Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Kwanza mbele za Mungu ni wapi?? Au unadhani kila mahali ni Mbele za Mungu? Ili kuwe Mbele za Mungu kuna Kanuni zake.Yesu anatibu roho na automatically mwili pia unapona.
Barakoa haitibu chochote ni ushuhuda wa uwoga mbele za Mungu..... Lakini ukiwa Bar vaa barakoa maana huko ni makao ya shetani!
Unadhani Yesu alivopindua zile Meza pale Hekaluni Ibada zilikuwa haziendelei? Na wao pia pamoja na Uchafu wao wote uliokuwa unaendelea bado walijiona kwamba wapo Mbele za Mungu!!
Ndio maana Yesu alijua kwamba si kila anayejiona yupo mbele za Mungu ni kweli kwamba yupo Mbele za Mungu na akasema "si kila anaiitae Bwana, Bwana, Ataingia kwenye ufalme wa Mungu!".
Yuda naye si alikuwa "mbele" za Mungu lakini hakuwa na Mungu.