisahau kuwa ametajwa kati ya ICONS OF THE NATION 13, tokea tumepata uhuru na hicho nadhani ni kikubwa kuliko hii PHD kwasababu atakumbukwa miaka na miaka na JINA LAKE LIPO NATIONAL MUSEUMS

Pia, wasomi UDSM mwaka huu walishamtunuku tuzo ya heshima kutokana na Inspiration anayotoa kwa vijana kupitia mziki wake

JE UTANIPENDA??
King Of Afropop
 
Kaimba na wasanii kibao wa kimataifa kwa kutumia lugha ya kiswahili katika song zake na za featuringishwa.Mufano Bracket ft Baba tifa-alive.
anatendea haki kabisa kwenye
UHAKIKI WA FASIHI SIMULIZI
na
LITERATURE IN ENGLISHMAN
na ametumia Flashback Narration kwa uzuri kabisa kwenye #JE UTANIPENDA??
kwa kweli jamaa anaweza.
Na naishauri serikali tutumie mashairi ya Dangote kujibia Mitihani ya NACTE ya madogo wetu wa pramari,skonga na yuniveziti.
keeping it just up!! Chief bin Wasafi Dangete.

Kabisa mkuu
 
DIAMOND anahadhi kubwa zaidi ya hiyo kama alivyosema Kidingi hapo juu,tena kwa kuongezea ni kwamba pia halishawahi kupata tuzo ya heshima inayotambuliwa kimataifa aliyoipata South Africa lakini si mbaya akaongezewa kwa vile anazidi kuipa heshima nchi yetu wazo zuri wahusika wamelisikia watalifanyia kazi kwa vile wanaona jitihada zake.
 
Last edited by a moderator:
Aongeze pesa na kusaidia jamii kama mzee Mengi then twaweza fikiria kumpa recognition certificate. Doctrine bado sana.
 
Ametoa mchango mkubwa sana katika ukuzaji wa lugha adhimu ya kiswahili barani Afrika na dunia kwa ujumla. Vyuo vya Tanzania mulikeni hili hasa hasa chuo kikuu cha Dar es salaam idara ya kiswahili mchango wa huyu ndugu yetu.

Hivi sisi wa Tz n nani aliyetulogaaaa
Kwa mchango upi haswaa diamond alioulete Tz hadi apewe PHD
Jamaa kaendelea katika tasnia yake hayo n mafanikio yake binafsiii.. hebu sema kupitia mafanikio yake ametengeneza ajira kwa watu wa ngapi? Zinazoonekana na zisizo onekana,, amechangiaje pato la Taifaa.. amegusa maisha ya jamiii kwa kiasi gani. Nini mchango wake wa wazi???
 
Unadhani PHD wanagawa Kama Maji ya bakhresa kwenye harusi,
 
Matatizo ya kuanzisha thread bar ndo haya sasa
 
Kizazi cha leo shida kweli. Unaijua thamani ya PhD wewe? Huko kupiga picha amejiviringishia hela ndo kunakuchanganya hadi unashauri apewe PHD. Mchango wake kwa jamii ni upi?
 
DIAMOND anahadhi kubwa zaidi ya hiyo kama alivyosema Kidingi hapo juu,tena kwa kuongezea ni kwamba pia halishawahi kupata tuzo ya heshima inayotambuliwa kimataifa aliyoipata South Africa lakini si mbaya akaongezewa kwa vile anazidi kuipa heshima nchi yetu wazo zuri wahusika wamelisikia watalifanyia kazi kwa vile wanaona jitihada zake.

Labda hao wahusika ziwe zimefyatu kama zako watampa.
 
Back
Top Bottom